Oman waamua kutujengea VIP na maduka kwenye Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,892
Oman kupitia Shirika lake la Viwanja vya ndege vya Oman Jumatatu Juni 13 walisaini mkataba wa makubaliano (MoU) na Kampuni ya Maendeleo ya Viwanja vya Ndege ya Kilimanjaro (KADCO) ili kuendeleza jengo la abiria la VIP katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

Makubaliano hayo yalitiwa saini na Abdul Nasser Abdullah al Yamani, makamu wa rais, Maendeleo ya Biashara, Viwanja vya Ndege vya Oman, na Christine Mwakatobe wa KADCO.
oman-airports.jpg

Makubaliano hayo yanaeleza kuwa Shirika la Viwanja vya Ndege vya Oman litafanya uendelezaji wa Jengo la Watu Mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, Ujenzi wa hoteli ya nyota tano kwa ajili ya abiria na jengo la biashara/maduka makubwa katika uwanja huo.

MY TAKE;

Wanyama wetu watapona? Madini yetu ya Tanzanite je?

=====

Muscat. Oman Airports has on Monday June 13 signed a memorandum of understanding (MoU) with Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO) to develop a VIP passenger terminal in Kilimanjaro International Airport.

Following the agreement, Tanzania will benefit from Oman Airports’ experience in airport management and VIP services.

The MoU was signed by Abdul Nasser Abdullah al Yamani, vice-president, Business Development, Oman Airports, and Christine Mwakatobe of KADCO.

The MoU stipulates that Oman Airports will undertake the development of the General Terminal for VIPs and hangar facility at Kilimanjaro International Airport, development of a five-star hotel for passengers and a business complex/shopping mall in the airport.

The MoU has scope for development of other facilities that may be agreed upon mutually between the parties.

‘This partnership will serve in developing the facilities referred to in the text of the MoU to ensure the provision of high-standard services as part of efforts to raise revenues for both the Tanzanian government that owns the airport and Oman Airports,’ a press release said

Chanzo: The Citizen
 
Oman kupitia Shirika lake la Viwanja vya ndege vya Oman Jumatatu Juni 13 walisaini mkataba wa makubaliano (MoU) na Kampuni ya Maendeleo ya Viwanja vya Ndege ya Kilimanjaro (KADCO) ili kuendeleza jengo la abiria la VIP katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro...
Huyu mama anapenda vya buree!!! Sijui kama anajua hamna BURE ISIYO NA GHARAMA
 
Oman kupitia Shirika lake la Viwanja vya ndege vya Oman Jumatatu Juni 13 walisaini mkataba wa makubaliano (MoU) na Kampuni ya Maendeleo ya Viwanja vya Ndege ya Kilimanjaro (KADCO) ili kuendeleza jengo la abiria la VIP katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro...
Hakuna uwanja wa kimataifa wa ndege usiokuwa na maduka. Yaelekea sisi tulishondwa hilo! Tusilaumu wala kusikitika kwa maduka hayo kuna hatua itapigwa.

Na wanyama watapona kwa kuwa hakutakuwa na duka la wanyama uwanjani. Hatiwezi kuishi kama kisiwa lazima twende na dunia. Tukipinga ku doubt jambo fulani basi pia tuwe na solution yake.

Kwenye hili wako sahihi iwapo kweli wanavutia watalii
 
Nilikuwa nashangaa kwanini serikali miaka yote hawakujenga mahoteli jirani na uwanja huu wa KIA?

Tusipige kelele sasa mdau wa maendeleo ameamua kuja kuwekeza baada ya nchi kufunguka na kuona fursa ambayo wazee wetu nashangaa hawakuiona inayotazama mlima maarufu wa Kilimanjaro na pia kujenga mahoteli wageni wafikie wakisubiri miruko / flight za ndege.
 
Oman kupitia Shirika lake la Viwanja vya ndege vya Oman Jumatatu Juni 13 walisaini mkataba wa makubaliano (MoU) na Kampuni ya Maendeleo ya Viwanja vya Ndege ya Kilimanjaro (KADCO) ili kuendeleza jengo la abiria la VIP katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro...
KWa Sasa Mimi sitaki Wala sikia waarabu, Kama ambavyo wamekua wakiwafanyisha kazi za ajabu ndugu zetu wapendao huko , mfano ni dada mmoja alifika kule la kaa miaka 3 ila mda wote nifungiwa ndani kisa analea mbibi mmoja,Sasa wametugeukia kwenye aridhi yetu wapo radhi wamasai wafe kisa wanataka wanyama
 
Unataka kusikia watu gani sasa?
 
Utakuta waarabu na ahadi yao walishapewa ksbisa kwa malipo ya maduka KIA ambayo hata hayajajengwa wala hatujui ni ya aina gani. Hii nchi sijui
 
Nilikuwa nashangaa kwanini serikali miaka yote hawakujenga mahoteli jirani na uwanja huu wa KIA?

Tusipige kelele sasa mdau wa maendeleo ameamua kuja kuwekeza baada ya nchi kufunguka na kuona fursa ambayo wazee wetu nashangaa hawakuiona inayotazama mlima maarufu wa Kilimanjaro na pia kujenga mahoteli wageni wafikie wakisubiri miruko / flight za ndege.
Serikali haikujenga lakini si kwamba hayapo.
 
Wanatujengea bure kwanini? kuna kitu gani tumeshawapa? au tutawapa?

Samia atakaporudi aje kutolea ufafanuzi haya mambo, sio tuambiwe ni "unconditional love" toka kwa wajomba.

Mkuu kwani hutaki Mjomba atusaidie wapwa zake?
 
Back
Top Bottom