Ni nini hatima ya kanisa la Feel free?

Ni nini hatima ya kanisa la Feel free?

Mbona hii ishu umeikomalia sana? mara damu ya mtu inanuka, mara ameua kama una ushahidi si upeleke polisi ili akamatwe? Au umeshiriki kwa kiasi gani mpaka uanze kuongea kama una uhakika kwamba hakujinyonga bali ameuliwa?
Wewe bado ni mgeni hapa jukwaaani hakuna unachojua ni Bora utulie Tu hata ishu za mtaani zenyewe hujui ni nini kinaendelea juu ya masanja na kanisa lake
 
Tunamalizia wiki iliyokuwa na drama nyingi kuhusiana na mwajiriwa wa Msanii Masanja mkandamizaji kwa cheo cha katibu kwenye shughuli zake za usanii na kanisa aliyepoteza uhai kwa kinachosemwa kajinyonga

Asilimia 99 ya mijadala ilitawaliwa kwenye kujadili yafuatayo
.Kifo tata cha katibu
.Mahusiano ya katibu na mke wa boss wake
.Reaction ya Masanja baada ya hayo matukio
.Na mwishowe watoto wa Masanja na mkewe

Athari kwenye shughuli zake za kisanii ni kama hazikugusiwa kabisa
Athari kwenye makampuni aliyoingia nayo mikataba ya kufanya matangazo ya kibiashara pia hayakujadiliwa kabisa
Athari kwenye kituo chake cha kiimani/kanisa pia zimejadiliwa kwa uchache
Kwenye mijadala husika na wachache walijaribu kugusia athari binafsi na za kifamilia

Kwenye mada hii tutaangazia athari za kanisa la Feel free church na hatima yake
Ukiachana na Makanisa yaliyojengwa kitaasisi na mifumo kamili ya utendaji kazi, makanisa mengi hasa yaliyoibuka karne hii yenye kumilikiwa na watu binafsi, yalipotea, kufa, kupoteza mvuto, kuzorota ama kufifia kutokana na wamiliki wake kupata dhoruba mbalimbali za kimaisha

Makanisa ya Marehemu mama Rwakatare, Nabii Elijah, Mzee wa upako, Mfalme Zumaridi ni mifano michache ya hicho nilichokiandika hapo juu kwa hapa nchini.. Kwakuwa wao ndio roho ya kanisa, basi kilichowapa wao kililipata kanisa pia

Kanisa la msanii Masanja mkandamizaji, lililoanza kama utani, ni kanisa changa lililokumbwa na upepo wa dhoruba kutokana na mmiliki wake kukumbana na changamoto za kimaisha. Achana na uchanga wake yeye ndio alikuwa mkuu wa hilo kanisa na shughuli zote nyeti na muhimu zilikuwa chini yake kama makanisa mengine ya namna hiyo yalivyo
Yaani ustawi wa kanisa, kukua na kushamiri kwake vyote vilikuwa mikononi mwa mwanzilishi wake.. Maombi, mahubiri, maono, na shughuli zote za kiroho vilikuwa mateka chini ya roho moja!

Msiba wa katibu wa Masanja ulikuwa msiba wa kanisa! Kama kulikuwa na katibu ina maana basi kulikuwa na viongozi wengine wa kukaimu na kukasimu madaraka pindi wakubwa wakiwa hawapo! Kanisa la jisikie huru lilipaswa kuonekana popote kivyovyote kwenye jambo kubwa kama hilo la msiba bila kujali yatokanayo!

Kwa kutofanya hivyo kanisa limejitia doa kubwa na baya mbele ya jamii na watu wachache waliokuwa na imani nalo! Kwa kuzidi kuharibu mmiliki akashindwa kutofautisha mambo binafsi ya kifamilia na ya kanisa lake! Akaenda huko mbele ya waumini wake na kuanza kuwapa vichambo vya uhakika wote walioshiriki mijadala mitandaoni kuhusiana na sakata zima!

Taswira nzima ya kanisa ilipigwa upofu pale! Na inawezekana lile likawa ndio kusanyiko la mwisho ama la lenye waumini wengi! Jumapili hii ndio itatoa majibu na hata kama wakiwepo wengi ni kwa ajili ya kwenda kushuhudia umbea

Kashfa na tuhuma zilizomkuta Masanja zinaathiri moja kwa moja shughuli zake zote za kisanii lakini kubwa na baya zaidi kanisa lake
Kashfa na tuhuma hizi ni tofauti na zile zilizowahi kuwapata wamiliki wa yale makanisa mengine kama kina
Zumaridi kupigana maofisa wa serikali
Mzee wa upako na ulevi
Gwajima na uzinzi
Geodavie na uchawi nknk
Hili la Masanja ni tuhuma za mauaji na mazingira tata ya kifo husika na ishu za kifamilia..! Imekaa vibaya mno!

Kwa jicho la kiimani na kiroho tunaweza kusema ni changamoto na jaribu la kiimani..! Lakini kwa tafakuri nyepesi kabisa ni huduma ipi kubwa ya kiroho aliyowahi kuifanya kiasi cha kumtikisha shetani hata aamue kulipa kisasi!?

Hatima ya kanisa la jisikie huru limo mikononi mwa suluhu ya kiroho kama Masanja mkandamizaji na familia yake hawana vinasaba na damu ya mtendaji wake katibu wake! Damu ya mtu hunuka., na harufu yake hutiwa chaji na roho iliyomo ndani yake... Roho ni kitu kisichokufa hivyo huibeba damu yake kutengeneza mizania ya haki..
Aisee huu uzi inabidi ukae chini uusome walau mara saba ndio utaelewa. Masanja alishatengenezaga shimo lake muda mrefu ni suala la muda tu kwa yeye kutumbukia na kufukiwa humo japo kwasasa ni kama hataki kuingia kwenye hilo shimo ila kwa kanuni ya kiasili kuna mazingira yatamsukuma aingie kwa hiari yake, hizi mambo za kuua mtu hata kwa kushiriki kwa maneno ni hatari sana kiroho kuliko wengi wanavyodhani tumwachie Mungu aseme naye ila nikijaribu kuvaa viatu vyake nashindwaa hata kuvigusa... ni jambo zito mno ambalo kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo anavyoona ukubwa wa madhara ya uamuzi wake..
 
Kabisaaa unazungumzia hatima ya kanisa lake sema ndio ivo watu lazima waunganishe na lile tukio.
Hizi mada zinatusaidia nasi kutafakari na kujifanyia self examination ili makosa ya wengine yawe funzo kubwa kwetu
Tunaweza kumzodoa na kumcheka Masanja kutwa kuchwa kumbe kikombe chetu kinatusubiri.. Ndio maana nikiandika naandika kwa tahadhari kubwa mno
 
Mshana unautumia vibaya umaarufu wako hapa jf kuliendeleza hili jambo ila utakuja kuvuna matokeo yake.

Hapa jukwaani huwa wanakuona wewe mtaalamu wa mambo ya rohoni ila mimi huwa nakuona mweupe sana

Hivi unapata wapi ujasiri wa kutuhumu watumishi wa Mungu hadharani namna hii?

Anyway, utakuja kuvuna unachopanda.
 
Mzee baba mbona umemuandama sana Masanja?

Una maslahi gani kinzani naye?
 
Kuliweza hilo wanahitaji seclusion na deliverance kubwa sana, kujishusha na kupotea mitandaoni kwa muda
Huko kwenye seclusion na deliverance mzunguko utakuwa mrefu,bora asome maandiko mwenyewe pale kwenye kipengele cha mke mzinzi,atekeleze maelekezo yale,maisha yasonge.
 
Mshana unautumia vibaya umaarufu wako hapa jf kuliendeleza hili jambo ila utakuja kuvuna matokeo yake.

Hapa jukwaani huwa wanakuona wewe mtaalamu wa mambo ya rohoni ila mimi huwa nakuona mweupe sana

Hivi unapata wapi ujasiri wa kutuhumu watumishi wa Mungu hadharani namna hii?

Anyway, utakuja kuvuna unachopanda.
Huyu atakuwa Masanja mwenyewe
 
Mbona hii ishu umeikomalia sana? mara damu ya mtu inanuka, mara ameua kama una ushahidi si upeleke polisi ili akamatwe? Au umeshiriki kwa kiasi gani mpaka uanze kuongea kama una uhakika kwamba hakujinyonga bali ameuliwa?
Ili uelewe nilazima uwe na uwezo mkubwa kiakili sio tu fursa kua jamii forum

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Nadhani mke wa masanja atafutiwe watu wa kumshauri asirudie upumbavu maana unamcost masanja kwenye kila angle. Masanja amekua muungwana sababu angeamua vinginevyo ndio angechafua zaidi kanisa na yeye mwenyewe hivyo kaamua kuibeba aibu yote na alijua inawezekana kabisa mkewe alikua analiwa na katibu
Asirudie Ila amrudishe KATIBu

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
sikiliza Mkuu, we bado mchanga kwenye baadhi ya vitu kwepa aibu ndugu...unajiaibisha wewe,wazazi na familiya yako.

kwa kifupi inaonekana bado hujajua kwanini sehemu kubwa ya watu wanamfakamia Masanja...inshort jamaa anadharau za kichoko changanya na unabii wa kimchongo ndo unamuangusha kabisa

Majigambo yakipumbavu anayojitahidi kuyaonyesha mbele za watu na kuwaona wengine wanaohangaika na maisha na bado hawajafanikiwa kama ni wazembe

Ni much know mmoja hivi ambaye bado hajajijua kuwa ni limbukeni na mshamba wa maisha

Karma is a bitch...!!

hizi ni baadhi ya sehemu mbalimbali tulizowahi fanya aidha majadiliano,story ama shughuli kadhaa wa kadha na picha nyingine ni ziada tukifanya kazi na wengi wa watu wengine very humbe eg. Joti, hivyo Masanja namjua vyema

View attachment 2387302
View attachment 2387303View attachment 2387304
kanumba aliwahi kusema MASANJA NI LIMBUKENI, remember dar to lagos
 
Back
Top Bottom