Ni nini hatima ya maelfu ya hotel za kitalii zilizopo jiji la Arusha?

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,461
Uuzaji na ubinafsishaji wa mali za wananchi watua huko Kilimanjaro. Kuna kila dalili hali ikawa mbaya kwa wananchi waliojenga mahotel ya Kitalii arusha mjini kwani:

1. Watalii watashuka uwanjani watalala hapo hapo uwanjani na asubuhi wataondokea hapo kwenda National Park.

2. Wakitoka National park watalala hapo hapo uwanjani na kurukia ndege hapo hapo uwanjani.

3. Waarabu wa Loliondo watafurahi kulala airport na kurusha wanyama kwao mwisho wa siku hawatarudi mbugani kuangalia wanyama tena .

4. Hotel hiyo itajengwa eneo la KIA au Rais Samia ametenga eneo lake ili hotel iwe yake.

5. Mkataba ni wa miaka mingapi na hotel itakuwa mali ya nani?

6. Ni kweli watu wa kanda ya kaskazini wameshindwa kuendeleza uwanja huo kwa kujenga eneo la nyota tano na maduka?

7. Ni kigezo gani kimetumika kuwapa watu wa oman uwanja huo?

8. Mbunge wa Jimbo la Hai, ameuza uwanja na amesimamia uwanja kuondoka anatarajia kurudi Jimboni kuomba kura 2025?

9. Eneo la Kilimanjaro airport lilikuwa na mgogoro na wamasai na mbunge akawahakikishia kuwa eneo lso liko salama na watarejeshewa? Sasa limetolewa kwa Waarabu?

10. Je kuuzwa kwa Kilimanjaro airport Ngorongoro ipo salama haijauzwa?

11. Maswali ni mengi kuliko majibu ila kiuhalisia Saa100 kwa miaka 2 ameuza kila kitu.

7FF41F27-BCEF-4847-932A-97398BA4463C.jpeg
 
Uuzaji na ubinafsishaji wa mali za wananchi watua huko Kilimanjaro.
Kuna kila dalili hali ikawa mbaya kwa wananchi waliojenga mahotel ya Kitalii arusha mjini kwani:

1. Watalii watashuka uwanjani watalala hapo hapo uwanjani na asubuhi wataondokea hapo kwenda National Park.

2. Wakitoka National park watalala hapo hapo uwanjani na kurukia ndege hapo hapo uwanjani.

3. Waarabu wa Loliondo watafurahi kulala airport na kurusha wanyama kwao mwisho wa siku hawatarudi mbugani kuangalia wanyama tena .

4. Hotel hiyo itajengwa eneo la KIA au maza ametenga eneo lake ili hotel iwe yake.

5. Mkataba ni wa miaka mingapi na hotel itakuwa mali ya nani?

6. Ni kweli watu wa kanda ya kaskazini wameshindwa kuendeleza uwanja huo kwa kujenga enro la nyota tano na maduka?

7. Ni kigezo gani kimetumika kuwapa watu wa oman uwanja huo?

8. Mbunge wa Jimbo la Hai, ameuza uwanja na amesimamia uwanja kuondoka anatarajia kurudi Jimboni kuomba kura 2025?

9. Eneo la Kilimanjaro airport lilikuwa na mgogoro na wamasai na mbunge akawahakikishia kuwa eneo lso liko salama na watarejeshewa? Sasa limetolewa kwa Waarabu?

10. Je kuuzwa kwa Kilimanjaro airport Ngorongoro ipo salama haijauzwa?

11. Maswali ni mengi kuliko majibu ila kiuhalisia Saa100 kwa miaka 2 ameuza kila kitu
Labda Hoja hapo ni moja tu ,ambayo ni eneo lililojengwa hotel inaweza kuathiri flow ya watalii mjini, lakini uwekezaji kwenye sector ya hotel kwa njia ya ubinafsishaji ni jambi lipo muda mrefu nchini hata kempinski anamiliki muarabu sasa tusiwe tunafuata tu mkumbo na kulalamika kila kitu, embu lete hoja ya msingi kwanini isijengwe hoteli ya nyota tano hapo kia ili watanzania wakapata ajira na nchi na mkoa ukapata mapato
 
Hiyo tenda ingetangazwa na ikawa wazi arusha watanzania wapo wengi wenye uwezo kuliko hao watu wa pembe waliokimbilia oman sasa wanajiita Waarabu
 
Sorry mkuu ila huna hoja yeyote,
Hio hotel itakuwa kubwa kiasi gani kuaccomodate watalii wote wanaotua KIA ?
Je hao watalii wanaenda tu mbugani? Watalii wanakaa hapo A-City week - Mwezi nao watakuwa wanalala hapo hapo kiwanjani?
Ni woga wako tu but ujenz wa hoteli kama hizo ni muhimu, uzuri kwa Tz maeneo bado mengi, wengine wajenge pengine simple tu
 
Uuzaji na ubinafsishaji wa mali za wananchi watua huko Kilimanjaro. Kuna kila dalili hali ikawa mbaya kwa wananchi waliojenga mahotel ya Kitalii arusha mjini kwani:

1. Watalii watashuka uwanjani watalala hapo hapo uwanjani na asubuhi wataondokea hapo kwenda National Park.

2. Wakitoka National park watalala hapo hapo uwanjani na kurukia ndege hapo hapo uwanjani.

3. Waarabu wa Loliondo watafurahi kulala airport na kurusha wanyama kwao mwisho wa siku hawatarudi mbugani kuangalia wanyama tena .

4. Hotel hiyo itajengwa eneo la KIA au maza ametenga eneo lake ili hotel iwe yake.

5. Mkataba ni wa miaka mingapi na hotel itakuwa mali ya nani?

6. Ni kweli watu wa kanda ya kaskazini wameshindwa kuendeleza uwanja huo kwa kujenga eneo la nyota tano na maduka?

7. Ni kigezo gani kimetumika kuwapa watu wa oman uwanja huo?

8. Mbunge wa Jimbo la Hai, ameuza uwanja na amesimamia uwanja kuondoka anatarajia kurudi Jimboni kuomba kura 2025?

9. Eneo la Kilimanjaro airport lilikuwa na mgogoro na wamasai na mbunge akawahakikishia kuwa eneo lso liko salama na watarejeshewa? Sasa limetolewa kwa Waarabu?

10. Je kuuzwa kwa Kilimanjaro airport Ngorongoro ipo salama haijauzwa?

11. Maswali ni mengi kuliko majibu ila kiuhalisia Saa100 kwa miaka 2 ameuza kila kitu.

View attachment 2673845
Utalii wa Wanyama uko Ovarated sana Bongo.
 
Hata ukiambiwa huwezi amini
Mkuu si utaje humu tusipende umbea na uzushi , tusiwe watu wa kulalamika bila ya kuwa na hoja za msingi, taja huyo mtanzania mwenye 5 star hotel ili tuone uzoefu wake kwenye jambo husika , ama sivyo utaishia kumpa kitu dalali halafu yeye aende akatafute tena mwekezaji na hili jambo limeshatokea sana huko nyuma, watu wanaomba vitu lakini uwezo na uzoefu hawana ,wanaishia na wao kutafuta tena mwekezaji, si bora serikali itafute mtu mwenye uwezo na experience na jambo husika .
 
Hiyo tenda ingetangazwa na ikawa wazi arusha watanzania wapo wengi wenye uwezo kuliko hao watu wa pembe waliokimbilia oman sasa wanajiita Waarabu
International airport zote duniani huwa na hotel kadhaa katika viunga vya uwanja wa ndege. Kwamba KIA au JNIA haina hotel ni kituko. Kwa kwaida hoteli hizo hulenga wasafiri ambao kwa sababu moja au nyingine hulazimika kulaa hapo au kupumzika hapo kwa muda mrefu wakisubiri connection. Huwa hazilengi watalii wanaokwenda kwenye nchi husika. Fikira hata kama ni wewe unakwenda kufanya utalii katika nchi fulani itakuwa ajabu ukifika ulalae airport halafu uende kuona kuvutio fulani halafu urudi airport ka kupanda ndege kurudi nyumbani. Hivyo usiwe na wasiwasi ndugu. Hotelk za mjini Arusha zitaendelea kuwa na soko. Hivyo hata wewwe kama una mzigo wa kutosha wekeza tu kwenye hoteli mjini Arusha.
 
Waliotufunga minyororo enzi hizo na tuliwafukuza kwa nguvu Sasa tumeanza kuwakabidhi nchi, Kuna miaka inakuja nchi za kiafrika itakushida hakutakua na ardhi ya kilimo, hakutakua kua na ufungaji, hakutakua na wachimbaji wadogo wazawa kma tunavyosikia tutakua vibarua, tutakua watazamaji Kama mashabiki wa Mpira, hata elimu hizi za dunia ya tatu hazitakua na maana tena ni mahangaiko tu.
 
Back
Top Bottom