Ni ngumu kutuelewa

Huo mda wa kumuelewa mtu niliyekutan nae ukubwan natoa wapi kikubwa ananipa huduma ninazotak bas inatosha
Ila sisi mnataka tuwaelewe na tusipowaelewa kosa mnasema hatufai kuolewa? Ajabu
 
Akiwa anafanya effort atleast na mimi naweza jisogeza ila sio mzima mzima
Kwahiyo kila kitu ni hadi aanze mwanamke? Mbona kuumbwa alianza mwanaume? Si mnasema nyie ni viongozi wetu kwenye kila kitu mbona kwenye mapenzi mnataka sisi ndo tuwe viongozi wenu? Imeandikwa wapi?
 
Kwahiyo kila kitu ni hadi aanze mwanamke? Mbona kuumbwa alianza mwanaume? Si mnasema nyie ni viongozi wetu kwenye kila kitu mbona kwenye mapenzi mnataka sisi ndo tuwe viongozi wenu? Imeandikwa wapi?
Usiwape wengine misimamo yangu hii ni kwa mujib ya mimi

Ila mwanamke anatakiwa kumheshim mwanaume nani jukum la mwanaume kumpenda mwanamke
 
Usiwape wengine misimamo yangu hii ni kwa mujib ya mimi

Ila mwanamke anatakiwa kumheshim mwanaume nani jukum la mwanaume kumpenda mwanamke
Siyo wewe tu nasikia wanaume wengi wanasema eti wao kupenda mwanamke ni hadi huyo mwanamke ndo aanze kumheshimu sasa nani hapo anatakiwa aanze? Mwanaume kumpenda mwanamke au mwanamke kumheshimu mwanaume? Na biblia haijaspecify nani aanze ila wanaume wengi watakwambia mwanamke ndo aanze kumheshimu mwanaume

Ila mimi naona mwanaume ndo anatakiwa aanze kumpenda mwanamke kwa sababu mbili moja kwa sababu ninyi ndo mlianza kuumbwa na ndo viongozi wetu kwenye kila kitu mbili ninyi ndo mnaotongoza sasa hauwezi kumtongoza mwanamke akakukubalia halafu unamsubiri tena yeye ndo aanza wewe uliyetongoza ndo unatakiwa uanze kuonyesha yale uliyoyanadi kwenye mtongozo wako halafu mwanamke yeye atatambaa na beat lako tu

Sisi wanawake hatuna roho ngumu kihivyo ila nyie wanaume unaweza ukajitoa kwa mwanaume ukamfanyia kila kitu ila bado linakuacha linaenda kwa mwanamke ambaye hakuna cha maana anachompa ndo maana kwenye mapenzi wanaoumia sana ni wanawake kuliko wanaume sema sisi tunasononeka kimya kimya tunanyanyuka tunaendelea na safari ila nyie unakuta huyo ndo mwanamke wako wa kwanza kukutenda ila unalalamika utasema umeonewa yaani wakati hayo mambo yapo kwa jinsia zote

Ila tu nyie mnadhani hapa duniani kwenye swala la mapenzi mlikuja kustarehe halafu wanawake ndo tulikuja kuteseka kwahiyo mwanaume ndo anatakiwa aanze kumpenda mwanamke na huko ni pamoja na kumjali na kutokumsaliti halafu na yeye ndo atakuheshimu sasa tatizo linakuja wanaume wengi siku hizi hapo kwenye kutokutusaliti pamewashinda which means mapenzi ya yamewashinda na ndo maana hata na sisi wanawake kuwaheshimu kumeshatushinda
 
Unaelewa tofauti ya unachokihoji na nukuu unayoihoji?
 
Hakuna tofauti yoyote hapo yeye kataja maovu ya wanawake na mimi nimetaja maovu ya wanaume hivi wanaume kwanini kila mnapoambiwa ukweli hamtaki kukubali mnatafuta sababu za kujitetea tu?
Unaelewa tofauti ya unachokihoji na nukuu unayoihoji?
 
Hivi sulemani alitubu kisa kuwa na masuria yote hayo? Au alitubia zambi zake alizofanya ambazo wewe na Mimi hatujui zote na hatujui ni zipi?

Tatizo mnapenda kutafuta usawa sana western culture zinawaharibu sana ndio uasherati na uzinzi ni zambi kwa wote ila ndo hvo sisi wanaume suala la kucheat kwetu ni changamoto sana ambayo wachache wetu wameweza kuikabili lakin haimaanishi tumeihalalisha Achane mashindano yasikuwa ya maana hapa ni zahiri comment yako inaonyesha au inataka usawa hio kitu haiwezekani mtabaki chini ya matakwa yetu
 
Mbona haujanielewa? Mimi nimesema uzinzi na uasherati ni dhambi kutokana na maandiko na siyo kutokana na kutaka usawa tatizo wanaume mnafanya dhambi kwa makusudi kwa kutaka kujitofautisha na wanawake

Na mnadhani wanawake ni malaika kwamba wao ndo hawawezi kufanya dhambi kama kweli kujizuia kuchepuka lingekuwa ni swala gumu kiasi hicho basi Mungu angewaruhusu kuzini na kufanya uasherati

Ila kwa vile amewakataza wote basi wanaume mnaosema kuwa hilo swala ni gumu mnajiendekeza tu wakati kujizuia mnaweza sana na hakuna excuse kwa mwanaume na mwanamke yeyote mzinzi au muasherati wote wana dhambi mbele za Mungu

Wote watahukumiwa wasipotubu na wakitubu watasamehewa sasa nyie endeleeni kuleta udume wenu hadi kwenye sheria za Mungu kwa kudhani mnatukomoa sisi kumbe mnajikomoa wenyewe eti viongozi viongozi ndo mfanye dhambi kwa makusudi? Yes hayo ni makusudi sababu Mungu ameshakataza bahati mbaya unaijua wewe?
 
Akiringa unakuja hapa una adili na mengine shida ya nini

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
Sawa mwanaharakati
 
Nyie sometimes hata mkiwa mmechoka tu ni mwendo wa kugombana na kununiana na hata wivu huwapelekea kutununia ama msipotimiziwa au kuruhusiwa mambo yenu pia mnanuna, binafsi nawafahamu kiasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…