Watu8 natambua ukongwe wako hapa JF! Nimekukuta hivyo naamini una ukomavu wa kiakili kimtazamo na kimaono.. JF inatukuza kwa namna hiyo ndio maana ni rahisi sana kutambua post ya mgeni halisi na mgeni mwenyeji kwa muktadha wa utambulisho wetu
JF ni forum huru kwa sheria, vigezo na masharti yake! Imejijenga na kujipambanua kwa namna ambayo imekuwa tegemeo la wengi na chanzo muhimu cha taarifa kwa yale yote yanayotokea kwenye jamii
Mimi ni mwandishi mchambuzi ninayependa kuangalia kila tukio na kila habari kwa engo zote ili kukidhi mahitaji ya kila mmoja.. Nikiri wazi napenda kuandika
Sina maslahi kinzani na Masanja bali nina maslahi na wale wote wanaopenda kujifunza kupitia makosa ya wengine.. Nami pia hujifunza kupitia maandiko ya wengine
Kwenye hii ishu ya Masanja wengi wameandika mengi, kwa kulaumu,kwa kudhihaki kubeza umbea nknk.. Nimepitia mabandiko karibia mane nami nikaandika mada tatu ukiacha hii
Baadhi ya mada ziliishia level ya kawaida ya kuonesha chuki kwa masanja kutokana na hulka yake huko nyuma! Kumbuka kwenye mapito yetu maishani tunaacha footprints mioyoni mwa watu ambazo huwa hazifutiki.. Na siku ya siku ikifika watu watazirudufu nyayo zako upenuni kwa wema ama kwa ubaya!
Nimechagua kwa makini sana kwenye mada zangu nne maneno ya kuandika ili kuepusha hisia za kinyongo, rohombaya, wivu nk.. Na pia kuepesha marudio ya mada huku nikijaribu kuangazia kila upande wa tukio zima ili kuitendea haki dhana nzima ya home of great thinkers
Kila habari huwa na miguu minne
1. Tetesi- hii inaweza kujulikana ama kutojulikana na wengi mitandaoni
2.Ithibati ya tetesi ambayo hugeuka kuwa kamili ambayo .. Hapa ndio huwa kuna breaking news! Na ndio kipindi ambacho kila mtu huandika chochote
3. Habari kuwa ya kawaida na watu kurudi kwenye tukio husika na kuanza sasa kulichambua kwa ladha na vionjo mtu apendavyo..!
4. Kuelekea tamati ya tukio, hapa wengi hawana habari tena kwakuwa walishaandika na kumaliza... Lakini kuna wale wa kufanya majumuisho na kuangalia nini kiliachwa na kwa sababu gani kiliachwa na je kinafaa kufanyiwa mjadala kwa manufaa ya wengi kama sio wote?
Mada zangu nne kwenye sakata zima linalomgusa Masanja kama key player zimezingatia huo mtitiriko na sina mada nyingine zaidi ya hii kwenye hili labda litokee tukio lingine jipya ndani ya tukio kuu
Mada ya kwanza ilimhusu katibu
Mauaji mengine Tabata..mtoa taarifa anasema marehemu kajinyonga, lakini walinda sheria wamegoma hiyo sababu.. Ushahidi ni mwingi sana wa kumtia hatiani lakini kama kawa marehemu hana haki... Huyu si wa kwanza na hatakuwa wa mwisho Mauaji haya ni mfululizo wa vifo vinavyohusiana na mapenzi...
www.jamiiforums.com
Katibu katibua au katibuliwa?
Mada ya pili ilikuwa ni mwendelezo wa mada ya kwanza
Part 1 ilikuwa ujumbe wa katibu kulilia penzi la mke wa mtu kisha kikafuatia kifo kinachosemekana cha kujinyonga.. Hii part one always ndio huwa hot sana hasa mitandaoni na nje ya mitandao! Mengi yalitokea hapa lakini kwa sehemu kubwa yakiacha mkanganyiko na sintofahamu kubwa Moja lenye ukakasi...
www.jamiiforums.com
Part 3 sakata la Katibu: Kitendawili hakijatenguliwa bado. Je, Katibu katibua ama katibuliwa?
Mada ya tatu ilihusu utata wa watoto
Wanasema sura sio roho! Kumbe hivi ni vitu viwili tofauti ndani ya mamlaka moja.. Ndugu wasiopendana Kuna watu hawapendi kabisa kujiangalia kwenye kioo.[emoji23] sura zao zinawasuta, zinaona aibu, zinaona soni Wengine hawapendi kujiangalia wanapotoka kufanya jambo fulani baya. . Sura ya...
www.jamiiforums.com
Sura zetu hutuonea haya na kutusuta
Na ya nne inahusu kanisa! Ukiangalia hakuna heading inamtaja Masanja hata moja
Naamini nimetoa ufafanuzi mzuri[emoji1545]