Ni nani waliongeza cha juu kwenye manunuzi ya ndege ya mizigo?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,652
698,266
Mama kalalamika kwamba invoice ya mwisho ilikuwa tulipe $37,000,000 lakini ikaja invoice ya $86,000,000 ongezeko la zaidi ya asilimia 100 nje ya mkataba wa awali na mama alipohoji akaambiwa spare zimepanda bei.. Je ni nani wanaruhusu malipo ya serikali yatoke? Hawa wafuatao sahihi zao ndio zinahusika.

1. Mwanasheria Mkuu wa Serikali
2. Waziri wa fedha
3. Mlipaji Mkuu wa Serikali
4. Gavana wao BoT
5. Waziri wa Uinzi(?) Kwa vifaa vya usalama na jeshi
6. CDF (?) Kwa vifaa vya usalama na jeshi
7. Mkaguzi Mkuu wa Serikali?
8....
9....

Hiyo ndio timu na sidhani kama kuna wengine nje ya hao. Je, mama aliposema kwamba kama huko nyuma walikula hazikuwatosha.. Alimaanisha hawa ama?

Kwa nchi zinazojali utawala wa kisheria katika uhalisia wake nusu ya hao hapo juu kufikia muda huu hawakupaswa kuwepo ofisini.
 
1: ATCL Management
2: TGFA Management
3: Ofisi ya AG
4: Ofisi ya Mlipaji Mkuu wa Serikali

Etc, hizo ofisi hawawezi kwepa hii kadhia, hizo ni fedha nyingi mnooo... Naamini hadi Mama kachukia vile, lazima kachukuza na kawaita na kujua madudu yote na upigaji wa wazi wazi, ndio maana kasema watupishe yaani wajiuzulu wao wenyewe.

Sasa wasipojiuzulu au kuachia nafasi zao, itabidi haraka Rais Mama Samia, awafukuze kazi haraka kwa barua toka Ikulu.
 
1: ATCL Management
2: TGFA Management
3: Ofisi ya AG
4: Ofisi ya Mlipaji Mkuu wa Serikali

Etc, hizo ofisi hawawezi kwepa hii kadhia, hizo ni fedha nyingi mnooo... Naamini hadi Mama kachukia vile, lazima kachukuza na kawaita na kujua madudu yote na upigaji wa wazi wazi, ndio maana kasema watupishe yaani wajiuzulu wao wenyewe.
Sasa wasipojiuzulu au kuachia nafasi zao, itabidi haraka Mh. Rais Mama Samia, awafukuze kazi haraka kwa barua toka Ikulu.
Hawezi, mkono wa mstaafu uko hapo.

Narudia tena, hawezi.

Hakuna wa kufukuzwa hata mmoja.

Mama kama angekuwa na uwezo huo hakupaswa kutoka na kutuambia. Tulitakiwa tuone watu ni fired bila sisi kujua kinachoendelea. Ndo uongozi.

Mama aliona Magu hana huruma. Akasahau kuwa hii nchi ina wajanja fulani wanaendesha nchi kama choo binafsi.

Atamkumbuka Magu, na nchi ishamshinda. Watu wanapekenyua hadi kilemba chake.
 
Baada ya ulafi wa mali za umma kuanikwa na CAG, hakika rais wetu Samia anatakiwa asaidiwe pakubwa na kwa haraka, ikiwemo kumwombea Mungu ampe ujasiri, akili na hekima itokayo juu.

Kakwama kabisa na kuishia tu kulalamika na kutukana: "...stupid..., ...pumbavu..."!

Nani ataogopa kuendelea kuiba na kula fedha za umma kwa kulalamikiwa na kutukanwa tu bila kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria?!

Credit: Gwappo Mwakatobe
 
1: ATCL Management
2: TGFA Management
3: Ofisi ya AG
4: Ofisi ya Mlipaji Mkuu wa Serikali

Etc, hizo ofisi hawawezi kwepa hii kadhia, hizo ni fedha nyingi mnooo... Naamini hadi Mama kachukia vile, lazima kachukuza na kawaita na kujua madudu yote na upigaji wa wazi wazi, ndio maana kasema watupishe yaani wajiuzulu wao wenyewe.
Sasa wasipojiuzulu au kuachia nafasi zao, itabidi haraka Mh. Rais Mama Samia, awafukuze kazi haraka kwa barua toka Ikulu.
Kwhy wewe Mwigulu unaona hiyo list Yako ndio inafaa kujiuzulu?

Muda mwingine muwe mnaona aibu mnapotuibia Watanzania
 
Mama kalalamika kwamba invoice ya mwisho ilikuwa tulipe $37,000,000 lakini ikaja invoice ya $86,000,000 ongezeko la zaidi ya asilimia 100 nje ya mkataba wa awali na mama alipohoji akaambiwa spare zimepanda bei.. Je ni nani wanaruhusu malipo ya serikali yatoke? Hawa wafuatao sahihi zao ndio zinahusika
1. Mwanasheria mkuu wa serikali
2. Waziri wa fedha
3. Mlipaji mkuu wa serikali
4.Gavana
5. Waziri wa ulinzi(?) Kwa vifaa vya usalama na jeshi
6. CDF(?) Kwa vifaa vya usalama na jeshi
7. Mkaguzi mkuu wa serikali?
8....
9....
Hiyo ndio timu na sidhani kama kuna wengine nje ya hao.. Je mama aliposema kwama kama huko nyuma walikula hazikuwatosha.. Alimaanisha hawa ama?

Kwa nchi zinazojali utawala wa kisheria katika uhalisia wake nusu ya hao hapo juu kufikia muda huu hawakupaswa kuwepo ofisini
Hao wote ulio taja hawana nguvu kuamua kazi yao ni kuweka sahihi tu kuna clique yenye nguvu ndani ya chama yenye maamuzi ya mwisho........ndo wanao panga hela ya ziada itagawanywa je, hilo jambo ni mchakato mrefu sio tukio sema kwa hilo kulikua na miscommunication kati ya Raisi na procurement clique ila itawekwa sawa bila kuvictimize mtu yoyote. Nchi ina wenyewe.
 
Kwenye bili ya dola 37 elfu ikaongezwa cha juu dola 49 elfu halafu watu kama hawa uwaambie kuhusu katiba mpya watakuelewa kweli

Yaani watu wezi sana, $ 49 mil ni sawa na fedha zetu tshs 114 bil, watu hawa hawajali kabisa, mimi naona Mama angewafukuza pale pale aliposema waondoke wenyewe, yaani angesema barua zao za kufukuzwa kazi zipo tayari leo baada ya kikao hiki waondoke kabisa wezi hawa wakubwa sana, sbb itakuwa ni chain kubwa ya wapigaji ktk dili hilo
 
Hao wote ulio taja hawana nguvu kuamua kazi yao ni kuweka sahihi tu kuna clique yenye nguvu ndani ya chama yenye maamuzi ya mwisho........ndo wanao panga hela ya ziada itagawanywa je, hilo jambo ni mchakato mrefu sio tukio sema kwa hilo kulikua na miscommunication kati ya Raisi na procurement clique ila itawekwa sawa bila kuvictimize mtu yoyote. Nchi ina wenyewe.
Ila this time mbona kama wamepiga ndefu sana? Ongezeko la zaidi asilimia 100
 
Yaani watu wezi sana, $ 49 mil ni sawa na fedha zetu tshs 114 bil, watu hawa hawajali kabisa, mimi naona Mama angewafukuza pale pale aliposema waondoke wenyewe, yaani angesema barua zao za kufukuzwa kazi zipo tayari leo baada ya kikao hiki waondoke kabisa wezi hawa wakubwa sana, sbb itakuwa ni chain kubwa ya wapigaji ktk dili hilo
Kuna baadhi ya nchi wangekamatiwa palepale ukumbini maana waliwepo wote
 
Back
Top Bottom