Ni nini chamvutia mbu masikioni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini chamvutia mbu masikioni?

Discussion in 'JF Doctor' started by Quemu, Nov 20, 2008.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hivi kwa nini ukilala mbu huwa anapenda kusogea masikioni na kupiga mluzi wake unaokera sana?

  Je kuna maelezo yoyote ya kisayansia yanayoelezea hii tabia mbaya sana ya viumbe hawa?
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mbu wanafata kwenye masikio kwasababu ya Carbon dioxide unayotoa mdomoni, pia kwenye masikio kuna thin skin with superficiall blood vessels. Wanapenda kwenye miguu sababu ya harufu inayotoka huko ni attratact tosha. Need more?
   
 3. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ushi, ahsante....lakini umenichanganya!

  1) Sasa kuna uhusiano gani kati ya Carbondioxide kutoka mdomoni na wao kwenda kupiga kelele masikioni? Kwa nini wasipige kambi mdomoni kabisa? Na ni vipi kwa wale tunaofunga midomo wakati wa kulala? Inakuaje yani?

  2) Hiyo thin skin iko ndani ya sikio au nje? Wao wanafaidika vipi wakienda kupiga mdundiko wao masikioni..tena ukiwa umelala?

  3) Kiutaratibu watu uoga kabla ya kulala. Sasa sijui miguu hutoa harufu gani hiyo wakati ni misafi? Hata hivyo, huko miguuni sio shida.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  QM una maswali mazuri sana

  1) Mdomoni blood vessel ziko mbali QM, mbu huenda sehemu kufata source ya CO2, sasa husogea karibu na sikio

  2) Thin skin ipo nje ya sikio, blood vessel zipo juu mbu inakuwa rahisi kufikia mishipa ya damu na kufyonza damu kwa proboscis (mouth part)

  3) Miguu hutoa volatile odour moja wapo ni unsaturated fats ambazo naturally miguu hutoa regardless umeoga ama usafisha hiyo huvutia sana mbu.

  Nitakupa mfano Kuku mbu huenda kuuma kwenye combs and wattles, unajua tena kuku ana manyoya na miguu yake ina magamba, its an adaptaion na evolution inafavor hayo...
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ushi wa Rombo, maelezo murua, ahsante... nami naomba kuuliza maswali machache.

  -- hiyo carbondioxide siyo kuwa ile inayotokea puani kama process ya kupumua, au unamaanisha ile inayotekea mdomoni tu?

  --je, mbu hawa detect na kutumia kwa navigation infrared heat emission katika kuvinjari kwao?

  --je, concentration ya emission ya infrared heat katika mwili hai correspond na organ za mwili, hivyo kichwani kuwa kuna joto?

  Akhsante, ni hayo tu.

  SteveD.
   
 6. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #6
  Nov 21, 2008
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mie naomba kuuliza, je mbu anaweza kung´ata hata kiumbe kilicho kufa? maiti ya binadam mathalani.
   
 7. M

  Mama JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Juu ya hiyo, aking'ata maiti aliyefariki kwa malaria, kuna uwezekano wowote wa mbu huyo kuambukiza malaria kwa binadamu hai?
   
 8. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hiyo ya miguu imeeleweka kwa ufasaha.....

  Turudi masikioni....

  ...Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa hawa viumbe upenda masikio kwa sababu ya hizo vessels zipo karibu kuzifikia. Na kwamba huenda kule kufyonza damu. Sawa? Kama ni hivyo, mbona wakifika masikioni upiga kelele tu na sio kung'ata viiile? Kwa nini ukiamka asubuhi unakuta umeng'atwa na kuvimba sana mikononi na miguuni, na sio masikioni? I mean, kutokana na maelezo yako, nilitegemea masikio ndio yangekuwa na majereha mengi sana ya ung'ato wa mbu. Au?
   
 9. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kumbe Mkuu Ushirombo ni Dakitari?
  Stay blessed man.
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  QM

  Nashukuru umenielewa vizuri, husikia makelele ya hao mbu kwasababu masikio yako karibu, pamoja na masikio kuwavutia mbu huwa hawezi kunyonya damu kwa urahisi hapo either kwa sababu binadamu naye yuko sensitive sana kuzuia ama wakati mwingine huwa anaficha maeneo hayo kwa shuka ama net. Sasa anacha miguu na mikono ikiwa exposed. Ntakuambia kitu kingine si mbu wote wanahitaji damu, huhitajika zaidi na mbu majike ili waweze kutaga mayai.

  Ushi
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  SteveD

  Carbon dioxide ni kwenye source zote, mdomoni ama ile ya kwenye pua, upo sahihi pia mbu hupenda pia kwenda eneo lenye joto ambalo liko sawa na la binadamu ie 37 celcius, SteveD Mbu hupendelea sehemu zile ambazo mishipa ya damu ipo jirani kurahisisha unyonyaji wa damu. Ni combination ya vitu ambavyo huvutia mbu, nikieleza vyote darasa litakuwa gumu na halitapendeza. Kuna sababu pia ambazo husababisha mbu kuuma zaidi mtu X kuliko Y nitataja kifupi tu, mfano quality ya damu ie Haemoglobin content, iron concetration ambazo hutofautiana watu na watu.

  Nadhani nimejitahidi kufafanua kama unawalakini uliza

  Ushi wa Rombo
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu Chacha wa Mwita Marwa!!

  Mbu huwa hang'ati kiumbe kilichokufa sababu joto linakuwa chini la maiti, hata damu ukiiweka bila kuweka kwenye joto la walau 25 celcius mbu ni viumbe wa ajabu sana tofauti na Nzi!! In short

  Ushi
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dear Mama

  Mbu hang'ati maiti, kwanza joto huwa chini pia kwenye maiti kuna kitendo kinaitwa Rigor mortis is one of the recognizable signs of death that is caused by a chemical change in the muscles after death, causing the limbs of the corpse to become stiff and difficult to move or manipulate na blood vessel huwa zina collapse, Mbu haumi maiti na kwa maana hiyo haenezi malaria. Jamani msichanganye mbu na Inzi. I am I clear mama?

  Son, Ushi
   
 14. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ushi,

  Hakika darasa umelitoa

  Sasa naelewa kwa nini mbu wananizingira sana mimi kuliko watu wengine niliokaa nao karibu... I mean, unakuta tuko watu kibao, lakini mbu wananisumbua peke yangu....lol

  Anyhow, basi angalau wangekuwa wanafyonza hiyo damu mpaka wavimbiwe kimyakimya tu....kuliko kuja kupiga miluzi masikioni. You know! Unakuta mtu umelala usingizi mnono unasikilizia ndoto yako ya "kuloa"....halafu hawa viumbe wasio na aibu, adabu, wala heshima wanakusogelea sikioni na kuanza "ng'oooooooooooo"... mpaka wanakuharibia starehe yako...gademu!

  Ahsante kwa darasa Ushirombo
   
 15. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ushirombo,

  Mbu atajuaje kwamba nikimnga'ta mtu X badala Y nitapata damu yenye "Haemoglobin na iron content" bora zaidi kabla hajang'ata ?

  Na kama sikio na pua zote zinatoa hewa ya pumzi, tena zaidi pua, na kama kivutio cha sikio hapo ni ukaribu wa mishipa ya damu, sasa mbu atajuaje kwamba nikinga'ta karibu na sikio nitakuta mshipa wa damu kiurahisi kuliko karibu na mfupa wa pua ?
   
 16. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ushirombo jitahidi kuwa makini na maelezo yako. Wengi wanategemea knowledge hii kuitumia. Si kweli kuwa mbu jike pekee ndiyo anauma. Ila mbu jike ndiyo anahitaji zaidi damu kwa ajili kutaga. Fortunately mbu jike pekee ndiyo ana uwezo wa kubeba na ku-transmit Plasimodium spp. Lakini ikumbukwe si mbu wote wana transmit malaria. Wengine tofauti kabisa. Kuna Anopheline, Culex ,,,, and so
  Kuwa updated kuhusu kung'atwa na mbu pitia kidogo hii website. http://www.telegraph.co.uk/scienceandtechnology/science/sciencenews/3305140/Why-some-people-are-prone-to-mosquito-bites.html
   
 17. M

  Malila JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  pia sio kila jamii ya mbu wanaimba nyimbo.mbu wengine hufyonza damu kimya kimya.Ukiona mbu anayeimba kanyamaza basi jua anafyonza au kesha fyonza na ameishia. Ni kweli mbu waimbao bongo fleva wasumbufu sana.
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu nimejitahidi kutumia lugha nyepesi kufikisha ujumbe kulingana na maswali. Nafikiri kama ningeandika kila kitu ningeweka confusion kubwa!! NADHANI UMENIPATA
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kuhani

  Maswali mengine bana, mbu ana receptors ambazo husaidia hayo. Sasa tukianza kuzungumzia odorant receptor mjadala utaharibika. Kama una muda soma hili chapisho, very interesting mtu mwenye malaria (mwenye parasites) mbu hupenda zaidi kuuma yeye sababu ni rahisi hapo, adapation na evolution parasites waweze kuwa propagated kwenye population.
   
 20. M

  Mama JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  tatizo ni huyu

  malaria.jpg
   
Loading...