Ni nani aliyeleta na aliyetengeneza uchawi hapa duniani?

Ni nani aliyeleta na aliyetengeneza uchawi hapa duniani?

Shy land

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
6,245
Reaction score
2,856
wiseboy utafiti na wadau wengine mnaoamini kwamba watu tumeubwa na Mungu naomba mnijuze aliyeumba uchawi ni nani? na mtu wa kwanza kueneza uchawi hapa duniani ni nani?

Kama ni sheteni anahusika katika maswala ya uchawi,! shule za shetani za kufundisha uchawi ziko wapi? kwa nini wachawi wananguvu kubwa kiasi kwamba Mungu ameshidwa kuwaagamiza.?
 
Last edited by a moderator:
Mods kwa heshima ya wanaJF na uongozi wote nisegefurahishwa na tabia yenu yakufuta thread hii, kama munilivyo jana. tupo hapa kwa lengo na kuongeza maarifa na kujifunza zaidi, kufuta thread ambazo hazina dalili yoyote ya uchochezi, dharau au kejeli kwa watu wengine, ni unyanyapaa wa hali ya juu.

BACK TO TOPIC
wiseboy utafiti na watu wengine munaoamini kwamba watu tumeubwa na Mungu naomba munijuze aliyeumba uchawi ni nani? na mtu wa kwanza kueneza uchawi hapa duniani ni nani?

kama ni sheteni anahusika katika maswala ya uchawi,! shule za shetani za kufundisha uchawi ziko wapi? kwa nini wachawi wananguvu kubwa kiasi kwamba Mungu ameshidwa kuwaagamiza.?

kama umeZaLiwa na wazazi anza nao kuwauliza
 
Last edited by a moderator:
Hata ukiambiwa huto amini.

Jina limenitoka ila alianzisha uchawi ni Asili ya mwanaadamu inasemekana ni elimu na kulikuwako na kitabu maalum alikuwa anacho huyo jamaa ila baadae kwa amri ya Mungu akamrisha malaika akakichukue kwa maelezo yawanujua inasemekana ilisahauliwa page moja ya kitabu cha uchawi ktk pirika za kukichukua so page hiyo moja ndo inayofanya kazi uchawi wote unaowona unatendeka duniani unataka kujua zaidi kajiunge na uchawi utajua zaidi
 
Uchawi ni elimu kama zilivo elimu nyingine ambazo watu husoma na kujifunza na elimu zote ni zake mwenyezimungu,amini ya kwamba heri na shari zote zinatoka kwa mungu kama mtihani kwa mwanadamu . mungu akitaka jambo huwa na asipotaka jambo basi haliwi.
Sasa Uchawi kama Uchawi ni elimu ambayo ilishushwa duniani na malaika wawili wakijulikana kama Haruta na Maaruta katika mji wa babel enzi hizo na watu walijifunza kama elimu nyingine ya kawaida kwa matumizi ya kawaida, Sasa binadam wa enzi hizo walienda mbali sana juu ya elimu hiyo na kuanza kumuasi mungu kwa kuitumia elimu hyo vibaya kwa kuwadhuru wengine na hata kufikia hatua ya kumuona mungu si chochote ndipo mungu alipoamuru malaika waende duniani kuchukua nyaraka za elimu hyo ila tayar baadhi ya watu walikua washakua na ujuzi kidogo juu ya elimu hyo na ndo leo hadi Sasa watu wanarithishana.
Kwa hiyo kaka uchawi ni elimu kutoka kwa mungu kama vile biology na chemistry na wala hakuna kiumbe yoyote alienzisha wala kumiliki elimu hii na ndo mana hao wachawi wenyewe wanapata shida sana kumdhuru mtu na wengine hushindwa kabisa na kutulia tulii.
 
Maneno yako muafaka sana ni kweli elimu hiyo ililetwa duniani iwe kama test kwa mwanadamu,na kuongezea zaidi hao wachawi pia hushirikiana na mwalimu wao mkubwa ambaye ndio shaitwaani yule tunayemjua siku zote.Lakini kwa kuongezea tuu,hiyo elimu sisi waafrika tumeshindwa kuitumia vizuri,na kama tungeliweza fanya hivyo basi naamini leo hii dunia ingetuheshimu sana kwa jinsi tungelikuwa na uwezo wa kutatua matatizo mengi yanayoikumba hii dunia ya sasa.Kwa mfano uganga ambao huwa unashabihiana na uchawi siku zote labda leo hii ungechanganywa pamoja na uchawi waafrica tungeweza solve problems nyingi za kiafya hapa duniani.Huku maulaya tungekuwa tunaingia bila kutumia usafiri wa anga tungekuwa na uwezo wa kufika kwao through kusafiri kwa ungo na hata immigration prwa moderators,yaani ocess tusingekuwa tunapitia lakini kwa ubinafsi wetu sisi waafrika tumeshindwa kuufanya uchawi kuwa ni alimu ambayo inayoweza ikafundishwa darasani kama vile wakati unapofundisha physics au masomo mengine,hili lingelikuwa nalo liwe somo maalum Africa.Nimesoma malalamiko ya mtoa hii thread ya kufutiwa topic zake hata mimi ninamuunga mkono kwa hilo maana watu ka mimi tumegeuzwa weeping boy wa hawa sijui wanaojiita moderators,wanachagua baadhi ya watu humu na kuwafanyia ushenzi wa ,mara huruhusiwi changia kitu au mara nyingine topic kupotezwa bila hata ya notification yeyote ile.Mimi hapa nimeamuaga kupageuza sehemu ya kupita tuu na in fact i am no longer very serious like before with this forum na ninawashangaa sana sijui ni kwa nini paranoia imewaingia hawa moderators kwa baadhi ya watu humu,hapa tupo kila mtu kutoa mawazo na mchango wake kwa lugha ya wageni wanasema frredom of expression but inavyoonekana wanajaribu kutaka tufikiri jinsi wanavyofikiria wao,tamati.Mr Murage Msherwampamba.
 
kama umeZaLiwa na wazazi anza nao kuwauliza

Hata wazazi wangu hawajui nishawi kuwauliza hawakunijibu chochote, labda kama wazazi wako wanajua nipe mawasiliano yao niwaulize ili wanieleweshe vizuri.
 
WAKUU
devcon, Sirdirashy NA MSHERWAMPAMBA
Mawazo yenu yote yanafanana kwamba uchawi uliletwa na MUNGU kupitia malaika wake Haruta na Maaruta katika mji wa bebali kwa maelezo ya devcon.
munasema watu walijifunza uchawi na hadi watu wengine wakaaza kudhuru watu na kumkejeli Mungu na kujiona wao kama wanaweza, jambo ambalo lilimfanya Mungu atume tena malaika waichukue ile elimu.

mkuu devcon umesema maswala yote ya heri na shari huletwa na Mungu,!

1,wakati huo tunaabiwa Mungu anaupendo mkubwa kwa sisi wanadam, je? lengo lake kuu ilikuwa ni nini? kuuleta uchawi hapa dunian?

2, unaweza ukanifafanulia zaidi malaika wakoje? je? wanategenezwa au wanazaliwa, hadi wawe wanatumwa na mungu kuleta uchawi duniani?

3,je? wakati huo elimu ya uchawi mungu anaileta mtu wa kwanza kupewa jukumu la kuwafundisha wazake alikuwa anaitwa nani?
 
Kaka@bush land nashukuru sana kwa maswali yako mazuri nami naomba nikujibu kama ifutavyo
1)lengo la mungu kuleta uchawi hapa duniani kwanza ni mtihani kwa mwanadamu pia lilikua ni kuwapa wanadamu elimu juu ya binadam na mazingira yake na kuweza kupata utambuzi wa mambo mbalimbali, kwa mfano ukichukua mafuta ya mzaituni ukijipaka kila sehem yenye tundu kila unapolala basi shetani au majini wabaya hawawezi kukuingia kwani ndo njia zao hizo, lakini wanadamu wa Zama hizo waliitumia elimu hii vibaya kwa kuwadhuru binadam wenzie,ndo mana mungu kwa kua ana upendo akaghadhibika na kuamuru elimu ile irejee kwake lkn tayar watu walikua washapata ujuzi kidogo ndo huu unaotusumbua hadi leo.
2) malaika ni viumbe kama viumbe wengine ila tofauti yao wao wameumbwa kwa moto ni sisi ni kwa udongo, pia malaika hawazaliwi wala kutengenezwa kama magari wao waliumbwa kwa neo kua na wakawa. Malaika ndio watumishi wakuu wa mungu na wana kazi mbalimbali si kuleta uchawi pekee bali hata kuleta mvua, wahai,(maono), kuchukua nafsi yako, kuandika matendo yako mabaya na mazuri ya kila siku n.k, malaika wapo wa aina nyingi kulingana na idara zao.
3) uchawi uliletwa dunia na malaika wawili Haruta na Maaruta katika mji wa babel ambayo ndo Iraq ya sasa, kwa hyo watu wa kwanza kujifunza elimu hii ni watu wa mji wa babel.nafikiri nimekujibu kaka
 
Last edited by a moderator:
Nikiongezea hapo juu lengo la kuleta uchawi ili tupimwe sababu kama kuna pepo na moto hivyo vitu tutavifikiaje bila mtihani? sasa kuna watu wanajaribiwa na wachawi kisha wanamsahau mungu na kuingia katika upotovu mkubwa.
 
devcon swali la tatu hujanijibu, kwamba mtu ambaye alipewa uwezo na malaika wa kuwafundisha wezeke uchawi ni nani?? kama unawajua wanafunzi wakanza kujifunza uchawi itakuwa vyema zaidi kama ukiwataja.. thanks.
 
Huyu mungu wenye upendo na maarifa mengi kwa nini? aumbe kiumbe tena aanze kukipima? wakati uwezo wa kuumba kiumbe ambacho hakifanyi maovu kama anavyotaka inawezekana? Huyu mungu yupo? kweli. wiseboy saidia kujibu hili swali.
 
Last edited by a moderator:
wiseboy utafiti na wadau wengine mnaoamini kwamba watu tumeubwa na Mungu naomba mnijuze aliyeumba uchawi ni nani? na mtu wa kwanza kueneza uchawi hapa duniani ni nani?

Kama ni sheteni anahusika katika maswala ya uchawi,! shule za shetani za kufundisha uchawi ziko wapi? kwa nini wachawi wananguvu kubwa kiasi kwamba Mungu ameshidwa kuwaagamiza.?
Majîbu ya maswali yako yanapatkana sumbawanga. Nenda kawaulize akina pinda.
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na yote mimi ningependelea somo la uchawi lianzishwe Afrika na watoto wote wafundishwe namna ya kuutumia na namna ya kutibu,na pia kufanya inventions za kisayansi kwa kutumia uchawi.Kumbukeni kule kisiwa cha Haiti wenzetu waliupata uhuru wao toka kwa mfaransa through uchawi(vodoo)inavyosemekana wale watu wa kule asili yao ni nchi ya Togo ambako ndiko mahali kwenye strong vodoo barani Africa,tena kule nasikia hirizi zina uhai,zinatoa pumzi kama vile ni kiumbe fulani hivi wenyewe wafaransa waliachia ngazi kwa jinsi uchawi wa mtu mweusi ulivyokuwa mbaya na mkali sana,uhuru ulipatikana kiulaini sana kule.Pia hata hawa wakikuyu wa Mau Mau nawao nasikia walikuwanavyo vitu vikali sana,ambavyo viliwasaidia kuwapa mori wa kupigana na pia kule usukumani kuna mnyama ka Fisi ambaye hutumiwa kiuchawi kama vehicle,huyo fisi anakimbia utafikiria yeye ni jet fighter,halafu pia kule kuna watu waliochukuliwa ki mazingara wanaoitwa mintunge,hawa kazi yao kubwa ni kulimishwa na kufanya uvuvi wa samaki ingawaje ni haramu ktk dini zote lakini economicaly wangeweza kuisaidia nchi yetu kwa namna moja au nyingine.Mr Murage Msherwampamba.
 
Hata ukiambiwa huto amini.

Jina limenitoka ila alianzisha uchawi ni Asili ya mwanaadamu inasemekana ni elimu na kulikuwako na kitabu maalum alikuwa anacho huyo jamaa ila baadae kwa amri ya Mungu akamrisha malaika akakichukue kwa maelezo yawanujua inasemekana ilisahauliwa page moja ya kitabu cha uchawi ktk pirika za kukichukua so page hiyo moja ndo inayofanya kazi uchawi wote unaowona unatendeka duniani unataka kujua zaidi kajiunge na uchawi utajua zaidi

Wenzetu wanamuita nabii kisisina
 
Nikiongezea hapo juu lengo la kuleta uchawi ili tupimwe sababu kama kuna pepo na moto hivyo vitu tutavifikiaje bila mtihani? sasa kuna watu wanajaribiwa na wachawi kisha wanamsahau mungu na kuingia katika upotovu mkubwa.

Swadaqta
 
devcon swali la tatu hujanijibu, kwamba mtu ambaye alipewa uwezo na malaika wa kuwafundisha wezeke uchawi ni nani?? kama unawajua wanafunzi wakanza kujifunza uchawi itakuwa vyema zaidi kama ukiwataja.. thanks.

Kaka naona umeamua kunibana zaidi,kiukweli jina halisi la mtu huyu unaemtaka wewe silifahamu ila historia ya uchawi ndo iko hvo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom