nadhani naweza kujadili mahakama ya kadhi ingawa naona nalazimishwa kutoa hoja wakati nikiendelea kutafiti kuhusu extent ya kile kinachoitwa udini katika taifa letu.
Naomba wakuu mnipe muda mtaburudika na kujifunza mengi na kwa vile ni topici tete[sensitive topic]naomba mnipe time nitawajibu.
Ila kwa sasa ninayo machache:
inaonekana kabisa watu wanachanganya baina ya mahakama ya kadhi na mfumo wa mahakama nchini au zile zinazoitwa mahakama za kiislamu kwa mujibu wa sheria kamili za dini hiyo ya kiislamu kama katika maeneo ya somalia na kwingineko.
Nielewavyo mahakama ya kadhi iliwahi kuwepo huko nyuma ikifanya kazi sambamba kabisa na mfumo wa sasa, hii mahakama kadhi yake ni kutoa suluhisho kwa mambo ya kawaida ya waislamu kama vile matatizo ndani ya ndoa hadi kufikia talaka!mirathi na mengineyo. sina hakika sababu hasa zilizopelekea mahakama hiyo kufutwa lakini sidhani kama it is anything to do with political unity manake haina uwezo wa kugawanya watu kiimani kabisa.
Kule zanzibar mahakama ya kadhi bado ipo na inaexist kikatiba kabisa ya zanzibar lakini mtu anaweza kucounter argue kwamba kadhi wa zanzibar ni presidential appointee[very strange!] na bajeti yake ipo hasa katika mfuko wa jamii zanzibar.
sasa nipo puzzled kiasi na suala kwa sababu mbili:
1. maaskofu wtu hawa hawa wakati wa kampeni waliwahi kusema kikwete ni chaguo la mungu,walifanya hivyo ilhali walikuwepo viongozi ambao naamini ni wakristo katika kinyang'anyiro cha urais kama vile mbowe, mrema na wengineo lakini hawakufanya ajizi wala udini wakadai ni chaguo la mungu, sijui maaskofu wetu hawakuisoma ilani ya chaguo la mungu au walivutiwa na mgombea tu na sio anayoyaahidi manake kama wangesoma wangeona kuwa CCM imeahidi kuweka mahakama ya kadhi!
2.Naona ukiangalia katika waislamu wengi wenye uelelewa wa kawaida utaona kwamba katika vitu ambavyo huwa wananung'unika dhidi ya serikali, mahakama ya kadhi haimo kabisa katika orodha, awali wakati wa uchaguzi nilidhani hii ni ajenda ya ccm kutaka kuonesha kwamba wapo beneti na waislamu lakini sasa naona inaprove ngumu kwao ikiwa waziri mary nagu anaetakiwa kusimamia ilani ya ccm katika mfumo wa sheria anapogwaya na hilo
Hivyo nadhani kuna a bit of dilemma in terms ya walioandika na wanachokidai maaskofu lakini ni wajibu wao kuionya serikali ksama viongozi wa kijamii natumai wametumia haki yao ya msingi kikatiba kutoa maoni hayo.
Just a piece of ushauri kwa viongozi wetu wa kidini, tusikurupuke kuwapa viopngozi wetu wa kisiasa hadhi za kiimani kwani politics ni mchezo tofauti kabisa na pili kwa viongozi wetu tulenge katika umoja zaidi kuliko kuserve individual interests!
naomba kutoa hoja