Ni nani alimuua Sophie..!?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398

SOPHIE-TOSCAN-DU-PLANTIER.jpg
sophie.jpg
sophie-toscan-plantier-ian_4wpfp_2020qs.jpg
Sophie Toscan Du Plantier
392909-sophie-toscan-du-plantier-ici-avec-son-637x0-2.jpg
Sophie Toscan Du Plantier Siku ya harusi yake na mumewe
toscan-enfin-sur-les-ecrans.jpg
Sophie Toscan Du Plantier akiwa na mumewe
sophie_toscan_du_plantier_reference.jpg

Ian-Bailey-is-wanted-in-F-007.jpg
Mtuhumiwa Ian Bailey

Ian-Bailey.jpg
00059e45-640.jpg
Bailey akiwa na mpenzi wake Jules Thomas
200806281133_zoom.jpg
Mazishi ya Sophie Toscan Du Plantier


Hii nayo ni miongoni mwa kesi ambazo mpaka leo haijapatiwa ufumbuzi kutokana na kugubikwa na utata mkubwa.

Ilikuwa ni saa nne kamili asubuhi ya Desemba 23, 1996, katika mji wa Dunmore uliopo katika pwani ya kusini magharibi mwa mji wa Dublin nchini Ireland mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Sophie Toscan Du Plantier, mwili wake ulikutwa na majirani zake ukiwa umelala pembeni ya barabara jirani na nyumbani kwake akiwa amefariki huku akiwa amevaa vazi la jioni na viatu vikubwa vya ngozi ambavyo vilikuwa vimefungwa barabara kama vile alikuwa akitembea kwenda mwendo mrefu. Mwili wake ulikuwa una jeraha kubwa kichwani kuonyesha kwamba ameuwawa.

Polisi wa nchini Ireland maarufu kwa jina la The Garda walifika kwenye eneo la tukio muda mfupi baadae na kufanya uchunguzi wa awali kabla ya kuhamia nyumbani kwake na kuendelea na uchunguzi zaidi. Walipofika katika nyumba yake walikuta mlango ukiwa wazi na taa zote za ndani zikiwa zinawaka, walipoingia ndani walikuta viti viwili vikiwa vimewekwa kwa karibu jirani na sehemu maalum ya kukokea moto kwa ajili ya kupunguza joto ndani ya nyumba katika kipindi cha majira ya baridi. Pia zilikutwa glasi mbili za mvinyo zilizotumika zikiwa zimewekwa kwenye beseni la kunawia mikono.

Polisi wale wakiendelea na uchunguzi wao. Waliingia chumbani kwake na kukuta kitanda chake kikiwa kimevurugika kama vile kulikuwa na mtu aliyelala muda mfupi uliopita au kilikuwa hakijatandikwa tangu siku iliyopita, hata hivyo kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha kwamba tendo la kujamiiana lilitendeka katika kitanda kile. Awali wataalam wa uchunguzi wa eneo la tukio walidhani kwamba wana mahali pa kuanzia baada ya kukuta nywele zilizonyofolewa zikiwa katika mkono wa Sophie lakini baadae wataalam wa uchunguzi wa viasili (DNA) walikuja kugundua kwamba zile nywele zilikuwa ni za Sophie mwenyewe.

Ingawa mwanamke huyu alikuwa ni raia wa Ufaransa, ambapo alikuwa ni muandaaji na mtayarishaji wa vipindi vya Luninga nchini humo, lakini pia alikuwa na makazi yake na mumewe Daniel Toscan Du Plantier nchini Ireland. Na alikuwa na Kawaida ya kwenda nchini Ireland mara kwa mara wakati mwingine akifuatana na mwanae aliyekuwa na umri wa miaka 15 aitwae Pierre, aliyemzaa kwenye ndoa yake ya awali. Safari hii mauti yalipomkuta alikwenda nchini humo akiwa peke yake.

Alikuwa ni maarufu katika eneo hilo, ambapo alikuwa na nyumba yake mwenyewe na alikuwa na marafiki wengi sana wengi wakiwa ni majirani zake. Zoezi zima la uchunguzi wa mwili wa Sophie lilianza na bahati mbaya, kwani ilichukuwa masaa 24 daktari bingwa wa uchunguzi wa maiti Dr. John Habirson kufika kwenye eneo la tukio, pamoja na kwamba walijulishwa mapema kuhusiana na tukio lile. Hivyo kwa muda wote ule mwili wa Sophie ulikuwa umelala pale kwenye eneo la tukio kwa masaa yote 24 huku ukiwa umefunikwa na shuka ya plastic.

Kutokana uchelewaji huo ilikuwa ni vigumu kwa mtaalam yule kumaizi kwa usahihi muda hasa Sophie alipofariki. Hata hivyo baada ya mwili ule kufanyiwa vipimo zaidi na wataalam tofauti tofauti katika Hospitali ya Bandon General ndipo hatimae Dr. Harbison akaja na majibu. Kwa kifupi Dr. Habirson aliwaeleza Polisi kwamba kabla ya kuuwawa Sophie alishambuliwa kwa mapigo kadhaa kichwani na kitu kizito mfano wa nyundo kisha akauwawa kwa kuangushiwa kitu kingine kizito kichwani mfano wa tofali la zege. Hata hivyo Daktari huyo alibainisha kwamba mwili wa Sophie haukukutwa na dalili zozote zinazoonyesha kuwa alishiriki tendo la ndoa kabla ya kuuwawa au kunyanyaswa kijinsia.

Kwa kuanzia Polisi wa upelelezi walianza kwa kuchunguza nyendo za Sophie tangu alipoingia nchini Ireland. Taarifa za kiuchunguzi zilionyesha kwamba mnamo Desemba 20, 1996 Sophie alisafiri kwa ndege akitokea katika Jiji la Paris na kuelekea katika Jiji la Cork lililoko Magharibi mwa Ireland hiyo ikiwa ni takriban masaa 48 kabla hajauwawa. Katika mkanda wa Video unaorekodi matukio ya kila siku katika uwanja wa ndege wa Cork kwa sababu za kiusalama ulimuonyesha Sophie akikodi gari na kuondoka nalo huku akiendesha mwenyewe, ambapo aliendesha kwa umbali wa kilomita 112 hadi kwenye nyumba yake ambayo iko katika ukanda wa pwani ya Dunmore Bay, eneo ambalo husifika kwa kukaa watu maarufu wengi wakiwa ni wahamiaji kutoka nchi za Ulaya na Marekani, Eneo hilo husifika sana kwa kuwa na usalama wa hali ya juu.

Hata hivyo ilikuja kubainika kwamba kabla hajafika nyumbani kwake Sophie alisimama njiani katika eneo liitwalo Ballydehob na kununua kuni za kuotea moto nyumbani kwake kisha akaelekea katika mji mdogo wa Schull ambapo aliingia katika klabu moja na kujipatia kinywaji baridi. Alipotoka hapo ndipo akaelekea nyumbani kwake moja kwa moja. Siku iliyofuata Sophie alionekana tena kwenye mji wa Schull akitoa pesa kwenye Mashine ya kutolea fedha maarufu kama ATM.

Siku nyingine iliyofuata yaani Desemba 22,1996, Sophie aliondoka nyumbani kwake tena na kuendesha gari lake alilokodi umbali wa kilomita 25, ambapo alitembea kando kando ya bahari hadi kwenye ngema ya baharini (Cliff). Baadae aliwatembelea marafiki zake mtu na mkewe waliojulikana kwa majina ya Yvonne na Tom Ungerer, ambapo walikubaliana kwamba angejumuika nao katika kusherehekea Christmas. Wakati anarejea nyumbani Sophie alipitia kwenye Klabu moja iitwayo O'Sullivan iliyoko katika eneo la Crookhaven ambapo alimwambia mmiliki wa klabu aitwae Angela O'Sullivan kwamba atasafiri kwenda nchini Ufaransa katika mji wa Toulouse siku ya Christmas ili kuungana na mumewe kusherehekea Christmas.

Hakukaa muda mrefu katika Klabu hiyo, aliondoka na kurejea nyumbani kwake. Kwa mujibu wa taarifa zilizochukuliwa kutoka kwenye simu yake ya nyumbani ilionyesha kwamba jioni hiyo alimpigia simu rafiki yake mmoja aishie nchini ufaransa pamoja na mtumishi na mwangalizi wa nyumba yake pale nchini Ireland aitwae Josie Hellen ambapo ilionyesha kwamba alimpigia simu mara mbili. Kisha baadae kabla ya saa tano usiku alimpigia mumewe aliyekuwa nchini Ufaransa katika mji wa Toulouse kwa mapumziko ya Christmas. Baada ya hapo hakuwasiliana na mtu yeyote mpaka alipokutwa amefariki siku iliyofuata.

Mpaka kufikia hapo Polisi bado walikuwa hawajapata ushahidi wowote wa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa mauaji yale. Hivyo kutokana kukosekana kwa ushahidi wa kutosha ilibidi polisi waanze kuchunguza maisha binafsi ya Sophie nchini Ufaransa. Kwani walikuwa na wasiwasi kwamba huenda muuaji alikuwa akimfuata Sophie tokea Paris nchini Ufaransa mpaka nchini Ireland kwa dhumuni la kumuuwa. Mwanzoni mwa uchunguzi wao Polisi walikuja kugundua kwamba yapo maswali mengi sana kuhusiana na mahusiano yake na mumewe ambayo yalikuwa hayana majibu yanayojitosheleza.

Sophie mwanamke mrembo aliyekuwa na sura na umbo la kuvutia, aliolewa na Daniel Toscan Du Plantier mtengenezaji filamu maarufu nchini Ufaransa aliyewahi kuwa Rais wa Chuo cha watengeneza Filamu nchini Ufaransa miaka mitano iliyopita. Mwanae Pierre aliyekuwa na umri wa miaka 15 wakati huo ni mtoto aliyemzaa kutoka kwenye ndoa yake ya awali. Daniel alikuwa akimzidi mkewe kwa takriban miaka 20 kwa umri. Mtumishi wake wa ndani nchini Ireland aitwae Josie Hellen akihojiwa na Polisi alikiri kwamba katika mazungumzo yao ya kawaida yeye na Sophie, aliwahi kudokezwa na Sophie kwamba ndoa yake na Daniel imekuwa ikikumbwa na matatizo ya mara kwa mara na kuna wakati aliwahi kumdokezea kwamba kuna uwezekano mkubwa wa yeye Sophie kufikia makubaliano ya kurudiana na baba yake Pierre, mumewe wa zamani waliyetalikiana.

Alipoulizwa kama labda Sophie alikuwa na mpenzi mwingine nchini Ireland, Bi Hellen alikanusha kuhusu Sophie kuwa mpenzi nchini Ireland. Kwa maneno yake mwenyewe Bi Hellen alisema, "Kama angekuwa na mpenzi hapa nchini kwa uhakika ningefahamu kuhusu jambo hilo, tena sio mimi peke yangu bali pia na majirani zake woote waliomzunguka."

Mnamo Januari 13 Askari wa upelelezi wa nchini Ireland walisafiri kutoka nchini Ireland hadi Paris nchini Ufaransa ili kumhoji Daniel Toscan Du Plantier mume wa Sophie, ambapo hakutoa mwanga wowote ambao ungewawezesha Polisi Kumjua muuaji aliyemuuwa mkewe na ni kwa sababu gani. Kutokana na kukosa taarifa zozote muhimu zitakazowawezesha kumkamata muuaji, Askari wale wa upepelezi waliachana na wazo la kuyahusisha mauaji yale na muuaji kutoka nchini Ufaransa. Kutoka nchini ufaransa Askari wa upepelezi walirejea nchini Ireland na kujipanga upya katika upelezi wa kesi hiyo ambayo ilijaa utata mwingi.

Kwa kuanzia Askari wale walianza uchunguzi wao kwa kumchunguza jirani yake na Sophie aliyejulikana kwa jina la Ian Bailey aliyekuwa na umri wa miaka 40 wakati huo. Huyu ni mwandishi wa kujitegemea aliyehamia katika eneo hilo la Pwani ya Cork akitokea nchini Uingereza mwaka 1992, hiyo ikiwa ni miezi michache tangu Sophie anunue nyumba katika eneo hilo. Bailey alikuwa ni mwandishi wa habari wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio muda mchache tu baada ya mwili wa Sophie kuonekana. Baadae Bailey alianza kuripoti habari kuhusu mauaji yale katika magazeti mbalimbali ya pale Ireland na ya nchini Uingereza.

Hiyo haikuwa ni sababu ya kumtilia mashaka Bailey kwani kimsingi alikuwa ni mwandishi wa habari wa kujitegemea ambae alikuwa akiheshimika na baadhi ya vyombo vya habari, na kwa kuwa lile lilikuwa ni tukio kubwa haikuwa ni kosa kuliandika. Kilichowavuta Polisi mpaka kumkamata Bailey ni kutokana na minong'ono iliyokuwa ikisemwa na watu mitaani. Kulikuwa na maneno yaliyosambaa mitaani kwamba siku moja baada ya Mauaji ya Sophie, Bailey alionekana akiwa na Michubuko kwenye mkono wake, na pia yuko mwanamke mmoja alikiri kumuona mtu anaefanana na Bailey akiosha viatu vyake kwenye chemchem ya maji majira ya asubuhi sana siku aliyouwawa Sophie.

Polisi walipomhoji Bailey alikanusha kuhusika na mauaji yale, alipoulizwa kuhusu michubuko aliyonayo katika mkono wake. Alidai kwamba michubuko ile ilitokana na kuumia wakati akikata mti wa Christmas kwa ajili ya kupamba nyumbani kwake. Polisi walipomuuliza mahali alipokuwa usiku wa siku ya mauaji ya Sophia, Bailey alidai kwamba alikuwa nyumbani kwake pamoja na mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Jules Thomas. Mpaka kufikia hapo polisi walikuwa hawajapata ushahidi wa kutosha wa kumtia nguvuni muuaji si kwa Ireland tu bali pia na Ufaransa.

Nao waandishi wa habari kutoka nchini Ufaransa ambao walifurika katika mji wa West Cork nchini Ireland ili kufuatilia upelelezi wa kesi hiyo hawakusita kuishambulia Idara ya uchunguzi wa maiti (State Pathologist) kwa kuwachukuwa masaa 24 kufika kwenye eneo la tukio. Waandishi hao walikitafsiri kitendo hicho kama uzembe wa hali ya juu, na kuituhumu pia idara ya Polisi ya nchini humo kwamba imekosa umakini katika utendaji wake wa kazi.

Mnamo Februari 6, 1996 Daniel Toscan Du Plantier alifungua kesi dhidi ya muuaji wa Sophia katika mahakama kuu ya nchini Ufaransa, ingawa muuaji alikuwa bado hajajulikana.

Akizungumzia swala hili, mwanasheria wa Daniel aliyejulikana kwa jina la Allan Spinneret aliwaambia waandishi wa habari kwamba wamefungua kesi hiyo ili kuwepo na ushirikiano kati ya Polisi wa nchini Ufaransa na wale wa nchini Ireland. Kwa maneno yake mwenyewe mwanasheria huyo alisema, "itakuwa ni utoto kudhani kwamba tunataka kuleta ushindani kati ya idara ya Polisi ya nchini Ireland na hii ya hapa Ufaransa katika swala hili, kwani ni jambo la kawaida pande mbili za Polisi kushirikiana"

Mnamo Februari 10, 1996, katika hali isiyo ya kawaida Polisi wa nchini Ireland walimkamata Ian Bailey pamoja na mchumba wake Jules Thomas ambapo waliwahoji kwa takribani masaa 12 na kuwaachia huru (kwa mujibu wa sheria za Ireland mtuhumiwa hawezi kushikiliwa na Polisi kwa zaidi ya masaa 12 bila kufunguluwa mashtaka)

Bailey aliporejea nyumbani kwake akiwa na mchumba wake alitumia muda huo kuandika makala ndefu kuhusu mahojiano yake na Polisi na kisha kuituma makala hiyo katika gazeti la The Star la nchini uingereza. Siku iliyofuata gazeti hilo lilitoka likiwa na habari hiyo ndefu iliyojaa katika kurasa nne. Baada ya mahojiano hayo msemaji wa Polisi aliyejulikana kwa jina la Noel Smith ambae ndie aliongoza mahojianao hayo aliwaambia waandishi wa habari kwamba faili la mahojianao litapelekwa kwa mwendesha mashtaka wa serikali (DPP) kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

Siku zilipita, miezi ilipita lakini Bailey hakufunguliwa mashtaka na idara ya Polisi nchini Ireland iliendelea kushikwa na kigugumizi juu ya uamuzi wa kesi hiyo. Mpaka kufikia Desemba 1996 ambapo ndio ulikuwa unatimia mwaka mmoja tangu kifo Sophia kitokee lakini bado kesi hiyo ilikuwa haijapatiwa ufumbuzi. Kutokana na kuwa mume wa Sophia Daniel Toscan Du Plantier alikuwa rafiki wa karibu wa rais wa Ufaransa wa wakati huo Jacques Chirac, kuanzia hapo uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ireland na Ufaransa ukaanza kudorora.

Msemaji wa Daniel aliyejulikana kwa jina la Paul Haennig akiongea na waandishi wa habari alisema kwamba Daniel ana uhakika kwamba mkewe aliuwawa na muuaji wa Ireland lakini anashangazwa na namna polisi wa nchini humo wanavyolichukulia swala hilo.

Mpaka sasa bado kuna vuta nikuvute kati ya mamlaka ya ya sheria ya Nchini Ufaransa na ile ya nchini Ireland. Mahakama kuu ya nchini Ufaransa imetaka bailey apelekwe nchini humo ili ashitakiwe kwa kosa la mauaji ya Sophie, lakini bailey amekuwa akikata rufaa katka mahakama kuu ya nchini Irelanda kupinga kupelekwa nchini Ufaransa kushitakiwa kwa kosa hilo. Kwa mara ya mwisho shauri lake la kukata rufaa ya kupinga kwake kurejeshwa nchini Ufaransa lilisikilizwa hapo mnamo Januari 13, 2012, ambapo shauri hilo liliahirishwa tena.
Hata hivyo mnamo Machi 1, 2012, Bailey alishinda katika rufaa yake hiyo kutaka asipelekwe nchini Ufaransa ili kuhojiwa kuhusika na mauaji ya Sophie Toscan Du Plantier.

Akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama kuu ya Dublin, Bailey ambaye ameishitaki serikali ya Ireland kwa kumkamata na kumhusisha na mauaji hayo kimakosa alisema, "Mimi na mpenzi wangu Jules Thomas tumekuwa kama tuko jehanam, haya yalikuwa ni majaribu makubwa kwetu................Na ninaamini kwamba, huu ndio mwisho wa muendelezo wa tamthiliya hii. Bado nina mambo mengi ya kushughulikia kwa kipindi hiki.............."

 
Ni Ijumaa nyingine tena mabibi na mabwana kama kawaida nimekuja na mkasa wa kesi hii ambayo mpaka leo haijapatiwa ufumbuzi........ Kuna mambo mengi ya kujifunza katika kesi hii.
Nawatakia usomaji mwema.......................
 
Very interesting; Ila Jamani kuna majaribu makubwa duniani...Imagine huyo Jamaa (Bailey) angekuwa mbongo...Angesota segerea from 1996 hadi 2012 good years of your life going to waste! huko yenyewe kawekwa kitimoto for 16years! Omba Mungu yasikukute...
 
Kama kawaida mkuu...............unaweza kuipotezea kama hujaipenda....................LOL
Mkuu hakuan magazeti yanayo toka kwako sijayapenda, sema mengine yanakuwa yana ukurrasa marefu sana... mpaa unachoka kabla hujayasoma.
 
Nimekisoma hiki kisa huku nikilinganisha na jinsi polisi wetu wanavyofanya upelelezi wao, hususan jinsi walivyodili na kifo cha Kanumba,, kwa kweli Tanzania intelijensia ipo kwa maslahi ya watawala tu..
 
Very interesting; Ila Jamani kuna majaribu makubwa duniani...Imagine huyo Jamaa (Bailey) angekuwa mbongo...Angesota segerea from 1996 hadi 2012 good years of your life going to waste! huko yenyewe kawekwa kitimoto for 16years! Omba Mungu yasikukute...

Kwa kipindi chote alichokuwa anachunguzwa jamaa alikuwa huru tu akiendelea na shughuli zake kama kawaida................ Kwa wenzetu mtu hawekwi ndani hivi hivi, ni kupoteza nguvu kazi na kuiingiza nchi hasara.
 
Kwa kipindi chote alichokuwa anachunguzwa jamaa alikuwa huru tu akiendelea na shughuli zake kama kawaida................ Kwa wenzetu mtu hawekwi ndani hivi hivi, ni kupoteza nguvu kazi na kuiingiza nchi hasara.

Ukishajua we mtuhumiwa, tena wa mauaji Amani ya moyo inakosekana kabisa yani...Mi imeniboa mtu from no where unakuja kuhusishwa
 
Alifariki 23-12-1996
hii ni 23- 1+2 - (1+6) - (3*3 ) + 3 *3

Mpaka leo kesi inazungushwa n.k illuminti @work with brain concusion. hahah!
 
Ukishajua we mtuhumiwa, tena wa mauaji Amani ya moyo inakosekana kabisa yani...Mi imeniboa mtu from no where unakuja kuhusishwa

Et kwa sababu ya kiherehere chake, kuwa wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio..............................!
 
Alifariki 23-12-1996
hii ni 23- 1+3 - (1+6) - (3*3 ) + 3 *3

Mpaka leo kesi inazungushwa n.k illuminti @work with brain concusion. hahah!
Kweli eh! Unajua hili jambo hadi leo linawaumiza vichwa...........
1-Kwanza kakutwa na nywele kwenye kiganja chake, lakini baada ya uchunguzi zikagundulika kwamba ni nywele zake
2-Pili Nyumbani kwake palikutwa viti viwili karibu na jiko la kuotea moto kipindi cha majira ya baridi na glasi mbili za mvinyo kwenye beseni la kuoshea vyombo...........Je mgeni gani alimtembelea siku hiyo
3-Tatu kitanda chake kilivurugika kama vile mtu alilala na alipoamka hakutandika (Hakukuwa na dalili za tendo la ndoa kufanyika katika kitanda hicho)..........Kumbuka alitoka na vazi la jioni labda kwa matembezi ya jioni ili kunyoosha mwili.....Huenda baada ya kulala mchana ule
4-Nne Hakuwa na mpenzi nchini Ireland, lakini aliwahi kunukuliwa na mfanyakazi wake wa ndani akisema kwamba ndoa yake na Mumewe Daniel Tosca Du Plantier imekuwa ikikumbwa na matatizo ya mara kwa mara na kuna uwezekano wa yeye Sophie kufikia makubaliano ya kurudiana na mumewe wa awali ambaye ndio baba wa mtoto wake pekee.............Lakini pia mumewe Daniel Tosca Du Plantier alipohojiwa na Polisi waliosafiri kutoka Ireland, hakutoa maelezo ambayo yangeweza kuwasaidia kumpata muuaji..................!?
5-pamoja na Polisi wa Ireland kuwahoji mashahidi wapatao 240, lakini wameshindwa kutegua kitendawioli hicho...........Je kunani hapo....................!?
 
Very interesting though, ingekuwa vizuri tungesikia kuna mtu alikamatwa, maana hii ni kama part 1 na hivo tuna hakika utatuletea part 2 mchambuzi
 
mtambuzi hii kesi imeniccmua,nawaza juu ya hatma ya haka katoto(lulu)na serikali ye2 iliyojaa ufisadi mpaka kwenye issue kubwa kama hizi!!kesi ya 96 nikiwa std2 til nw...daa it means na ya kanumba itakua hivi maana imejaa utata.wanaweza wakawa wanakashikiria kabinti kawa2 buree kumbe muhucka yupo kitaa kwa raha zake....
 
Hili la bailey kuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kukutwa na michubuko...ata kama ni mwandihi...inanipa maswali mengi na inanikumbusha utata fulani..anyway ipo siku ukweli utapatikana.
 
Back
Top Bottom