Sheria mpya ya Manunuzi ya vitu vya "mtumba" bila PPRA ni kupanua ubadhirifu

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,552
11,902
8Video Clip ipo Chini"Mwigulu Kama Makamba na Nape! Wanasaka za Uchaguzi (ndoto za Urais)"
Jana, 08/09/2023 huko Dodoma Serikali kupitia Bunge lake ilipitisha sheria mpya ya manunuzi ya serikali.

Ambapo sasa ni ruksa kwa serikali au taasisi yoyote ile ya Umma nchini inaweza kununua vifaa au mitambo yoyote ambayo imekwisha tumika (Second hand used items) kwa lugha ya Kiswahili "mtumba"

Kibaya zaidi ni kwamba katika sheria hiyo,Mzabuni ambaye ni serikali,atafanya tathmini ya ubora wa bidhaa au mitambo husika bila kulazimika kufuata muongozo wa manunuzi ya serikali PPRA.

Bali imetamkwa kwamba badala yake serikali itamtumia Mwanasheria mkuu wa Serikali na pamoja na tume maalumu ya wayaalamu ili kujiridhisha na kuhakiki ubora wa bidhaa au mitambo husika.

Hapo ni wazi kabisa Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba anataka kupanua wigo wa kutafuta pesa za kuhonga na kuitekeleza Ndoto yake ya kuusaka urais wa Mawe.

Tumekwisha shuhudia kashfa nyingi sana nchi kupitia manunuzi ya Umma,tena udanganyifu kwenye vitu ambavyo ni vipya.

Je, hili la waziri kuteua watu na kuwaita jopo la wataalamu.Si ndio yatakuwa yale ya MV Magogoni kwa mfano wa hivi karibuni?

Au yale ya Makamba na Bodi yake ya Tanesco tuliposhudia akiwatoa wataalamu bobezi.

Na kisha kuwaweka watu wake wengine wakitokewa kampuni ya ving'amuzi huko DSTV.

Matokeo yake ameiacha Tanesco ikiwa hoi na nchi ikiwa gizani.

Ni michezo ya mawaziri wa Samia kundi hili la Kimfumo Sambamba na Nape (Anayetupiga kupitia Kampuni za Simu na Bundle).

Na January aliyekwisha tupiga kupitia mikataba ya kifisadi huko Nishati kuanzia Tanesco,Umeme wa Upepo,Gesi ya Mtwara nk.

Huu ni Uhunni mwingine toka kwa wahuni ndani ya CCM na unapaswa kukemewa na kupingwa hadharani bila chenga.


View: https://youtu.be/2id2Un32SSw?si=xxTTqn_7J2KUCr3bPia, soma: Waziri Mwigulu apendekeza sheria mpya ya Serikali kununua vitu vilivyotumika (mtumba)
 
Mwigulu anajiongezea wigo wa kupiga fedha; rushwa plus bakshish ya 10%!
 
Hakika kibibi Betina kinalipeleka Taifa katika janga kubwa la kijamii na kiuchumi! Kinawaza fedha tu za wizi yeye na mume wake!
 
Back
Top Bottom