Ni nani Dr. William Mgimwa?

Ni nani Dr. William Mgimwa?

Nilikua kwa website ya Tz parliament kucheck cv ya waziri wa fedha nikastaajabu kuona anaitwa dr na huku hana elimu hiyo ikanibidi nije jf labda nitapata chochote juu ya udr wake cha ajabu hamna mtu anaejua huyu bwana ka doctorate kutoka chuo gani. Hivi kujiita dr ni sifa ccm? Hii nchi inaenda wapi na elimu za uongo mara dr. mary nagu, dr. mary mwanjelwa na sasa dr mgimwa, kitu inabidi kifanyike hapa.
 
Kwa jinsi hotuba yake ilivyokuwa jana, na kwa jinsi aliwasilisha bajeti; amini usiamini anapwaya sana. Ni kama hajui anachosema ana kukifanya; mzaha mwingi nchi inateketea, haina majibu ya maswali ya wafanyakazi mei mosi, haina majibu kwa mtanzania wa kawaida na shida zake za kila siku.
 
Ukweli ni msomi, mchumi. Lakini jambo moja linamtia doa. Akiwa NBC ndiye alikuwa afisa aliyeaminiwa na serikali kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalam na katika ubinafsishaji wa NBC. Alikuwa yeye na Bw Singili, MD wa Azania Bank. Ingawa inadaiwa alijitahidi sana kuukataa utaratibu wa ubinafsishaji huo, wakubwa walimtishia na hatimaye NBC ikauzwa kwa sh bilioni 18. Baadaye, makaburu wakachakachua, ikadaiwa, ati uundaji wa NBC (1997) Limited katika kupitia mahesabu, nayo ilikuwa inadaiwa na NBC Sh bilioni 18. Kwa hiyo NBC ikauzwa sh sifuri! sifuriiiiii! (hujui hesabu bilioni 18 toa bilioni 18=Sifuriii. Kwa hiyo atakumbukwa kwa kuuza NBC kwa bei sifuriiiiii!
 
Nimeshangaa kuona amefundisha chuo cha benki toka mwaka 81-89, ni kuwa chuo cha benki dr. Amon Nsekela kilianza kazi mwaka 87 na ndipo nilipomfahamu wakati mzee wangu akiwa mwalimu pale. Cv yake haijakaa vizuri.
 
Kwa jinsi hotuba yake ilivyokuwa jana, na kwa jinsi aliwasilisha bajeti; amini usiamini anapwaya sana. Ni kama hajui anachosema ana kukifanya; mzaha mwingi nchi inateketea, haina majibu ya maswali ya wafanyakazi mei mosi, haina majibu kwa mtanzania wa kawaida na shida zake za kila siku.
. Naomba kukuuliza mheshimiwa yafuatayo:
i. Kwani Mh. Waziri kaandaa hiyo bajeti peke yake?
ii. Wataalamu wa wizara ya Fedha, BOT, Mashirika ya Fedha nk hawakuhusika?
iii. Je ana muda gani hapo HAZINA hata tumtoe makosa kupitia bajeti aliyokuta imeandaliwa?.
iv. Mwisho usisahau ni mara ya kwanza yeye kusimama Bungeni na kupewa jukumu kubwa kama hili. It is obvious anaweza kuwa ametetereka ktk kuongea na kuwasilisha mada. Hilo lisitufanye tuendelee kumuona hafai.
v. Watanzania wenzangu safari ya ukombozi wa Mtanzania bado ni ndefu hivyo nasisitiza tumpe muda anaweza kuwa Daudi aliyemuua Goliati. Tupunguze negativity kubwa tuliyonayo inayosababisha upofu hata yaliyo mazuri hatuyaoni wala hatutayaona tukiendelea hivi. Tumuombee yeye na viongozi wengine watuongoze vizuri na kwa uadilifu, pia na tuiombee Tanzania yetu, nani ajuae Daudi amepatikana?
Qeen Esther
 
Naomba ufute kauli yako, TUMAINI kinatoa wanasheria vilaza..vilevile majority ya watu wanaoenda kusoma IFM, IAA na MZUMBE wanakuwa hawakupata credit nzuri Form VI za kuwawezesha kuingia UD kusoma BCOM, BA Economics nk. Tunao makazini, wengi wao ni mzigo tu hata huku maofisini.

Acha ujinga.
 
. Naomba kukuuliza mheshimiwa yafuatayo:
i. Kwani Mh. Waziri kaandaa hiyo bajeti peke yake?
ii. Wataalamu wa wizara ya Fedha, BOT, Mashirika ya Fedha nk hawakuhusika?
iii. Je ana muda gani hapo HAZINA hata tumtoe makosa kupitia bajeti aliyokuta imeandaliwa?.
iv. Mwisho usisahau ni mara ya kwanza yeye kusimama Bungeni na kupewa jukumu kubwa kama hili. It is obvious anaweza kuwa ametetereka ktk kuongea na kuwasilisha mada. Hilo lisitufanye tuendelee kumuona hafai.
v. Watanzania wenzangu safari ya ukombozi wa Mtanzania bado ni ndefu hivyo nasisitiza tumpe muda anaweza kuwa Daudi aliyemuua Goliati. Tupunguze negativity kubwa tuliyonayo inayosababisha upofu hata yaliyo mazuri hatuyaoni wala hatutayaona tukiendelea hivi. Tumuombee yeye na viongozi wengine watuongoze vizuri na kwa uadilifu, pia na tuiombee Tanzania yetu, nani ajuae Daudi amepatikana?
Qeen Esther

Utakuwa umesikia hata wabunge wa CCM ambao ni vilaza sana, wamekubaliana na mawazo yangu kuwa anapwaya, ameandaa bajeti kama ya city council, maneno ya mbunge wa CCM.

Ukweli ni kwamba hajaandaa pekee yake lakini ni flag carrier, hakuna upanuzi wa wigo wa walipa kodi, hakuna mipango ya kuongeza kipato ukitoa kuongeza kodi kwa walipakodi waliopo, mfanyakazi kodi bado kubwa sana, ukilipwa mil 3 unalipa kodi mil 1 kila mwezi, je wafanyabiasha wanalipa hiyo kodi? kwa nini mfanyakazi ambaye ni maskini ukilinganisha na wafanyabiashara?? JIBU ni dogo, wabunge hawalipi kodi kwenye mishahara yao, na pia ndo wafanyabiashara wakubwa TZ. Sasa waziri angevunja hilo, wabunge walipe kodi kwa mishahara, na wafanyabiashara kodi iongezeke kama ilivyo kwa mlipwa mshahara.

Je Mgimwa kama yuko fit kichwani, anadhani ni dhambi kunywa soda au bia? mbona nchi inaendeshwa na wanywa bia na soda, kodi kila mwaka inapanda kwenye maeneo hayo, ni kivipi??? Migodi na mikataba mibovu mbona haikuguswa?? Wezi au mafsadi je?, hiyo fedha mbona haipo kwenye bajeti, hii ina maana serikali haitaki kufuatilia watu hawa na kurejesha fedha zetu???

Pamoja na kukubaliana kwa kina na Mhagama kuwa bajeti ni mbovu tena kama ya city council, bado sikubaliani na hoja ya wabunge wa CCM eti pikipiki zisilipe kodi ya mapato, huu ni upumbavu mkubwa. Hakuna mtu ambaye afanye biashara bila kulipa kodi ya mapato, asiwepo ili kujenga uwezo wa kujitegemea, tena kodi yenyewe 90,000/-kwa mwaka!!! mimi napendekeza hata watoto wadogo from 5yrs walipe kodi ya 500/-kwa mwaka ili kuwajengea ufahamu na uzalendo kwa nchi yao. wajue ni wajibu kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yao.

Kwa ufupi bajeti haina matarajio ya watu wenye akili timamu, ni mbaya haina jipya wala haitupeleki kwenye kujitegemea, kukuza uchumi na mengineyo. Japo mabadiliko yamefanyika juzi tu, lakini haimanisha waziri wa fedha aseme pumba harafu tunyamaze vile kaingia juzi, hilo ni kosa kubwa, ingekuwa uwezo wangu vile CCM hakuna watu kwa sasa wenye akili nzuri, ZITO angepewa hiyo wizara na bajeti mbadala yake ingekuwa ndo bajeti ya nchi 2012/13. Tusione aibu, tunajenga nchi.
 
I know him.Ni mtu muadilifu na mchapa kazi.alikuwa NBC Iringa kama accountant,then akawa lecturer pale chuo cha NBC cha Amon Nsekela Iringa after that alihamishiwa hapa DAR na kisha kushika nyadhifa mbalimbali mpaka kuwa Director.na baada ya hapo alienda BOT na baadae kujiunga na shughuli za siasa ambapo kwa sasa ni mbunge wa kalenga.nimesoma na watt wake pale IR na mkewe (mama Flora) ni mwanamke mwenye roho nzuri sana na kwa ujumla ni familia yenye maadili,wachapa kazi na ni mfano wa kuigwa.ni majiran pia so nawafahamu vizuri.ameandika publications nyingi tu kiumjumla anatufaa na tutegemee mabadiliko mengi ikiwa ni pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei.Kila la heri Dk.william Mgimwa

Mimi cna haja ya kujua cv yake lkn kwa hii bajeti ameonyesha ameshindwa kupunguza makali ya ugumu wa maisha kila kitu kimepanda juu kodi juu hata kwa cm je huo mpango wa wananchi wa vijijini kuwa na cm utawezekana?
 
hivi huu u dr aliupatapata vipi au ndio ulea wa kupeana tu,..........katika majopo ya watu mfano huyu alikuwa anajibu maswali sana darasani basi tumuite dr.................
 
Kwa mtazamo wangu ni kwamba tukitaka kuzuia mfumuko wa bei ni lazima serikali ianzishe vyanzo vingi vya mapato ili isitegemee tu kodi kutoka kwa wafanya biashara na mashirika binafsi ambayo ndiyo yanayopandisha bei za bidhaa ili kumudu gharama za uendeshaji pamoja na kodi.Pia tukuze uzalishaji wa bidhaa za ndani ili wafanyabiashara wakose kisingizio cha kupandisha bei eti kwa ajili ya usafirishaji kutoka nje.ISSUED BY ERICK.(UDSM)
 
To go to school is another thing and to be educated is another thing.tanzania wasomi wana elimu na cv za kutisha ila hawana maarifa.ni kama huyo minister.wa finance.ERICK(UDSM)
 
Hey always what you see is what you get and if you want to andstand someone judge what he says.our finance minister is good but something to much care is peformance and his accountability to work to meets international levels bcz he has been given higher duties and responsibilities.dont judge the book by looking its cover.
 
Back
Top Bottom