Ni muda muafaka wa kuliokoa Taifa

kacnia

JF-Expert Member
Sep 16, 2014
3,893
15,247
Salaam watanzania wenzangu.

Dunia imekumbwa na janga kubwa (uviko19) na kila tabaka limepigwa na butwaa lisijue cha kufanya. Baada ya tafakari ya miezi kadhaa, hatimaye suluhisho maridhawa juu ya janga hili limepatikana.

Kutokana na maelezo ya wataalamu juu ya ulazima wa kuendelea kujikinga na uthibitisho kuwa hata baada ya kuchomwa chanjo ya corona bado muhusika atapata maambukizi, ni wakati sahihi wa taifa kufanya maamuzi yafuatayo(kwa nia njema)

Ni hivi-
Kwanza iandaliwe orodha ya majina ya watanzania ambao wamekwisha kuchoma chanjo ya covid19 na iwekwe hadharani kwa ajili ya ufuatiliaji wa matokeo ya chanjo walizo choma.

Pili, wananchi waliobaki wote (ambao hawajachoma chanjo hizo) pia watambulike na afya zao zifuatiliwe kwa ukaribu.

Baada ya muda (hata miaka miwili) itolewe takwimu iliyojikita katika utafiti yakinifu juu ya idadi ya vifo vilivyotokana na ugonjwa huu kutoka kundi namba moja (waliochoma chanjo) na kundi namba mbili (ambao hawajachoma), majibu yatakayopatikana hapo yatatuleta pamoja kama taifa na kufikia uamuzi sahihi wa nini kifanyike, kuliko hivi sasa maswali ni mengi kuliko majibu.

Wasiwasi: walioleta hiki kirusi hawakujipanga katika suala zima la kukihalalisha duniani, jambo linalopelekea muitikio hasi dhidi ya upambanaji wake.

Tanzania ni nchi ya ahadi, watanzania tunasifika kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa akili (kama hauna ni wewe), basi katika hili tusizikalie akili zetu

Nawasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom