Ni nini hatima ya kanisa la Feel free?

Ni nini hatima ya kanisa la Feel free?

Mambo mabaya na mazuri ya Watu Wa Mungu Wa Kweli , Jehova Elohim aliyesema kwa Moto na Kwa radi yaliandikwa na kusimuliwa Kwa vizazi vyote , sembuse Hawa watumishi Wa Mshahara wanaosaka Maisha na ufahari Wa Dunia.!!
Daudi alichepuka na MKE Wa Askari wake ikawekwa wazi mpaka Leo vitukuu wanajua kuwa Babu Yao alichepuka na MKE Wa MTU.

Yusuf alikataa kuchepuka na MKE Wa Mfalme ikafichwa Lakini Baadae ikawekwa wazi na Mpaka Leo tunajifunza uadilifu na uaminifu Wa Yusuf.

Nyakati hizi zitabiriwa ,kiila Jambo linalofanyika sirini litawekwa wazi.Likifanyika kwenye Giza litawekwa wazi kwenye Nuru.
Hakuna dhambi isiyo na gharama.
MASANJA ameibeba dhambi ya mkewe ni lazima itamgharimu kimwili na kiroho pia.
Yesu alizibeba dhambi za wanadamu Kwa gharama ya uhai wake.
Someni Vitabu, Yaani Biblia. Mtapata ufahamu.
Biblia inasema ,"asomaye na afahamu'
Vijana mnatakiwa kusoma biblia vizuri kabla hamjaandika mitandaoni. Musa alivunja agizo la Mungu na kuoa mwanamke wa Ethiopia. Miriamu na Haruni (dada na kaka wa Musa) wakaanza kumhukumu.

Alichofanya ni kuwakaripia wao badala ya Musa mwenye makosa. Miriamu akawa mkoma kwa siku saba na pona yake ilitokana na maombi ya Musa ambaye walikuwa wanamsema ana dhambi.

Biblia iko wazi kabisa, Mungu anajua namna ya kushughulika na watumishi wake pale wanapomkosea na sio kazi ya mtu mwingine kuhukumu.

Warumi 14:4
Wewe ni nani hata umhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Ni bwana wake tu awezaye kuamua kama amesimama au ameanguka. Naye atasimama kwa sababu Bwana anaweza kumfanya asimame.

Hapa ukimuuliza Mshana kama anao ushahidi wowote wa Masanja au mke wake kufanya dhambi hawezi kuwa nao isipokuwa haya maneno ya mitandaoni.

Anyway, mimi nakaa pembeni, kila mtu atavuna anachopanda.
 
Mshana unautumia vibaya umaarufu wako hapa jf kuliendeleza hili jambo ila utakuja kuvuna matokeo yake.

Hapa jukwaani huwa wanakuona wewe mtaalamu wa mambo ya rohoni ila mimi huwa nakuona mweupe sana

Hivi unapata wapi ujasiri wa kutuhumu watumishi wa Mungu hadharani namna hii?

Anyway, utakuja kuvuna unachopanda.
Msania anamtumikia Mungu gani?
 
Watu8 natambua ukongwe wako hapa JF! Nimekukuta hivyo naamini una ukomavu wa kiakili kimtazamo na kimaono.. JF inatukuza kwa namna hiyo ndio maana ni rahisi sana kutambua post ya mgeni halisi na mgeni mwenyeji kwa muktadha wa utambulisho wetu

JF ni forum huru kwa sheria, vigezo na masharti yake! Imejijenga na kujipambanua kwa namna ambayo imekuwa tegemeo la wengi na chanzo muhimu cha taarifa kwa yale yote yanayotokea kwenye jamii

Mimi ni mwandishi mchambuzi ninayependa kuangalia kila tukio na kila habari kwa engo zote ili kukidhi mahitaji ya kila mmoja.. Nikiri wazi napenda kuandika

Sina maslahi kinzani na Masanja bali nina maslahi na wale wote wanaopenda kujifunza kupitia makosa ya wengine.. Nami pia hujifunza kupitia maandiko ya wengine
Kwenye hii ishu ya Masanja wengi wameandika mengi, kwa kulaumu,kwa kudhihaki kubeza umbea nknk.. Nimepitia mabandiko karibia mane nami nikaandika mada tatu ukiacha hii

Baadhi ya mada ziliishia level ya kawaida ya kuonesha chuki kwa masanja kutokana na hulka yake huko nyuma! Kumbuka kwenye mapito yetu maishani tunaacha footprints mioyoni mwa watu ambazo huwa hazifutiki.. Na siku ya siku ikifika watu watazirudufu nyayo zako upenuni kwa wema ama kwa ubaya!
Nimechagua kwa makini sana kwenye mada zangu nne maneno ya kuandika ili kuepusha hisia za kinyongo, rohombaya, wivu nk.. Na pia kuepesha marudio ya mada huku nikijaribu kuangazia kila upande wa tukio zima ili kuitendea haki dhana nzima ya home of great thinkers

Kila habari huwa na miguu minne
1. Tetesi- hii inaweza kujulikana ama kutojulikana na wengi mitandaoni

2.Ithibati ya tetesi ambayo hugeuka kuwa kamili ambayo .. Hapa ndio huwa kuna breaking news! Na ndio kipindi ambacho kila mtu huandika chochote

3. Habari kuwa ya kawaida na watu kurudi kwenye tukio husika na kuanza sasa kulichambua kwa ladha na vionjo mtu apendavyo..!

4. Kuelekea tamati ya tukio, hapa wengi hawana habari tena kwakuwa walishaandika na kumaliza... Lakini kuna wale wa kufanya majumuisho na kuangalia nini kiliachwa na kwa sababu gani kiliachwa na je kinafaa kufanyiwa mjadala kwa manufaa ya wengi kama sio wote?

Mada zangu nne kwenye sakata zima linalomgusa Masanja kama key player zimezingatia huo mtitiriko na sina mada nyingine zaidi ya hii kwenye hili labda litokee tukio lingine jipya ndani ya tukio kuu
Mada ya kwanza ilimhusu katibu


Katibu katibua au katibuliwa?

Mada ya pili ilikuwa ni mwendelezo wa mada ya kwanza


Part 3 sakata la Katibu: Kitendawili hakijatenguliwa bado. Je, Katibu katibua ama katibuliwa?

Mada ya tatu ilihusu utata wa watoto


Sura zetu hutuonea haya na kutusuta

Na ya nne inahusu kanisa! Ukiangalia hakuna heading inamtaja Masanja hata moja

Naamini nimetoa ufafanuzi mzuri[emoji1545]
Bro,
JF is where we dare to talk openly.
Shida iko wapi.
Hao wanaokosoa mada zao zenye weledi ziko wapi???

Si wengi tunawaona ktk majukwaa "pendwa".

Wengi hawajui JF na hizi mada za mafunzo zinasaidia saaana.

Halafu inshu ya Masanja isimfanye akaze fuvu...Masanja bila kusaidiwa kimawazi ktk angle tofauti anaweza kupanga au kufanya tukio zito ndani ya miaka miwili au mitatu. Inatakiwa watu wasene saana, wampe ushauri saana ili apime vutendo na hatua zake hapo baadaye.

Cha ajabu watu wanaoponda mada zinazohusu tukio hili hawashinikizi serikali kufanya uchunguzi juu ya kifo Cha katibu. Kana kwamba katibu hana haki ya utetezi ila msanja anayo.

However hili ni jukwaa huru kwanini mtu azuiwe kutoa maoni yake na havunji sheria?

Mkuu jisikie huru kuandika, usivunjike moyo hata kidogo.

Pia, kama kuna mtu feelings zake zimeguswa na hizi mada za Masanja basi atumie lugha ya staha kuelezea hilo. Si kufanya kama vile Mshana hajui anachokifanya.

Kiufupi humu jukwaani hakuna anayejitahidi kutumia muda wake kutafakari na kuandika mada zenye mashiko na zinazodumu muda wote kama Mshana. Mfano uzi wa selfie, vituko mtandaoni, na nyingine kadhaa wa nkadhaa ambazo ni muhimu na very educative.
Ntatoa mfano binafsi, juzi usiku kama saa saba kuna mtu alikoment ktk uzi wa " Hii imewahi kukutokea".
Ule uzi unaongelea jinsi watu walivyotenda mema na wakati huu wameshakufa na angali bado hatujawalipa mema yao.

Ingawa ule uzi nilishausoma miaka kadhaa nyuma lakini juzi umenigusa kwa hisia tofauti saaana....hali iliyopelekea kufanya mipango ya kumlipia ada kijana mmoja ambaye anachangamoto just because nilitaka kufanya jema kwa mtu ambaye nafahamu anashida ya kweli na Sina nasaba naye hata kidogo... Inshu yangu ni kuwa tusidharau mtu anapoua kutoa bando lake na muda kama kuna shida basi mfate hata PM mshauri siyo ku demoralize wazi wazi....

Jumapili njema.
 
Ahsante kwa mada hii kaka mkubwa, Cha kwanza naimani unawajua watanzania vizuri huwa wakiaminishwa kitu huwa ni ngumu kuwatoa mpaka litokee jambo ambalo mbele ya macho yao na bado kuna wajinga wataamiini ni majaribu tu, hii ni kwasababu wengi wao biblia wanaisoma kama gazeti au wanazo Bible kama urembo tu bila kuisoma.


Hivyo wengi sana wataendelea kumwamini na wataaminishwa vizuri ila kitu ambacho kitatokea mbele ikiwa katika hili jambo ama kashfa hii ni ya kweli basi hakutabaki salama lazima patawaacha midomo wazi baadae ila sio leo wala kesho, tuombe atokee mtawala mwenye uchungu na haki tutayajua mengi na sio masanja tu
Kuna Siri Kubwa Sana Katika Ndoa Ya Masanja.
Haiwezekani Mtu Unajiita Askofu wa Kanisa Unasimama Mbele Ya Waumini Nakuwatangazia Kuwa Huwezi Kumwacha Mkeo Kwa Sbb Ni Mzuri .Eti Ata nikimkuta Na Mwanaume Napima Kama Namuweza Kama Simuwezi Basi Namchukua Mke Wangu Nakutoka Nduki.
 
Mshana unautumia vibaya umaarufu wako hapa jf kuliendeleza hili jambo ila utakuja kuvuna matokeo yake.

Hapa jukwaani huwa wanakuona wewe mtaalamu wa mambo ya rohoni ila mimi huwa nakuona mweupe sana

Hivi unapata wapi ujasiri wa kutuhumu watumishi wa Mungu hadharani namna hii?

Anyway, utakuja kuvuna unachopanda.
Pumbavu ,Uganga Mmejigeuza Watumishi Wa Mungu.
 
Bro,
JF is where we dare to talk openly.
Shida iko wapi.
Hao wanaokosoa mada zao zenye weledi ziko wapi???

Si wengi tunawaona ktk majukwaa "pendwa".

Wengi hawajui JF na hizi mada za mafunzo zinasaidia saaana.

Halafu inshu ya Masanja isimfanye akaze fuvu...Masanja bila kusaidiwa kimawazi ktk angle tofauti anaweza kupanga au kufanya tukio zito ndani ya miaka miwili au mitatu. Inatakiwa watu wasene saana, wampe ushauri saana ili apime vutendo na hatua zake hapo baadaye.

Cha ajabu watu wanaoponda mada zinazohusu tukio hili hawashinikizi serikali kufanya uchunguzi juu ya kifo Cha katibu. Kana kwamba katibu hana haki ya utetezi ila msanja anayo.

However hili ni jukwaa huru kwanini mtu azuiwe kutoa maoni yake na havunji sheria?

Mkuu jisikie huru kuandika, usivunjike moyo hata kidogo.

Pia, kama kuna mtu feelings zake zimeguswa na hizi mada za Masanja basi atumie lugha ya staha kuelezea hilo. Si kufanya kama vile Mshana hajui anachokifanya.

Kiufupi humu jukwaani hakuna anayejitahidi kutumia muda wake kutafakari na kuandika mada zenye mashiko na zinazodumu muda wote kama Mshana. Mfano uzi wa selfie, vituko mtandaoni, na nyingine kadhaa wa nkadhaa ambazo ni muhimu na very educative.
Ntatoa mfano binafsi, juzi usiku kama saa saba kuna mtu alikoment ktk uzi wa " Hii imewahi kukutokea".
Ule uzi unaongelea jinsi watu walivyotenda mema na wakati huu wameshakufa na angali bado hatujawalipa mema yao.

Ingawa ule uzi nilishausoma miaka kadhaa nyuma lakini juzi umenigusa kwa hisia tofauti saaana....hali iliyopelekea kufanya mipango ya kumlipia ada kijana mmoja ambaye anachangamoto just because nilitaka kufanya jema kwa mtu ambaye nafahamu anashida ya kweli na Sina nasaba naye hata kidogo... Inshu yangu ni kuwa tusidharau mtu anapoua kutoa bando lake na muda kama kuna shida basi mfate hata PM mshauri siyo ku demoralize wazi wazi....

Jumapili njema.
@James Comey shukrani sana sana kwa mchango wako wenye kutia moyo.. Barikiwa sana[emoji1752][emoji1545]
 
Ni ukweli usiotia mashaka watoto wa Masanja wamefanana na katibu. Hivi Mshana Jr hawa watoto wakiwa wakubwa wataelezwa ukweli kuwa baba yao mzazi alikufa kifo cha aina ghani?
Coz internet never forget.
 
Ni ukweli usiotia mashaka watoto wa Masanja wamefanana na katibu. Hivi Mshana Jr hawa watoto wakiwa wakubwa wataelezwa ukweli kuwa baba yao mzazi alikufa kifo cha aina ghani?
Coz internet never forget.
Ukweli huwa haufichiki kuna siku watakuja kujua kila kitu kama hawatanyamaa milele kabla ya kujua[emoji2827]
 
Ukishamjua mngoni wako hakikisha mkeo ajui Kama umeshajua kichoendelea kati yao tena usihangaike kutaka kuwashika ugoni

Unamtengenezea ajari moja tu bodaboda wengi huwa ni wahanga wa hii kitu. Asipokufa atapata kilema ambacho hataweza kuwa na mkeo tena.

Sijaona kanisa likimzika katibu sijaona hata salamu za rambirambi zilizotolewa na kanisa.
 
Ukishamjua mngoni wako hakikisha mkeo ajui Kama umeshajua kichoendelea kati yao tena usihangaike kutaka kuwashika ugoni

Unamtengenezea ajari moja tu bodaboda wengi huwa ni wahanga wa hii kitu. Asipokufa atapata kilema ambacho hataweza kuwa na mkeo tena.

Sijaona kanisa likimzika katibu sijaona hata salamu za rambirambi zilizotolewa na kanisa.
Sijaona kanisa likimzika katibu sijaona hata salamu za rambirambi zilizotolewa na kanisa.[emoji2827]
 
Ni kweli . Wahubiri wamesahau kuwa Mwanaume ndiye Mfano Wa Mungu hapa Duniani. Ndio MAANA ya kuwa baba na Mlezi .
Wanaume Kwa maelfu ni waadilifu sana Lakini hawayumbishwi na mihamko ya kimitandao. Wanawake wengi ni Wazinzi waliozaa Nje ya ndo hivyo kujikuta wakiwa waongo Maisha Yao Yote.
Mwanamke aliyezaa Nje ya ndoa mara zote Inabidi awe Mwongo na kumdanganya mumewe kuwa MTOTO ni Wa kwake na kamwe hawezi kutubu na kusema ukweli kuwa huyu MTOTO Mmoja au Wawili SIO Wa kwako . Nilikosea kutoka Nje na kuzaa. Hiyo dhambi inabaki Moyoni mwake maisha yake Yote.
Pili wanawake wengi wamewadanganya Watoto wao na kuwakosesha Haki Yao ya kuwajua baba zao halisi kibiologia na kuwaacha Watoto wakiwiishi na baba bandia Maisha Yao Yote. Kuna wanawake waliozaa mpaka na baba zao ,wajomba zao na kaka zao Tena wakiwa Ndani ya ndoa. Hao ndio wanaposikia Makanisa ya kuwachamba wanaume wanakimbilia huko Ili kujipa uhalali Wa dhambi na dhamira zao zisizoisha kuwahukumu kwenye mioyo Yao.

Vitabu vya Dini vyote vimesimama kidete kipinga uzinzi na Wazinzi hasa wanawake wamewekewa Sheria Kali sana kwenye suala la zinaa Kwa Sababu Mungu aliona Athari kubwa ya zinaa Kwa mwanamke. Wayahudi mwanamke mzinifu alipigwa Kwa mawe na kuawa lengo lilikua kiwaepusha na tamaa ya kutoka Nje na kwende kuzaa na mataifa mengine yaliyokuwa yamejaa vinasaba vya kishetani na kichawi Kwa wakati Huo ambapo walizaa Watoto mashoga, wachawi na wasiompenda Mungu kama KAINI. Wanawake Wakati Huo walivutiwa na starehe na anasa za watu Wa mataifa mengine ndio MAANA MKE Wa Lutu aligeuka nyuma Ili arudi kwenye starehe za Sodoma na Gomora Yaani Mbele na nyuma.
Mungu aliwakataza wasigeuke nyuma Kwa MAANA kuwa wasijaribu Kutia Nia ya kurudi Kwenye Nchi hiyo iliyokuwa imejaa anasa za Kila aina.
Mwanamke alishindwa kutii. Akageuka Nyuma Ili arudi kwenye starehe.
Ni wazi kuwa palikua na mabishiano makubwa na ugomvi njiani kati ya Lutu na MKE wake. Mkewe akidhani kuwa Amri ya Mungu ya kutoka Sodoma na kwenda Nchi nyingine wasio ijua kwenda kuanza Maisha upya haikuwa Sawa. Aliona ananyimwa Haki ya kuishi anapotaka. Aliona mumewe Ana mambo ya kishamba na anaitia familia kwenye umaskini. Huenda WALIKUA wameshajenga na kumiliki NYUMBA Yao Halafu Mume anakuja anasema Mungu ametumuru tutoke hapa twende Tukaishi sehemu nyingine tuanze Maisha upya.
Ukaidi Wa mwanamke kwenye ndoa ni Hatari mno na Kila ulipotokea palitokea mabadiliko makubwa yaliyoiathiri jamii nzima kama Mume ataridhia kufuatana na uasi Wa mwanamke.
Hebu fikiria kama Lutu Naye angeamua kukaidi Amri ya Mungu na kusema ngoja nirudi kumfuata MKE wangu mana huenda MKE wangu amepata maono makubwa zaidi ya kurudi kwenda kuwahuburi Watu Wa Sodoma na Gomora.
Lutu alikua imara na anaamua kuendelea Mbele bila kugeuka nyuma kumfuata mkewe

Kwenye Biblia Kuna visa vingi ambavyo Wanawake wameleta matatizo makubwa kwenye jamii nzima kutokana na tamaa zao. Yusuf angejaribu kuzini na MKE Wa Mfalme leo Hii tusingeongea habari za uadilifu wake. Mpaka alikubali kufungwa Gerezani lakini hakutaka kutembea na MKE Wa Mfalme.

Lakini pia Kuna kisa Cha Mfalme Daudi na MKE Wa Uria Askari wake mkuu kabisa Aliyekua vitani. MKE Wa Uría alikubali kutembea na Mfalme wakati mumewe alipokua vitani .
Alipopata ujauzito wakatengeneza njama ya kumbambikia Mumewe Ile mimba Ili Kitanda kisizae HARAMU lakini Mungu akataka kuweka wazi ule uovu wao. Mfalme alimwita Uría arudi Nyumbani Kwa dharura. Uría akarudi akamwambia aende akapumzike Nyumbani kwake na Mkewe. Cha ajabu MTU Aliyekua vitani Siku nyingi lakini aligoma kwenda nyumbani kulala. Akasema siwezi kwenda kupumzika Nyumbani Wakati Nchi yangu IPO vitani na askari wenzangu nimewaacha wanaendelea kupambana.
Alijisikia Fahari kupigania Nchi yake na vizazi vyao zaidi KULIKO kwenda kulala na mkewe. Huyu ni mwanamke shujaa sana asiyetajwa na watu Wa Dini. Mwanaume mtiifu Kwa Mungu na Kwa Taifa na jamii nzima .
Njama ya Daudi na mchepuko wake iliposhindikana basi walipanga njama ya kumuua Mumewe.
Hivyo Mfalme Daudi alitoa Amri Uría awekwe kwenye kikosi Cha Mbele vitani. Hiko aliuawa na kuiacha familia yake.
Huo uovu Wa mwanamke kwenye ndoa Wahubiri wengi hawataji zaidi ya kumlaumu wanaume bila Huku wakiwasifia wanawake wakati hakuna Hata Mfano Mmoja Wa mwanamke aliyeweza kuishinda dhambi ya Zinaa Nje ya Sheria Kali ya Kukaa mbali na wanaume na kujisitiri.


Wanawake wengi hasa walioko kwenye makanisa hayo hawajui Mila za wanadamu Wala historia ya masuala ya kidini zaidi ya kuvaa nguo fupi na mabega wazi na kucheza miziki Kanisani. Hawajui kuwa shatani anatawala Mwili zaidi KULIKO roho.
Wengi hawasomi Biblia zaidi ya kusema "Mchungaji Kasema" .

Wanawake wengi wamepotoshwa zaidi kutokana na kufuata zaidi Mila za Kizungu KULIKO Neno la Mungu.

Kwa waislamu kumdanganya MTOTO baba yake ni dhambi.
Asante kwa tafakuri nzuri. Nimejifunza kuwa kumbe hata sisi wanaume tunaweza kung'ara (kwa matendo ya imani au vinginevyo), lakini tukawa na mambo ya usaliti kwa Mungu, lakini pia kwa binadamu wenzetu. Angalia Daudi alivyokuwa kipenzi cha Mungu, kiasi cha kumuahidi kuwa fimbo ya ufalme haitatoka kwenye ukoo wake! Lakini alifanya matendo maovu mbele ya Mungu na mtumishi wake (Uria) na kupanga njama (zilizofanikiwa) za kumuua Uria.
 
Mbona hii ishu umeikomalia sana? mara damu ya mtu inanuka, mara ameua kama una ushahidi si upeleke polisi ili akamatwe? Au umeshiriki kwa kiasi gani mpaka uanze kuongea kama una uhakika kwamba hakujinyonga bali ameuliwa?
Ukisikiliza maelezo ya polisi, kama una akili zilizotimia, utagundua kabisa kwamba katibu aliuawa lakini polisi wanaficha ukweli kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.
 
Tunamalizia wiki iliyokuwa na drama nyingi kuhusiana na mwajiriwa wa Msanii Masanja mkandamizaji kwa cheo cha katibu kwenye shughuli zake za usanii na kanisa aliyepoteza uhai kwa kinachosemwa kajinyonga

Asilimia 99 ya mijadala ilitawaliwa kwenye kujadili yafuatayo
.Kifo tata cha katibu
.Mahusiano ya katibu na mke wa boss wake
.Reaction ya Masanja baada ya hayo matukio
.Na mwishowe watoto wa Masanja na mkewe

Athari kwenye shughuli zake za kisanii ni kama hazikugusiwa kabisa
Athari kwenye makampuni aliyoingia nayo mikataba ya kufanya matangazo ya kibiashara pia hayakujadiliwa kabisa
Athari kwenye kituo chake cha kiimani/kanisa pia zimejadiliwa kwa uchache
Kwenye mijadala husika na wachache walijaribu kugusia athari binafsi na za kifamilia

Kwenye mada hii tutaangazia athari za kanisa la Feel free church na hatima yake
Ukiachana na Makanisa yaliyojengwa kitaasisi na mifumo kamili ya utendaji kazi, makanisa mengi hasa yaliyoibuka karne hii yenye kumilikiwa na watu binafsi, yalipotea, kufa, kupoteza mvuto, kuzorota ama kufifia kutokana na wamiliki wake kupata dhoruba mbalimbali za kimaisha

Makanisa ya Marehemu mama Rwakatare, Nabii Elijah, Mzee wa upako, Mfalme Zumaridi ni mifano michache ya hicho nilichokiandika hapo juu kwa hapa nchini.. Kwakuwa wao ndio roho ya kanisa, basi kilichowapa wao kililipata kanisa pia

Kanisa la msanii Masanja mkandamizaji, lililoanza kama utani, ni kanisa changa lililokumbwa na upepo wa dhoruba kutokana na mmiliki wake kukumbana na changamoto za kimaisha. Achana na uchanga wake yeye ndio alikuwa mkuu wa hilo kanisa na shughuli zote nyeti na muhimu zilikuwa chini yake kama makanisa mengine ya namna hiyo yalivyo
Yaani ustawi wa kanisa, kukua na kushamiri kwake vyote vilikuwa mikononi mwa mwanzilishi wake.. Maombi, mahubiri, maono, na shughuli zote za kiroho vilikuwa mateka chini ya roho moja!

Msiba wa katibu wa Masanja ulikuwa msiba wa kanisa! Kama kulikuwa na katibu ina maana basi kulikuwa na viongozi wengine wa kukaimu na kukasimu madaraka pindi wakubwa wakiwa hawapo! Kanisa la jisikie huru lilipaswa kuonekana popote kivyovyote kwenye jambo kubwa kama hilo la msiba bila kujali yatokanayo!

Kwa kutofanya hivyo kanisa limejitia doa kubwa na baya mbele ya jamii na watu wachache waliokuwa na imani nalo! Kwa kuzidi kuharibu mmiliki akashindwa kutofautisha mambo binafsi ya kifamilia na ya kanisa lake! Akaenda huko mbele ya waumini wake na kuanza kuwapa vichambo vya uhakika wote walioshiriki mijadala mitandaoni kuhusiana na sakata zima!

Taswira nzima ya kanisa ilipigwa upofu pale! Na inawezekana lile likawa ndio kusanyiko la mwisho ama la lenye waumini wengi! Jumapili hii ndio itatoa majibu na hata kama wakiwepo wengi ni kwa ajili ya kwenda kushuhudia umbea

Kashfa na tuhuma zilizomkuta Masanja zinaathiri moja kwa moja shughuli zake zote za kisanii lakini kubwa na baya zaidi kanisa lake
Kashfa na tuhuma hizi ni tofauti na zile zilizowahi kuwapata wamiliki wa yale makanisa mengine kama kina
Zumaridi kupigana maofisa wa serikali
Mzee wa upako na ulevi
Gwajima na uzinzi
Geodavie na uchawi nknk
Hili la Masanja ni tuhuma za mauaji na mazingira tata ya kifo husika na ishu za kifamilia..! Imekaa vibaya mno!

Kwa jicho la kiimani na kiroho tunaweza kusema ni changamoto na jaribu la kiimani..! Lakini kwa tafakuri nyepesi kabisa ni huduma ipi kubwa ya kiroho aliyowahi kuifanya kiasi cha kumtikisha shetani hata aamue kulipa kisasi!?

Hatima ya kanisa la jisikie huru limo mikononi mwa suluhu ya kiroho kama Masanja mkandamizaji na familia yake hawana vinasaba na damu ya mtendaji wake katibu wake! Damu ya mtu hunuka., na harufu yake hutiwa chaji na roho iliyomo ndani yake... Roho ni kitu kisichokufa hivyo huibeba damu yake kutengeneza mizania ya haki..[emoji2827]
Mkuu Mshana Jr nchi hii ina miumini ya ajabu sana....utashangaa baada ya skandali hii miumini ikaongezeka kwenye kijiwe hicho cha upigaji cha Masanja.
 
Back
Top Bottom