Ni nani alitaka kumuua Mzee Mangula? Kwanini?

Ni nani alitaka kumuua Mzee Mangula? Kwanini?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,755
Reaction score
861,171
Kama kuna kitu kina makengeza mengi ni hili la mzee wetu Mangula aliyepata ugonjwa wa ghafla akiwa kwenye majukumu yake na kukimbizwa hospital ya Taifa Muhimbili.

Wananchi hatukujua kabla kama kuna la ziada nyuma ya pazia kuhusiana na huu ugonjwa mpaka police walipotoa ripoti matokeo ya uchunguzi wa vipimo vya mzee Mangula kwamba vipimo majibu yanaonesha alilishwa sumu kwenye chakula

Mkanganyiko ni hapa police wanapotoa hii taarifa mara tu baada ya majibu kutoka. Maswali yamekuwa mengi na wengi wanaona kama utaratibu umekiukwa ama huu ni utaratibu mpya

Kumbe kulikuwa tayari na hofu ya mchezo mchafu kwenye huo ugonjwa? Kwahiyo sample Hazikwenda kwa madaktari wa kawaida bali kwa mkemia mkuu na majibu wakapewa police na si daktari wake?

Ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari wake mpaka pale atakaporuhusu vinginevyo.. Je kwenye hili Mzee Mangula karidhia litangazwe hadharani? Na vipi kuhusu daktari wake.

Je, kuna kesi yoyote imeshafunguliwa mahakamani na mlalamikaji ni nani!? Washukiwa ni nani?

Polisi imeshachimba bit kuwa itawatafuta wahusika 'walioweka sumu ' kwenye chakula, nje na ndani ya chama, nje na ndani ya nchi? Mbona kama ni mkwara wa haraka mno?

Kama sumu husika ilimpataa kupitia chakula
Je, ni nani siku hiyo alipewa tenda ya chakula?
Je, ni nani siku hiyo alimsavia mzee Mangula chakula?
Je, ni sumu ya aina gani mzee Mangula aliwekewa?

Hivi kwani haiwezekani ikawa pengine ni nzi wa kijani yule wa chooni ilitokea akapita kwenye chakula cha mzee Mangula na kuacha uchafu wake hapo uliomuathiri mzee?

Kuna mkanganyiko mkubwa sana kwenye hili kama sio propaganda kwakuwa taarifa ya police inazua maswali mengi kuliko majibu.

Hebu tuchukulie katika hali ya kawaida kabisa kwamba mzee Mangula alikuwa na maadui na wakaona njia bora ya kummaliza nia kupitia sumu kwenye chakula na sio njia nyingine yoyote.

Je, ni uadui juu ya nini? Ama kama ni chuki ni juu ya nini?
Je, ni kisasi?
Je, ni roho mbaya?
Je, mzee anajua nini ambacho wahusika/mhusika hawakutaka aendelee kukijua?
Je, Mzee hajui nini ambacho wahusika/ mhusika hawakutaka akijue?
Je, kwa kutumia sumu kwenye chakula mhusika/wahusika hawakuona hatari ya kujulikana haraka kama
mzee Mangula angeathiriwa na sumu kiasi cha kupoteza uhai na hatimaye mwili wake kufanyiwa post mortem?

Kwa kumbukumbu za nyuma Kolimba na Chachange wote marehemu hawa. Inasemwa walimalizwa kupitia sumu kwenye chakula maji... Kwanini huyu kitumike chakula?

Kuna risk kubwa kwenye kutumia chakula kama silaha ya sumu kwakuwa inahusisha watu wengi na mmoja anaweza kuharibikiwa biashara yake hasa kama chakula husika kililishwa kwa tenda..

Tunachezwa shere hapa na polisi ndio wanatuchanganya zaidi kuhusiana na hili lakini pia kuna wale vijana waliokuwa wanatabiri kuhusu kutokea tukio kubwaa je ni hili lililofeli ama kuna lingine?

Jr[emoji769]
 
Kwa nafasi ya Mangula ni rais kuwa na maadui kumbuka adui sio lazima uwe naye na ugomvi wa moja kwa moja wengine wanaweza kuwa maadui kutokana na kutofautiana au kuathiriwa na maamuzi yake kama kiongozi wa juu wa ccm lakini polisi wamekosea kukimbilia kutoa taarifa kwani wanawapa mwanya waliofanya hicho kitendo wakimbie au kuharibu ushahidi walichotakiwa ni kufanya uchunguzi kimyakimya na kuwatia hatiani wahusika
 
Hivi kwani haiwezekani ikawa pengine ni nzi wa kijani yule wa chooni ilitokea akapita kwenye chakula cha mzee Mangula na kuacha uchafu wake hapo uliomuathiri mzee?

Jibu lipo hapa👆👆👆👆👆 na nzi wa kijani tunawajua wanapatikana choo cha Lumumba.
 
Sheria inadai sample zitakazothibitishwa na mkemia Mkuu ndizo zitakuwa ushahidi mahakamani, kwa sasa kinachoelezwa ni tuhuma na si ushahidi maana kinachelezwa ni upelelez WA vyombo vya ulinzi na si uchunguz WA madaktar

Shaur kuanzishwa inawezekana kwa kuwa ni kiongoz WA kitaifa WA chama na inawezekana chama chake au familia kuomba polisi kufuatilia jambo kwa kina.

Kijasusi, hilo ni shambulio bovu na hawawez kutumia kamwe.

Aina ya sumu, sumu za kijasusi haziko hivyo na mpaka kutoka Lumumba hadi muhimbil baada ya kufaint angekufa.
Hakika unaona aina ya sumu ni sumu ya wadudu au wanyama wengine ambao utendaj WA binadamu ni tofaut na wao ndio maana kapona.

Maadui
Labda aliyeripoti anaweza kuwa na majibu mazur

Taarifa ya polisi
Ni nyepesi sana kutoa hizo shutuma, na sijui weledi WA jeshi uko wapi kutangaza kitu ambacho hakina ushahid hats chembe na kuzua taharuki wakat unaendelea kupeleleza.
Hao wote uliowataja juu, wanaweza sasa kuficha aina yoyote ya kitilia shaka lkn ndio utambue kwa taarifa ya polis inawezekana ni kutekeleza lengo LA kisiasa kutengeneza scandal kwa MTU ambaye ni tishio kwa chama .

Hifadhi hili kichwan labda liende kama wanavyotaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji123][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ikishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na Taasisi mbalimbali imebaini kwamba ndani ya mwili wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mzee Mangula kulipatikana na sumu,uchunguzi kuhusu tuhuma ya sumu hiyo ilivyoingia mwilini upelelezi bado unaendelea.

Ikumbukwe wiki iliyopita, Mzee Mangula akiwa kwenye majukumu yake alianguka ghafla na kukimbizwa hospitali ambapo alilazwa kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU)

Pia soma > Dar: Philip Mangula aanguka gafla, alazwa ICU. Rais Magufuli amjulia hali

Jr[emoji769]
 
Bad things comes in small packages and are effective in miniscule amounts. Nahisi ni huyo nzi wa kijani! Tusimdharau kabisa.

Daktari angetuambia kwanza kwanini na lini walichukua uamuzi wa kwenda kwenye toxicology. Manake kwa uzee ule kuna mengi. Waliona nini,was it massive tissue necrosis?Circulatory failure? Mzee alipopokelewa alikuwa anaongea? Walishtuliwa? Na nani,wakati gani? Mzee alihisi mzee mchezo mchafu au kuna aliyeasi akatoboa siri mzee apone?

Vipimo gani vingine walifanya?
 
Back
Top Bottom