Kama kuna kitu kina makengeza mengi ni hili la mzee wetu Mangula aliyepata ugonjwa wa ghafla akiwa kwenye majukumu yake na kukimbizwa hospital ya Taifa Muhimbili.
Wananchi hatukujua kabla kama kuna la ziada nyuma ya pazia kuhusiana na huu ugonjwa mpaka police walipotoa ripoti matokeo ya uchunguzi wa vipimo vya mzee Mangula kwamba vipimo majibu yanaonesha alilishwa sumu kwenye chakula
Mkanganyiko ni hapa police wanapotoa hii taarifa mara tu baada ya majibu kutoka. Maswali yamekuwa mengi na wengi wanaona kama utaratibu umekiukwa ama huu ni utaratibu mpya
Kumbe kulikuwa tayari na hofu ya mchezo mchafu kwenye huo ugonjwa? Kwahiyo sample Hazikwenda kwa madaktari wa kawaida bali kwa mkemia mkuu na majibu wakapewa police na si daktari wake?
Ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari wake mpaka pale atakaporuhusu vinginevyo.. Je kwenye hili Mzee Mangula karidhia litangazwe hadharani? Na vipi kuhusu daktari wake.
Je, kuna kesi yoyote imeshafunguliwa mahakamani na mlalamikaji ni nani!? Washukiwa ni nani?
Polisi imeshachimba bit kuwa itawatafuta wahusika 'walioweka sumu ' kwenye chakula, nje na ndani ya chama, nje na ndani ya nchi? Mbona kama ni mkwara wa haraka mno?
Kama sumu husika ilimpataa kupitia chakula
Je, ni nani siku hiyo alipewa tenda ya chakula?
Je, ni nani siku hiyo alimsavia mzee Mangula chakula?
Je, ni sumu ya aina gani mzee Mangula aliwekewa?
Hivi kwani haiwezekani ikawa pengine ni nzi wa kijani yule wa chooni ilitokea akapita kwenye chakula cha mzee Mangula na kuacha uchafu wake hapo uliomuathiri mzee?
Kuna mkanganyiko mkubwa sana kwenye hili kama sio propaganda kwakuwa taarifa ya police inazua maswali mengi kuliko majibu.
Hebu tuchukulie katika hali ya kawaida kabisa kwamba mzee Mangula alikuwa na maadui na wakaona njia bora ya kummaliza nia kupitia sumu kwenye chakula na sio njia nyingine yoyote.
Je, ni uaduli juu ya nini? Ama kama ni chuki ni juu ya nini?
Je, ni kisasi?
Je, ni roho mbaya?
Je, mzee anajua nini ambacho wahusika/mhusika hawakutaka aendelee kukijua?
Je, Mzee hajui nini ambacho wahusika/ mhusika hawakutaka akijue?
Je, kwa kutumia sumu kwenye chakula mhusika/wahusika hawakuona hatari ya kujulikana haraka kama
mzee Mangula angeathiriwa na sumu kiasi cha kupoteza uhai na hatimaye mwili wake kufanyiwa post mortem?
Kwa kumbukumbu za nyuma Kolimba na Chachange wote marehemu hawa. Inasemwa walimalizwa kupitia sumu kwenye chakula maji... Kwanini huyu kitumike chakula?
Kuna risk kubwa kwenye kutumia chakula kama silaha ya sumu kwakuwa inahusisha watu wengi na mmoja anaweza kuharibikiwa biashara yake hasa kama chakula husika kililishwa kwa tenda..
Tunachezwa shere hapa na polisi ndio wanatuchanganya zaidi kuhusiana na hili lakini pia kuna wale vijana waliokuwa wanatabiri kuhusu kutokea tukio kunwaa je ni hili lililofeli ama kuna lingine?
Jr[emoji769]