Ni mnyama gani huyu?

Ni mnyama gani huyu?

Miguu na masikio kama sungura lakini mkia wake mrefu hawezi kua yeye.
Sitaki kabisa kuamini kua huyo ni mtemi honey badger ameangushwa kizembe na mbwa?
huyo atakuwa kicheche tu mla kuku yule mzee wa kazi bwana asali hapana kuanguka kwa mr dog kabisa. simba mwenyewe anasanda.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Honey bedger anakimbia kama hataki
Anakula chochote anachokutana nacho
Anakula nyoka wote
Nyuki wakimuona wanamkimbia
Anachukua asali Kama kaitengeneza yeye
Akikutana na Kobe anakula mpaka Gamba lake
Ni mnyama anayeongoza kwa kutokua muoga porini
Hawezi kuuawa na mnyama yoyote
Huyo ndio Honey bedger mwenyewe a.k.a nyegere.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapo kwenye kula gamba la kobe umetunywesha chai
 
Huyu mdudu aliwahi kuingia kwenye banda la kuku aliua kuku kama wanne na kuwatia wengine vilema,
Jogoo hakuwa na jeraha lolote lile ila kesho yake nilimkuta bandani amekufa,
kwa hasira niliapa nikimkamata huyu kiumbe namtoboa jicho na kumvunja miguu miwili namuachia aende zake.
Pia majuzi juzi huyu mdudu katembelea banda la Kuku ile kuku kumuona kwa nje walipiga nduru hatari ndio kuamka nikamkurupusha
Ila kuna mdau mmoja aliniambia kuwa ana sumu kali sana kama akikutoa damu unaweza kufa sasa sijui kama ni kweli.
Hao mbwa wako ni hatari sana nimewapenda kalisheshe
 
Mnaosema huyo ni nyegere mna utaniiii..

Thubutuuuuuuuu....
Nyegere a.k.a honey badger umgalagaze kiasi hichoo?
Huyu ni kicheche...
View attachment 1456338
Angekua ni nyegere, Napendaka kumuita
Mr Die harder,
View attachment 1456340
Hio picha ya mtoa mada ingekua ya Maiti ya mbwa,
kama mbwa ni mbabe basi kujitahidi kwake angalau tungeona maiti mbili hapo.
Hata mbwa angekuwa mbabe bado kwa huyu jamaa angwkalishwa tu. Huyu bwana ngozi yake ni ngumu balaa, na ndo kinachomsaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye kula gamba la kobe umetunywesha chai
Inaweza kuwa kweli mdau huyu niliwahi kuona Makala moja ikimzungumzia Maisha yake asee nishida hata ukikutana naye inabidi umpishe mbali kabisa ni the most fearless animal.
 
Inaweza kuwa kweli mdau huyu niliwahi kuona Makala moja ikimzungumzia Maisha yake asee nishida hata ukikutana naye inabidi umpishe mbali kabisa ni the most fearless animal.

Kwenye hiyo makala walimuonyesha akiwa anakula gamba la kombe?
 
Back
Top Bottom