CCM: Ilani Ya Uchaguzi 2005-2010

Apr 27, 2006
12,621
1,241
Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania, Kwa Ari mpya, Nguvu Mpya NA Kasi Mpya,
Tanzania yenye neema tele inawezekana,

UTANGULIZI: 1

(8). Jukumu la kwanza ni kuitoa Tanzania kutoka kwenye dimbwi la uchumi ulio nyuma na tegemezi na kuiingiza katika mkondo wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea.

: Jukumu hilo ni letu Watanzania, wahisani wanatuunga mkono tu!

Jukumu la pili ni kuwashirikisha wananchi wote kwa njia ya uwezeshaji katika ujenzi wa uchumi na kutokomeza umasikini!

(9). Ilani hii ni kielelezo cha dhamira ya CCM ya kuiendeleza kazi nzuri iliyokwisha kufanywa na serikali ya awamu ya tatu ya rais Mkapa. Ikichaguliwa tena, CCM itahakikisha kwamba serikali ya awamu ya nne inaendeleza kazi ya kukuza uchumi na kupambana na umasikini wa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.


Wananchi Mnasemaje, hebu tuichambue kwa kina hii Mazingaombwe!
 
Wahisani wanatuungaje mkono wakati wao ndio wanaotoa 50%, ya bajeti yetu?

Ni lini tutajitoa kwenye uchumi tegemezi, wakati tunatumia billions kununua ndege moja tu ya rais?, pesa ambazo zingetumika kuanzishia benki ya maendeleo ya wananchi na kuondokana na uchumi tegemezi?

Eti kuendeleza dhamira nzuri ilianzwa na awamu ya tatu? Ipi hiyo?
 
Mzee Es haya ni maswali ambayo sisi Wananchi tunawauliza wanachama wa CCM ambao ndiyo wana serikali . Je wamewaeleza walio wapa kura ukweli kwamba serikali haina mpango wa kumkomboa mwanananchi kimatendo bali kwa maneno , na hotuba nzuri na kuipigiwa makofi? Wanatuunga mkono maana wanataa watuuzie ndege ili warudishe pesa zao wanazo tuungia mkono. Ndilo nalo ona hapa kwamba kuna plans za ajabu sana lakini wacha na mimi niangalie mwelekeo tutaishia wapi maana mwaka 2010 si mbali .
 
Mugishwagwe

Mimi pia huwa najiuliza hivi inakuwaje kwa rasilimali tulizonazo tuwe tunategemea 50 pc ya bajeti yetu itoke nje?

Mfano wangu siku zote ni kama mtu aliamua kuanza kujitegemea (uhuru 1961) halafu iwe kaoa nk then 50 pc ya gharama zake za maisha ziwe zinatoka kwa mtu mwingine kama ikitokea siku akataka na yeye ajiridhishe kidogo kwa mkeo utakuwa na ugumu kukataa!

Sasa kwa nchi ambayo kuna 'wahisani' wanaotufadhili inakuwa tabu sana kuendelea.

Kuna sababu zozote kwa nini hatuendei?

moja ya matatizo ni kuwa na viongozi ambao hawaonekani kukerwa na ukweli kuwa nchi yetu ipo nyuma, niliwahi kuandika katika magazeti kuwa tumekuwa na watendaji ambao wanaonekana kufanya kazi perfunctorily yaani kutekeleza wajibu wao wa kawaida badala ya kuwa wabunifu kuhakikisha tunasonga mbele, watendaji wanaofanya kazi kwa mtindo wa business as usual hawana nafasi katika kura yangu au hata niseme chama ambacho kinaendelea na utaratibu huo kura yangu itakuwa shubiri kwao.

Kwa sasa slogan ya ccm inatia moyo, kuleta maisha bora ya watanzania kwa ari mpya na kasi mpya na nguvu mpya! hawa wanasema business not as usual bali kwa mwelekeo mpya kabisa! tunasubiri tuone lakni based on what i have heard so far ni kuwa wanatalk the talk let us see them walk the walk.

yetu macho.
 
Tafit ,

Nimekuwa nikisoma michango yako mingi na kusema ukweli ninavutiwa sana , ila tatizo moja umekuwa ukisema mara kwa mara kuwa tuwape muda hawa viongozi . Swali kwangu kwako tuwape muda mpaka lini ? Na kwanini tuendelee kuwapa muda wakati tunaona our vessel is heading in the wrong direction ?
 
good point, mimi nadhani nitaanza kuwakosoa haswa kwa kushindwa kudeliver baada ya kuwa mwaka mmoja madarakani then nifanye tathmini ya kipi wamefanya, sasa hivi ni mapema kwa vile si unaona rais hata uteuzi bado hajamaliza!
 
Mzee wa Utafiiiiitiiiiiiiii,

Vipi hii article hapo juu, imefanyiwa utafiti au watu wanajadili tuuuu? Na hili kanisa vipi, mbona wana haraka hawa ya kuhukumu nabii wetu kabla ya mwaka mmoja kuisha?

Halafu wanasema eti rais anawabeba nani? Au huyu mwandishi ni mtu wa hii forum?
 
Mzee Es
Hii ndiyo CCM yako .Viongozi wake wana hadaa umma na kuitwa Nabii sasa wanakaribia kujua ukweli wanausema kwamba si haki , kwamba anawabeba watu fulani , ndiyo ilani ya CCM na ndiyo mengi kati ya machache ambayo Chama chako kinayafanya watu wanaanza kuamka sasa wanadhani jamaa ni Nabii bali mtu na interest zake .Mimi sikuwahi kukataa ubora wa Sera za CCM shida yangu iko kwenye kutekeleza tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
There we go...

Makanisa na hawa maaskofu walikuwa kimbelembele kusema JK ni nabii..chaguo la Mungu.. Sasa waache nabii afanye kazi yake.

ES, naomba tuungane na wanabodi tuanzishe topiki mpya ya " nini kifanyike serikali iache kuwa tegemezi" tukisha maliza Filgga aandae summary ipelekwe kunakohusika.

Ilani za CCM zilikuwa ni za kununua/kuomba kura toka kwa wananchi, Nothing else, ukiwaambia hazitekelezeki wanakuona sio mwenzao!! hilo ndio tatizo letu bongo, na hii inatokea kwasababu wananchi wengi ni mbumbumbu!! Maoni yangu ni kuwa baada ya miaka 15, CCM itakuwa na kazi saana kuomba kura za wananchi!!, mimi ni mwana CCM, ila kwa kasi hii Meli yetu itagonga mwamba 2020.
 
nadhani naweza kujadili mahakama ya kadhi ingawa naona nalazimishwa kutoa hoja wakati nikiendelea kutafiti kuhusu extent ya kile kinachoitwa udini katika taifa letu.

Naomba wakuu mnipe muda mtaburudika na kujifunza mengi na kwa vile ni topici tete[sensitive topic]naomba mnipe time nitawajibu.

Ila kwa sasa ninayo machache:

inaonekana kabisa watu wanachanganya baina ya mahakama ya kadhi na mfumo wa mahakama nchini au zile zinazoitwa mahakama za kiislamu kwa mujibu wa sheria kamili za dini hiyo ya kiislamu kama katika maeneo ya somalia na kwingineko.

Nielewavyo mahakama ya kadhi iliwahi kuwepo huko nyuma ikifanya kazi sambamba kabisa na mfumo wa sasa, hii mahakama kadhi yake ni kutoa suluhisho kwa mambo ya kawaida ya waislamu kama vile matatizo ndani ya ndoa hadi kufikia talaka!mirathi na mengineyo. sina hakika sababu hasa zilizopelekea mahakama hiyo kufutwa lakini sidhani kama it is anything to do with political unity manake haina uwezo wa kugawanya watu kiimani kabisa.

Kule zanzibar mahakama ya kadhi bado ipo na inaexist kikatiba kabisa ya zanzibar lakini mtu anaweza kucounter argue kwamba kadhi wa zanzibar ni presidential appointee[very strange!] na bajeti yake ipo hasa katika mfuko wa jamii zanzibar.

sasa nipo puzzled kiasi na suala kwa sababu mbili:

1. maaskofu wtu hawa hawa wakati wa kampeni waliwahi kusema kikwete ni chaguo la mungu,walifanya hivyo ilhali walikuwepo viongozi ambao naamini ni wakristo katika kinyang'anyiro cha urais kama vile mbowe, mrema na wengineo lakini hawakufanya ajizi wala udini wakadai ni chaguo la mungu, sijui maaskofu wetu hawakuisoma ilani ya chaguo la mungu au walivutiwa na mgombea tu na sio anayoyaahidi manake kama wangesoma wangeona kuwa CCM imeahidi kuweka mahakama ya kadhi!

2.Naona ukiangalia katika waislamu wengi wenye uelelewa wa kawaida utaona kwamba katika vitu ambavyo huwa wananung'unika dhidi ya serikali, mahakama ya kadhi haimo kabisa katika orodha, awali wakati wa uchaguzi nilidhani hii ni ajenda ya ccm kutaka kuonesha kwamba wapo beneti na waislamu lakini sasa naona inaprove ngumu kwao ikiwa waziri mary nagu anaetakiwa kusimamia ilani ya ccm katika mfumo wa sheria anapogwaya na hilo

Hivyo nadhani kuna a bit of dilemma in terms ya walioandika na wanachokidai maaskofu lakini ni wajibu wao kuionya serikali ksama viongozi wa kijamii natumai wametumia haki yao ya msingi kikatiba kutoa maoni hayo.

Just a piece of ushauri kwa viongozi wetu wa kidini, tusikurupuke kuwapa viopngozi wetu wa kisiasa hadhi za kiimani kwani politics ni mchezo tofauti kabisa na pili kwa viongozi wetu tulenge katika umoja zaidi kuliko kuserve individual interests!

naomba kutoa hoja
 
Kenya kuna ofisi ya kadhi Mkuu kwa miaka mingi, nahisi kuna haja ya kuangalia inawork vipi na whether imeleta mgawanyiko au hatari zozote za kidini.
 
Kulikoni
Kenya ni Nchi huru sawa na Tanzania . Kwa hiyo unasema kama Kenya wanaua watu na sisi tuue ama ? Kuanza na mahakama ya kadhi mwishowe tuta tangaziwa sharia . Je nani atamlipa huyo kadhi wako na Mahakama yake na mahakimu wake ? Je watu tena ambao ni waislam wakishindwa kupata suluu huko wanaweza kuja Mahakama ya kawaida ? Zanzibar achana nako karibia wote ni waislam kule na si Tanzania bara ndugu .OK mnataka Mahakama ya waislam na walipa kodi ambayo si waislam hawako tayari pesa yao imtunze kadhi wenu unasemaje ? OK wakristo nao wana andaa muswada sasa endeleeni na kutekeleza ilani zenu za Uchaguzi mtuletee vita .
 
Mugishagwe,

Simaanishi kuwa kila linalofanywa na Kenya nasi tuige. Nilitoa mfano tu wa Kenya kuwa wanayo Ofisi ya Kadhi Mkuu na haijaleta hayo matatizo yanayoogopwa, ina co-exist na mahakama nyinginezo poa tu. Wana matatizo yao mengine ya kikabila n.k. Na nlitoa mfano huo sio kushabikia muswada huo (as I am not really sure if Tz is ready for it right now), bali ni kwa kuona kuwa mwandishi wa article iliyotumwa hapo juu amekwenda mbali sana kulinganisha suala hili na mambo ya Israel/Palestine, Sudan/Darfur etc. Sijabahatika kupitia huo muswada bali nnavyoelelwa ni kuwa mahakama za kadhi ni kwa masuala ya ndoa, talaka, mirathi n.k pale ambapo wahusika wote wamekubali zitumike taratibu za kiislamu.

Mambo mengine yanaogopwa sana bila kufanyiwa utafiti, kama suala la OIC lilipigiwa kelele mno eti kujiingiza ni kuifanya nchi kuwa ya kiislam ilhali Uganda, Msumbiji etc ni members wa OIC na wala si nchi za kiislam, na wala hazijaekewa masharti kuwa lazima zibadilike kuwa za kiislam.. hata wanaoattend mikutano sio masheikh wao bali ni mawaziri na viongozi wao wengineo ambao wengi wao hata sio waislam. Nchi zao zinafaidika na mipango na misaada kadhaa ya kiuchumi ... it has nothing to do with plans to implement 'Sharia' kwa nchi wanachama.

I would agree kuwa when the issue is too sensitive kwa wananchi wa kawaida, kwa kutokulielewa kwao, si vizuri ku go ahead mpaka likae sawa.
Just like we we should not be rushed into EAC kabla wanacnhi wa kawaida hawajaelewa how it is going to work yet. Inaweza kuja leta matatizo kama ya muungano wa sasa kuwa vipengele na mipaka yake havieleweki.

Waandishi wetu wangetoa facts na sio kuyakuza mambo na kuchochea tu.
 
Hili suala la Mahakama ya Kadhi ilikuwa na agenda ya KICHAA MREMA!!!

NA BAADA YA HAPO KAIDI BMW AKAIRUKIA BILA KUICHAMUBA NA AKAAMUA KUIFANYA AGENDA YA CCM KWENYE ILANI!!!!

WA KULAUMU NI MKRISTU MKAPA NA SIYO KIKWETE!! NINAONA WENZANGU WANAMLAUMU JK. TUSIPOKUWA MAKINI KATIKA KUCHAMBUA NA KUWEKA MAMBO WAZI NA SOURCE ZAKE. TUNAWAPA WATU MWANYA WA KUTUITA WALALAMIKAJI!
TUWE MAKINI. BMW AMELAANIWA TU KATULETEA TAABU KUBWA Tanzaniaza kidini , ukanda to mention but a few.

unaweza hata wakati mwingine kuquestion kifo cha JKN KATIKA UTAWALA WAKE?
 
Mkwawa
salaam mkuu . Naomba kutofautiana nawe kwenye hili . Mkapa akatupeleka pabaya ndiyo lakini kwenye ilani ya mwaka 2005 hahusiki maana hakuwa mgombea wa Urais wa Ubunge. Hili ni jambo la JK na CCM yote maana wao ndiyo walitengeneza ilani yao ili waiuze . Hii ni baada ya kuona damage kwa waislam nadhani kuanzia mambo ya mwembechai nk .Mrema alianza lakini kama kawaida CCM have hijacked sera nyingi za wapinzani wakaruka na hii bila kujiuliza .Leo sasa tuna hii shida . Hii ni CCM yoye na si Mkapa maana hakuwa mgombea . Sasa wawape waislam then wakristo ama tubakie na Mahakama za kawaida .
 
ILANI YA CCM 2005/2006, SURA YA PILI:

(22). Mchakato wa kuitoa nchi yenye uchumi ulio nyuma na tegemezi kama ilivyo Tanzania kuelekea kwenye uchumi wa kisasa lazima uzingatie vipaumbele vikuu vitatu.

Kwanza lazima kuwaanda kwa elimu, maarifa na mwelekeo watu wneywe. Rasilimali watu ndiyo nyenzo kuu katika ujenzi wa uchumi wa kisasa. Uchumi wa kisasa hauwezi kujengwa na watu walijikita katika mitazamo ya kijadi. Lazima wawe watu walio tayari kujifunza maarifa mapya na tabia mpya zinazoendana na matakwa ya mapinduzi ya kilimo na viwanda, na pia masuala ya afya,

ndio maana katika kujenga msingi wa uchumi wa kisasa elimu ni lazima ipewe kipaumbele cha kwanza, elimu yakawaida, elimu ya ufundi na elimu ya watu wazima yenye manufaa.
 
Duh !! Hapa Es umeniaha hoi sana CCM yako haiendani na maandiko hayo hasa baada ya matamko ya juzi kwamba only Div 1 &2 wanastahili mkopo ili wasome sasa kweli tutafika kielimu ?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom