Ni nani Dr. William Mgimwa?

Hahaa..!! Elimu yake ni ndogo sana Mkuu..!! Hapo tuombe mungu uzoefu wake wa vijikazi vyake alivyofanya Tanzania ndio utasaidia. Vinginevyo hana lolote la kuiingiza Tanzania katika mchaka mchaka wa kimbizo la kiuchumi duniani. Elimu tunazosomea Tanzania ni kwa ajili ya shughuli za mimi na wewe na si kwa muunganiko wa kidunia ambao kwa wizara nyeti kama ya Fedha inahitaji ukamili. Endelea kuota tu..!!
 
Amon Nsekela Bank accademy sasa ni Ruco kipo iringa mjini. suala la Dr Mgimwa anaweza au hawezi tusubiri tutajua kwani mkulo alipoingia ilikuwaje? cha msingi tu mzee asiwasikilize akina Lukuvi watamwendesha sana
 
Lukuvi ni mweledi na amebobea kwenye fitna
 
Wakuu wanaoijua Mzumbe watufahamishe kama mwaka 1991 tayari ilikuwa inatoa masters degreee tena za MBA. Pili huyu Waziri Mteule anatumia initial ya Dr lakini kwenye CV aliyoiweka kwenye tovuti ya bunge haionyeshi kama ana P.hD ya kusomea. Ana udokta wa aina nini? Haya mambo watu wengine wanayachukulia juu juu lakini kwenye nchi za watu is a serious matter.

Watu wanaweza kudai tuna attack his personally au elimu sio kigezo cha kuwa kiongozi bora lakini nafikiri kuna umuhimu wa kujua elimu za viongozi wetu wa ngazi za juu kama ni za ukweli au ni za kuchakachua. Elimu sio kigezo pekee cha uongozi lakini watu wasidanganye ili kupata uongozi.

Inawezekama labda amepata P.hD yake baada ya kuweka CV yake kwenye tovuti ya bunge lakini ni bora aka-upadate CV yake kama ni hivyo. Hatutaki kuwa na waziri mwingine wa fedha ambaye elimu yake ni ya mashaka.
 
Inaonyesha ni jinsi gani uelewa wako wa mambo ya taaluma ulivo mdogo.
Mfumo wa IMF, IAA na Mzumbe unamundaa mwanafunzi kuwa mtendaji moja kwa moja once anapomaliza na kuingia kazini.
Mfumo wa UD & SUA unamundaa mwanafunzi kuwa analytical, thinker and critical. Hapa ni sawa na kumlinganisha graduate wa Engineering na fundi mchundo wanapoanza kazi, fundi mchundo ataonekana mzuri kuliko engineer but with time an engineer will excel above fundi mchundo.
Mwisho naomba unijubu maswali yafutayo;
1. Si kweli kwamba wanafunzi wengi wanaojoin hizo taasisi (IAA, Mzumbe, & IFM) performance zao za Form VI ziko chini kulinganisha na wanaojoin UD?
2. Nitajie at least three well renown, distinguished, and respected academicians/scholars waliopitia any of those institutions.
 
Mkuu naamini hatafanya kazi peke yake. Nchi hii ina waataalamu wengi na wazuri watasaidiana ktk kujenga uchumi wetu. Naamini ktk dhana nzima ya uwajibikaji bila kusahau TEAM WORK. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu ndg zangu.
 
Nundu, Ngeleja, Mkullo etc walikuwa wanafanya kazi peke yao? Mungu mnamsingizia sasa, amsaidie kutenda makuu mtu incompetent!

Ingawa sisemi kwamba mlengwa kwenye uzi huu si competent, lakini maswali yanayohojiwa juu yake, si ya kuyapuuzia hata kidogo. Tuko mama ntilie prominent na MBA zetu, lakini tuna hakika kazi ya uwaziri hatuiwezi, si kwa vile hatuna vigezo, bali sio competent in the current global economic and development perspective.

Tunahitaji mtu ambaye pamoja na vigezo vya elimu na uzoefu (iwe kitaifa au kimataifa) awe competent kama masuala yanayohusiana na kazi husika.
 
NB: siku zote jua kufanya vizuri form six sio kufanya vizuri chuoni, na kwa taarifa yako wanfunzi wengi wazuri huwa hawafanyi vizuri formsix kwa sababu system iliyopo haiwafevi!
Ww umetumia data zipi kuandika haya? Kwa tafsiri yako inabidi wanafunzi wanaopata zero and div. 4 ndio wapewe kipaumbele kuingia vyuoni halafu tuwaache na wenye div. I na II, au sio?
 
Bora na wewe mkuu umeona hoja tuyajaribu kujadili hapa ingawa kuna watu wanaleta ushabiki na upotoshaji wa hovyo!

CV haionishi mambo ya msingi ambayo tayari tumejulishwa. Tumeambiwa waziri wetu ni Dr, ila CV yake haionishi kitu chochote kuprove kwamba yeye kweli ni Dr. Pia CV yake ina makosa madogo madogo ya kiuandishi ambayo kwa watu makini wanapata mashaka kama waziri wetu kweli yuko serious.

Tatizo ni kwamba watu wengi wanahisi kuwa tunahoji haya kwa sababu ya roho mbaya, wivu au njaa!! Mtazamo wa namna hiyo ni wa hatari sana na kwakweli unanisikitisha!
 
Hujui kwamba JK anapingwa kwa dini yake?.Ushahidi rejea malalamiko ya Mtei kuhusu tume ya katiba.Mbona sijamsikia mzee akija hapa jamvini na kulalamika Kikwete kuwateua mawaziri wengi wakristo?.Hapo unapata jibu kwanin CDM inampinga kikwete kwa kila jambo hata jema.
 
Hivi kumbe kuna chuo cha NBC...(The National Bank of Commerce (NBC) - College). Kiko WAPI?

Kipo Iringa mjini, kiliuzwa RC Church walikinunua wameanzisha Constituent college ya SAUT inaitwa RUCO = Ruaha University College!
 
Kimsingi CV ya Dr. Mgimwa ni katika masuala ya fedha ni nzuri, ila naungana na Mkweche kwamba kwa aina ya siasa za nchi yetu wasomi wamekuwa hawafanyi vizuri maana wao hupenda kufanya mambo kwa kuzingatia ueledi lakini mfumo uliopo unataka siasa 90% Ueledi 10%.

Changamoto nyingine kwa Dr. Mgimwa na wasomi wengine walioibukia kwenye siasa nakupew majukumu yw Uwaziri ni kile kinachoitwa ILANI YA CHAMA TAWALA ambayo hata kama haizingatii kuleta manufaa kwa watanzania inabidi aifuate tu na mijamaa kibao inakuwa standby kuona kama wasomi wanatoka nje ya mstari. Lakini huu ndiyo mwendelezo wa mabadiliko angalau wanasiasa wenye ueledi wanapewa wizara kuendana na taaluma zao. Mfano Prof. Muhongo na Dr. Mgimwa.

Lila la kheri Dr. Mgimwa tumia ueledi wako tafadhali
 
Narudi Hiyo CV ya Kwenye Tovuti ya Bunge ina Matatizo za Kiuandishi!
Naweka wasifu wa Waziri wa Fedha,Kama alivyoutoa kwenye kipeperushi wakati wa kura za maoni 2010,Kipeperushi hata mie ninacho!ni mbunge wetu hapa kala -iringa,NIMEKIKOPI KAMA KILIVO,SIJAONGEZA WALA KUPUNGUZA NENO
1.JINA:William Agustao Mgimwa
2.MAHALI:Kijiji cha Magunga Tarafa ya Kiponzel
3.ELIMUπŸ™a)Digrii Uzamivu(PhD-Finance 2003)
(b)Digrii Uzamili(MBA Finance 1991)
(c)Stashahada ya juu ya mambo ya Fedha(PGDMFM)(1983-1984)
(D)Stashahada ya juu ya Taaluma ya Benki(ADBA)1978
4.MAFUNZO YA MUDA MFUPI(SHORT COURSES)
NCHI MIAKA NA MAFUNZO ALIOHUDHURIA KIUFUPI
UINGEREZA (1992,1993,1995,1997,2002)
Mafunzo ya Taaluma ya Benki na Uchumi Fedha
USA(AMERICA) (1998,2002,2001)Taaluma ya Benki na Uchumi Fedha
INDIA(BOMBAI&PUNE) (1993,1995,2001,2004,2007)Taaluma ya Fedha na Utawala wa Mabenki
PHILIPINE(UFILIPINO) (2002)Taaluma ya Mafunzo ya Wakuu wa vyuo vya Mabenki
ZIMBABWE (1998)Taaluma ya Fedha na Uchumi)
SWITZERLAND (2001)Taaluma ya Kutunza Mabenki(Risk management for Banks)
5.UZOEFU WA KAZI KWA UFUPI
KAZI:

  1. Mhsibu wa Benki NBC(1980)
  2. Meneja wa Benki NBC(1981)
  3. Mwalimu wa Chuo cha Benki Iringa(1981-1989)
  4. Meneja Mfawidhi wa Benki NBC(1996-1997)
  5. Mkurugenzi wa Benki NBC(1997-2000)
  6. Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu(BOT)-Mwanza(2000-2010)
6.UONGOZI KATIKA JAMII
a. Mwenyekiti wa NUTA-Chama cha wafanyakazi NBC-Mtwara(1978-1979)
b. Mwakilishi wa wafanyakazi ktk Baraza kuu la NBc(1982-1989)
c. Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Tawi
d. Diwani wa Kata ya Gangilonga Iringa(1991-1994)
e. Mjumbe Baraza la Wdhamini Mwanza-Children Foundation
f. Mkurugenzi(Board Member) waMikopo y Elimu ya Juu(HESLB)
7.MACHAPISHO NA VITABU ALIVYOANDIKA
1.A Training Manual of Project Planning Appraisal and Implemntation for NBC Training College 1993
2. Liquidity Management-A Dialema for BanksπŸ˜›rofessional Accountants Journal Vol.8 No.1 1994
3. Commercial Bank Lending-Tanzania Bankers Journal Issue No.8 of 1995
4. Banks and Liquidity Risk Management-NIBM Journal of India 2005
5. Advanced Credit Operations-Kitabu cha kufundishia Elimu ya Mikopo ya Mabenki-2007
6. Advanced Treasury Management- Kitabu cha Taaluma ya Uchuni Fedha na Hazina-2009
 
Maelezo haya mimi Mkweche nimeyaandika kama yalivo kwenye vipeperushi tulivyopewaga 2010 wakati wa mchakato wa kura za maoni Jimbo la kalenga!Nimeyakopi kama yalivo na mkitaka niScan kipeperushi pia naweza ninacho!
ila huyu ndio Dr mgimwa.
1.JINA:William Agustao Mgimwa
2.MAHALI:Kijiji cha Magunga Tarafa ya Kiponzelo
3.ELIMUπŸ™a)Digrii Uzamivu(PhD-Finance 2003)
(b)Digrii Uzamili(MBA Finance 1991)
(c)Stashahada ya juu ya mambo ya Fedha(PGDMFM)(1983-1984)
(D)Stashahada ya juu ya Taaluma ya Benki(ADBA)1978
4.MAFUNZO YA MUDA MFUPI(SHORT COURSES)
NCHI MIAKA NA MAFUNZO ALIOHUDHURIA KIUFUPI
UINGEREZA (1992,1993,1995,1997,2002)
Mafunzo ya Taaluma ya Benki na Uchumi Fedha
USA(AMERICA) (1998,2002,2001)Taaluma ya Benki na Uchumi Fedha
INDIA(BOMBAI&PUNE) (1993,1995,2001,2004,2007)Taaluma ya Fedha na Utawala wa Mabenki
PHILIPINE(UFILIPINO) (2002)Taaluma ya Mafunzo ya Wakuu wa vyuo vya Mabenki
ZIMBABWE (1998)Taaluma ya Fedha na Uchumi)
SWITZERLAND (2001)Taaluma ya Kutunza Mabenki(Risk management for Banks)
5.UZOEFU WA KAZI KWA UFUPI
KAZI:

  1. Mhsibu wa Benki NBC(1980)
  2. Meneja wa Benki NBC(1981)
  3. Mwalimu wa Chuo cha Benki Iringa(1981-1989)
  4. Meneja Mfawidhi wa Benki NBC(1996-1997)
  5. Mkurugenzi wa Benki NBC(1997-2000)
  6. Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu(BOT)-Mwanza(2000-2010)
6.UONGOZI KATIKA JAMII
a. Mwenyekiti wa NUTA-Chama cha wafanyakazi NBC-Mtwara(1978-1979)
b. Mwakilishi wa wafanyakazi ktk Baraza kuu la NBc(1982-1989)
c. Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Tawi
d. Diwani wa Kata ya Gangilonga Iringa(1991-1994)
e. Mjumbe Baraza la Wdhamini Mwanza-Children Foundation
f. Mkurugenzi(Board Member) waMikopo y Elimu ya Juu(HESLB)
7.MACHAPISHO NA VITABU ALIVYOANDIKA
1.A Training Manual of Project Planning Appraisal and Implemntation for NBC Training College 1993
2. Liquidity Management-A Dialema for BanksπŸ˜›rofessional Accountants Journal Vol.8 No.1 1994
3. Commercial Bank Lending-Tanzania Bankers Journal Issue No.8 of 1995
4. Banks and Liquidity Risk Management-NIBM Journal of India 2005
5. Advanced Credit Operations-Kitabu cha kufundishia Elimu ya Mikopo ya Mabenki-2007
6. Advanced Treasury Management- Kitabu cha Taaluma ya Uchuni Fedha na Hazina-2009

sijawahi kuona mtu anasifiwa kabla hata hajaanza kazi...Kikwete nae tulimsifu sana 2005.. tulieni tulieni subirini kwanza... atakapoanza kutoa misamaha ya kodi nyinyi nyinyi ndio mtaanza kumponda hapa...:hand:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…