Ni nini kinachosumbua Maalim Seif?

Ni nini kinachosumbua Maalim Seif?

Hebu tuacheni tupumue, hatulitaki hili dubwasha liitwalo muungano, Watanganyika mnachekesha, nyinyi mmejaaliwa ukubwa wa ardhi lakini badi mnaingangania Zanzibar. Kaeni na Tanganyika yenu tuachieni Zanzubar yetu tuchachoka na chokochoko zenu

Fumu, mimi binafsi sipendi ushirikiano wa kubembeleza mtu tuwe na uhusiano. Najua asilimia kubwa ya Wa-Zanzibar hawataki Muungano, na sipendi kabisa kuona wanaendelea kuwa katika kitu wasichokitaka. Nadhani hata huku bara watu wameshoshwa na vituko vya Zanzibar, na hakuna anaewataka. Tuwabembeleze kwani sie tunafaidika nini na Zanzibar ati? Kama ni mafuta huenda tunayo mengi kuliko yanayoweza kuwa Zanzibar, na wala hamna uhakika kama kweli yamepatikana.

Ila utashi wangu ni kwamba, ikiwa tunakubaliana kuvunja muungano basi mambo yafuatayo yanzingatiwe;

1. Ili kuzuia uwezekano wa kuja kunyanyaswa hapo baadaye, Watanzania bara waliko Zanzibar warudi kwao bara na wale walioko bara warudi kwao Zanzibar. Serikali zitakubaliana jinsi ya kuwarudishia mali zozote zisizohamishika walianzazo huko, ikiwa watashindwa kuziuza. Wale walioona kati ya Watanzania Bara na Visiwani wataruhusiwa kuchagua wanataka kuishi wapi.

2. Tanzania bara, ambayo iliacha kutumia jina Tanganyika huko nyuma iwe na uhuru wa kuendelea kutumia jina Tanzania ikitaka, kutokana na "branding" ambayokwa kiasi kikubwa imefanywa na Tanzania bara, na pia kwa kuwa Tanzania bara kuendelea kutumia jina Tanzania hakutaiathiri Zanzibar kwa namna yoyote. Tanzania inaweza pia kuchagua jina lolote jingine.

3. Mpaka wa baharini kati ya Zanzibar na Tanzania bara uwekwe kwa kufuata kanuni ya "international midline"

4. Utaratibu wa visa kati ya Tanzania Bara na Visiwani uanze mara moja ili kudhibiti muingiliano wa watu usio na uaratibu
 
Mkuu Synthesizer, umefika wakati tuite koleo kwa jina lake: kwangu mimi Maalim ni mtu mbinafsi, mnafiki, egoist and a remarkable genius. Sijapata maneno halisi ya kiswahili kwa baadhi ya hizo sifa zake. Nadhani inatosha kutoa majibu kwa mshangao uliouelezea kwenye mada yako.
 
Kila ninaposikia kauli za Maalim Seif juu ya Muungano, ninapata picha kwamba zinazotelwa na mtu mwenye hasira sana dhidi ya serikali ya Tanzania, hususa Tanzania Bara. Sizioni kauli za Seif kama zinazotolewa na mzalendo wa Zanzibar, bali kama zinazotolewa na mtu mwenye hasira ya kisasi dhidi ya watu fulani. Katika kauli zake nyingi zimejaa "exaggeration" za hali ya juu, za aina ya mtu ambaye anataka kuwakomoa watu au kikundi fulani.

Sasa najiuliza, ni nini kinachomsumbua Maalim Seifu hadi kuwa na hasira ya namna hii?

Ni wazi kwamba si uzalendo wa kuwa M-Zanzibar. Kumbuka kwamba Seifu alitoa mchango mkubwa kwenye kuwajibishwa kwa Abdu Jumbe. Sefu alimchukulia Jumbe kuwa msaliti wa Muungano. Seifu ni mojawapo ya Wazanzibar waliofaidi na kuneemeka sana na Muungano. Bila muungano Seifu asingekuwa hapo alipo. Sasa ni nini kilimbadili Seifu? Je ni hasira baada ya kugundua ndoto yake ya kuwa Raisi wa Zanzibar isingetimia kupitia CCM? Au ni baada ya mashitaka na tuhuma alivyofanyiwa huko nyuma na sasa anataka kisasi?

Kuna mambo Seifu anataja kama faida za Zanzibar kujitoa kwenye Muungano ambayo ukifikiria utaona kwamba anawadanganya WaZanzibar kwa kuwa hayatawezekana, hata kama kweli watajitenga na muungano, kwa kuwa ni ndoto za alinacha, hayako "realistic". Sasa je, Maalimu Seifu anaona kwamba anaingia uzeeni na sasa kuna dalili kwamba kamwe hatakuwa raisi wa Zanzibar na hivyo anaona ni bora tu alivuruge?

Ni nini kinachompa hasira hii Maalim Seifu, na lengo lake ni nini hasa?

Cc Barubaru
 
Last edited by a moderator:
Zanzibar in a siri nyingi!, tafuta kisa cha Sultan kumpachika ujauzoto mjakazi wa mkewe, ili kuficha siri, huyo mjakazi alikwenda kuozeshwa mahali mbali chap chap!, baadaye, mwana sulatan alizaliwa huko mjakazi alikoolewa!. Find out huyo mwana sulatan ni nani?!, tafuta uhusiano kati ya Sultanet ya Brunei na Sultanet ya Zanzibar!, find out who funds CUF and why?!.

Kwa taarifa tuu, CUF ilishinda 1995, ikashinda tena 2000!, pia ikashinda 2005!, na kushinda tena 2010 lakini kote kwa nini hawampi ushindi?!.

Visa vya Zanzibar havikuishia hapo, kuna ndugu tena wengine wawili, watoto wa baba mmoja, mama mmoja, tumbo moja!. CCM ikaamua kumzawadia urais kaka mkubwa, kisa ni kumuenzi baba yao aliyoifanyia makubwa Zanzibar, hivyo ule urais ulikuwa ni wa zawadi ya heshima ya marehemu babsa yao!. Baada ya kaka mtu kumaliza kipindi chake cha urais cha miaka 10!, mdogo mtu akachukua fomu kumrithi kaka mtu!. Chama kikamshauri, kwa vile aliyemaliza ni kaka yake wa tumbo moja, baba mmoja, mama mmoja!, hivyo kumpitisha mdogo mtu, itaonekana kama usultani!, mdogo mtu akagoma na kuibuka na madai mazito!, kuwa eti kama urais ni zawadi kwa mtoto wa yule Mzee waliomuheshimu, then "mtoto halisi aliyestahili ni yeye!".

Zanzibar haieshi vituko!, nataka niwashauri wajumbe wa bunge la katiba kuhakikisha Mwenyekiti wa kudumu anakuwa Mzanzibari, ili hoja ya serikali tatu ikishindwa, ije hoja ya serikali moja ndio itaimarisha haswa muungano na kuwakata kabisa hawa vilimimili na vitimbakwiri vya kutaka kuuvunja huu Muungano wetu adhimu, uliotokana na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.

Mapinduzi Daima!.
Muunganno Milele!.
Pasco

Umezidisha filfil
 
Kila ninaposikia kauli za Maalim Seif juu ya Muungano, ninapata picha kwamba zinazotelwa na mtu mwenye hasira sana dhidi ya serikali ya Tanzania, hususa Tanzania Bara. Sizioni kauli za Seif kama zinazotolewa na mzalendo wa Zanzibar, bali kama zinazotolewa na mtu mwenye hasira ya kisasi dhidi ya watu fulani. Katika kauli zake nyingi zimejaa "exaggeration" za hali ya juu, za aina ya mtu ambaye anataka kuwakomoa watu au kikundi fulani.

Sasa najiuliza, ni nini kinachomsumbua Maalim Seifu hadi kuwa na hasira ya namna hii?

Ni wazi kwamba si uzalendo wa kuwa M-Zanzibar. Kumbuka kwamba Seifu alitoa mchango mkubwa kwenye kuwajibishwa kwa Abdu Jumbe. Sefu alimchukulia Jumbe kuwa msaliti wa Muungano. Seifu ni mojawapo ya Wazanzibar waliofaidi na kuneemeka sana na Muungano. Bila muungano Seifu asingekuwa hapo alipo. Sasa ni nini kilimbadili Seifu? Je ni hasira baada ya kugundua ndoto yake ya kuwa Raisi wa Zanzibar isingetimia kupitia CCM? Au ni baada ya mashitaka na tuhuma alivyofanyiwa huko nyuma na sasa anataka kisasi?

Kuna mambo Seifu anataja kama faida za Zanzibar kujitoa kwenye Muungano ambayo ukifikiria utaona kwamba anawadanganya WaZanzibar kwa kuwa hayatawezekana, hata kama kweli watajitenga na muungano, kwa kuwa ni ndoto za alinacha, hayako "realistic". Sasa je, Maalimu Seifu anaona kwamba anaingia uzeeni na sasa kuna dalili kwamba kamwe hatakuwa raisi wa Zanzibar na hivyo anaona ni bora tu alivuruge?

Ni nini kinachompa hasira hii Maalim Seifu, na lengo lake ni nini hasa?

pole sana kwa kujitia wazimu kichwani., hiyo ndio khofu yenu kwamba maalim akiwa rais zanzibar atamleta mwarabu na kurudisha utumwa lakini pia muna wasiwas kwa udhalim munaoendelea kuufanya CCM kwamba maalim akipata madaraka atakufungeni jela na kuvunja Muungano, ndio upeo wenu wa mawazo hamlaumiki muna akili za samaki

Maalim kuzeeka au kutokuwa rais Zanzibar kutokana na umri isikupe homa., kwanza ufahamu maalim tayari ameshafanya kazi kubwa sana kuwaunganisha wazanzibari, na tayari ndoto zake zimekamilika kabla hatukuwa hivi, zamani ilikuwa ukiutaja muungano ilikuwa ni uhaini au kufungwa jela watu waliekewa mkono wa chuma wasiutaje muungano na kuubugudhi, sasa muungano wazanzibari wanapiga kelele hawautakii., na lazima utaenda na maji tu ww unajuwa.,

Kabla ya CUF hakukuwa na mfumo wa vyama vingi Tz, wala chama cha upinzani chenye nguvu kama CUF, CUF ndio iliyowaamsha watanzania ambao walikuwa wamelala usiku wa manane saivi kila kitu kipo tayari bado siku na saa tu CCM iage dunia., hayo ni mafanikio makubwa sana mkuu. Jengine saivi Zanzibar kuna serikali ya umoja kitaifa ni juhudi zake ww upo upo tu.,

Maalim Seif ni binadama kama mimi na wewe., akiondoka ndio kwanza shughuli inaanza sasa viongozi majasiri na shupavu tunawo wengi sana muhimu kwanza yeye mwenyewe atamke kuachia ngazi kutokana na umri.

Zanzibar kihistoria ni nchi iliyotawaliwa na Mwarab tumerithi mengi kwa waarab hatuwezi kujibadilisha tukawa na ngozi ya kinyamwezi au kisukuma na kimasai, uarabu sisi ndio makabila yetu yamo ndani ya mishipa yetu ya damu lakini kwa nini mupate joto na hataka akirudi huyo mwarabu atarudi zanzibar lakini si Tanganyika.,

Sasaivi mumegundua Zanzibar haitaki tena kuburuzwa muna tapatapa tu., chuki, kibri mara Maalim seif ana hasira ndio wazimu wenyewe huo sasa mumechanganyikiwa
 
Mtasema sana ,ila talatibuni ,Maalim kwa taarifa yenu anagombea tena ,yaani kibara tunasema mpaka kijulikane ,sasa mwanasiasa anaejua siasa ni yule anaezungumza kwa hasira ,na huyo ndie anaepata wasikilizaji kwani huwakoleza vibaya sana,kama utachunguza siku hizi wengi wa wanaopanda kwenye jukwaa la kisiasa wote karibuni wameanza kufuata nyayo za Maalim Seif ,kwani ni ngangari ndio inayosikilizwa na Zanzibar wameweza na sasa wametia mguu mmoja ndani ya Ikulu.

Na kuhusiana visa mnavyoviita vya siri ,mkianzia kwa Mfalme mpaka hapa tulipo ,inawezekana huko kuna visa vikubwa sana hivi mliangalia ITV jana ,jamaa kabaka mtoto wa miaka saba huko bara ,habari zimepelekwa polisi eti polisi wametoa dhamana na jamaa anavuruga mitaani na visa hivyo ni vingi huko kwenu ,kwani ukiwa na hela utafanya visa kibao tena vya
hali ya juu.

Kuhusu Jumbe huna unalolijua ,kafukuzwa na Nyerere au Seif ? Hivi wakati wa Nyerere Seifu angeweza kumfukuza au kumsaliti mtu na akafukuzwa au kuondolewa wadhifa wake ?

Kuhusu Muungano aloo kusema kweli hakuna anaeutaka mwanzo ilikuwa huko Zanzibar tu lakini leo hii hata huko Bara kelele ni hizo hizo ,Muungano hawautaki ,kwani ni njia ambayo WaCCMwanaitumia kukaa madarakani ,subirini tu mtasikia hili bunge la Katiba linavunjika kabla ya kufikia mwisho kwani hakuna anaetaka serikali mbili isipokuwa wahafidhina wachache wa CCM,huenda wakaachiwa hilo bunge wafabricate na kufanya wanavyotaka wao.
 
Mkuu Synthesizer, umefika wakati tuite koleo kwa jina lake: kwangu mimi Maalim ni mtu mbinafsi, mnafiki, egoist and a remarkable genius. Sijapata maneno halisi ya kiswahili kwa baadhi ya hizo sifa zake. Nadhani inatosha kutoa majibu kwa mshangao uliouelezea kwenye mada yako.

Mtafutieni kila majina mumpe lakini roho inakuumeni sn., ndio yeye aliyewaamsha watanzania kutoka kiza kinene na kuelekea kweupeni., kumchukia ww na familia yk is good for nothing., we respect him, we support him very much.,

Nyinyi tengenezeni midoli ya Julius Nyerere mueke majumbani mwenu muiyabudu tena mukimuomba kwa shida zenu., Judder!
 
Mkuu, nakuunga mkono kikamilifu katika mtazamo wako. Ninachosisitiza na naamini utanikubalia; Maalim ni kichwa hasa - a GENIUS. Maelezo yako yanazidi kunithibitishia. Sijui kama unataka kukataa hilo. Mimi binafsi huwa siabudu mtu awaye yeyote yule hata awe wa kiwango cha Julius Nyerere. Lakini huwa navitambua vichwa - ila marufuku kuviabudu. Ushauri wangu kwako nawe ujipime ujue umesimamia wapi.
 
Zenji na mnavyozaana kama panya...... mkijaa humo baada ya muungano kuvunjika mtaishi majini kama samaki:sly::sly:
 
mi nafikiri tuuvunje muungane na tuwe na visa.......hii itatusaidia Tanganyika kufanya biashara na Zanzibar ya bidhaa nyingi sana na kuongeza kiwango chetu cha mapato

soko liliko wazi kabisa.....UMEME,mbao,cement,vyakula na bidhaa zote itozwe kodi maana zitakuwa zinatoka nje ya nchi
 
Hebu tuacheni tupumue, hatulitaki hili dubwasha liitwalo muungano, Watanganyika mnachekesha, nyinyi mmejaaliwa ukubwa wa ardhi lakini badi mnaingangania Zanzibar. Kaeni na Tanganyika yenu tuachieni Zanzubar yetu tuchachoka na chokochoko zenu

Ongezeni nguvu basi katika kuidai, wadhani is wenyewe twautaka huu muungano? Ni wachache tu ndio wanaoulilia tenA kwa manufaa Yao.
 
pole sana kwa kujitia wazimu kichwani., hiyo ndio khofu yenu kwamba maalim akiwa rais zanzibar atamleta mwarabu na kurudisha utumwa lakini pia muna wasiwas kwa udhalim munaoendelea kuufanya CCM kwamba maalim akipata madaraka atakufungeni jela na kuvunja Muungano, ndio upeo wenu wa mawazo hamlaumiki muna akili za samaki

Kutokana na kauli kama hizi zako, pia nimegundua kwamba wengi huko Zanzibar mnaopiga sana kelele kwamba hamuutaki muungano ni malofa tu wa mitaani msio na mbele wala nyuma kimaisha, na wala haina maana kwamba muungano ukivunjika hali zenu kimaisha zitakuwa bora. Kama sio malofa basi ni wale limbukeni wa madaraka. Mnadhani kwamba muungano ukifa basi hali zenu zitakuwa bora sana, wavivu nyie. Wengi wenu mtaendelea kuwa malofa na huenda mkawa ndio chanzo kikubwa cha machafuko yatakayotokea Zanzibar baada ya kuwa mmejitenga na bara.

Ukweli ni kwamba natamani sana muungano uvunjike ili angalau nithibitishwe, mimi na watu wengine kama kina Nyerere, kwamba tulikosea kudhani Zanzibar haitakuwa shwari baada ya muungano kuvunjika.

So bring it on, na tuuvunje muungano.
 
Fumu, mimi binafsi sipendi ushirikiano wa kubembeleza mtu tuwe na uhusiano. Najua asilimia kubwa ya Wa-Zanzibar hawataki Muungano, na sipendi kabisa kuona wanaendelea kuwa katika kitu wasichokitaka. Nadhani hata huku bara watu wameshoshwa na vituko vya Zanzibar, na hakuna anaewataka. Tuwabembeleze kwani sie tunafaidika nini na Zanzibar ati? Kama ni mafuta huenda tunayo mengi kuliko yanayoweza kuwa Zanzibar, na wala hamna uhakika kama kweli yamepatikana.

Ila utashi wangu ni kwamba, ikiwa tunakubaliana kuvunja muungano basi mambo yafuatayo yanzingatiwe;

1. Ili kuzuia uwezekano wa kuja kunyanyaswa hapo baadaye, Watanzania bara waliko Zanzibar warudi kwao bara na wale walioko bara warudi kwao Zanzibar. Serikali zitakubaliana jinsi ya kuwarudishia mali zozote zisizohamishika walianzazo huko, ikiwa watashindwa kuziuza. Wale walioona kati ya Watanzania Bara na Visiwani wataruhusiwa kuchagua wanataka kuishi wapi.

2. Tanzania bara, ambayo iliacha kutumia jina Tanganyika huko nyuma iwe na uhuru wa kuendelea kutumia jina Tanzania ikitaka, kutokana na "branding" ambayokwa kiasi kikubwa imefanywa na Tanzania bara, na pia kwa kuwa Tanzania bara kuendelea kutumia jina Tanzania hakutaiathiri Zanzibar kwa namna yoyote. Tanzania inaweza pia kuchagua jina lolote jingine.

3. Mpaka wa baharini kati ya Zanzibar na Tanzania bara uwekwe kwa kufuata kanuni ya "international midline"

4. Utaratibu wa visa kati ya Tanzania Bara na Visiwani uanze mara moja ili kudhibiti muingiliano wa watu usio na uaratibu
Tanganyika inakuwasha nini hadi ushindwe kuitamka wazi wazi na kutumia jina la Tanzania bara? Huwa napata hasira na kichefuchefu pale ninapokuta mtu analazimisha kuibatiza Tanganyika kuwa Tanzania bara. Mbona Zanzibar wao hawaionei nchi yao aibu wakaiita Tanzania visiwani? Tupunguze ujinga na tuthamini historia yetu na utaifa wetu. Pointi yako No: 2 hapo juu ni utumbo mtupu
 
Zenji na mnavyozaana kama panya...... mkijaa humo baada ya muungano kuvunjika mtaishi majini kama samaki:sly::sly:

Huko mnazalishana kama manguruwe muungano ukifa mtaishi mwituni aka mbugani kama Nungunungu:loco:.
 
pumba.
kwa nini usitueleze hicho anachokisema sefu? wewe unafikiri sisi wote tunajua unachofikiria? halafu futa hiyo kauli yako ya kusema eti bila ya muungano sefu asingekuwa hapa alipo. si ajabu angekuwa hata zaidi ya hapa, who knows?

Back
Top Bottom