Ni mkosi au ndo biashara ya bodaboda ilivyo?

Cute Cindy

JF-Expert Member
Apr 9, 2019
211
591
Ni mwaka mmoja nimekuwa kwenye hii biashara ya bodaboda, wiki 2 zilizopita baada ya kubadilisha tairi la mbele la toyo, leo bike yangu ya toyo imepiga shoti kwenye wiring.. sasa sijui ni dereva wa bodaboda anakula njama na fundi ili nitoe hela, halafu toyo yenyewe mwezi wa pili mwaka huu ndio imetimiza miaka 3 tu tangu inunuliwe, wiring elf 20 halafu hesabu elfu 30 kwa wiki kuna faida hapo kweli

Narekebisha hili tatizo, ikitokea tatizo lingine nauza bike:mad:sijui wameniloga, coz juzi nilianza kuuza skygo kwa mkataba, nikiuza hizi bike mbili nitabakiwaa na bike 1, sijui ndio kufilisika kunapoanzia..
 
Lazima upate tabu mkuu, hicho unachokifanya ni biashara na sio ujasiriamali, mafanakio hayapatikani katika biashara bali ni katika ujasiriamali.
 
Mi ilinishindaga nikayauza maboksa halafu niliyemuuzia nayeye akanizulumu hela, nikaona aah sio kesi!!
 
Acheni kuwapa madereva kama mitaji yenu midogo.
Ingia barabarani mwenyewe uone kama hio biashara hailipi. Pesa zipo ila mnaibiwa.
Nyie ndo husema uber ,biashara ya duka, kulima nk hazilipi. Hizo biashara zin pesa nyingi ukiifanya mwenyewe.
Endesha hio pikipiki mwenyewe uone kam hutoiona pesa yako
Hakuna kitu kama ichi,ushauri wa namna hii uwa naudharau sana, ati " fanya mwenyewe" biashara yyt ile ukitaka ikue kuajiri watu hakuepukiki. Kikubwa unachopaswa kumwambia ni kwamba ama atafute dereva mwingine au umpe makavu kuwa anafanya biashara na sio ujasiriamali kwaiyo kuteseka ni lazima.
 
Mkuu nimemwambia kama mtaji wake ni mdogo ni bora aifanye mwenyewe kuna dhumuni gani la kuajiri mtu akuuzie duka lako na wewe upo? Hio biashara hatoweza kuifanya kwa ufanisi mkubwa kama utakaoufanya wewe nk.kuajiri watu hakuepukiki biashara ikishakuwa kubwa na wewe mfanya biashara una experience ya kutosha wa mzunguko na output ya biashara nk huyo bodaboda anamuibia kama anabisha aingie mwenyewe barabarani aone
Hakuna kitu kama ichi,ushauri wa namna hii uwa naudharau sana, ati " fanya mwenyewe" biashara yyt ile ukitaka ikue kuajiri watu hakuepukiki. Kikubwa unachopaswa kumwambia ni kwamba ama atafute dereva mwingine au umpe makavu kuwa anafanya biashara na sio ujasiriamali kwaiyo kuteseka ni lazima.
 
Acheni kuwapa madereva kama mitaji yenu midogo.
Ingia barabarani mwenyewe uone kama hio biashara hailipi. Pesa zipo ila mnaibiwa.
Nyie ndo husema uber ,biashara ya duka, kulima nk hazilipi. Hizo biashara zin pesa nyingi ukiifanya mwenyewe.
Endesha hio pikipiki mwenyewe uone kam hutoiona pesa yako

OK sasa hapo kwenye service ya wiring sijaelewa dereva ataniibiaje, wakati gereji tutaenda wote mc gregor
 
Wear and tear... depreciation... decrease in value.. time usage... uchakavu...
WW NI BOSI MASIKINI.. YAAN PIKIPIKI INA MIAKA 3 USHANGAE HAYO MATATIZO..?? system ya waya kujipiga shot ni kawaida inaweza hata kujipiga ingali mpya.. rekebisha chombo chako.. mpe bodaboda ikiwa safi na salama.. utaona pesa na utanufaika.. ss service hufanyi unatakaje..??
Nimekuachia bonge la TUSI....
 
Hakuna kitu kama ichi,ushauri wa namna hii uwa naudharau sana, ati " fanya mwenyewe" biashara yyt ile ukitaka ikue kuajiri watu hakuepukiki. Kikubwa unachopaswa kumwambia ni kwamba ama atafute dereva mwingine au umpe makavu kuwa anafanya biashara na sio ujasiriamali kwaiyo kuteseka ni lazima.
Mkuu upo sahihi.
Biashara yoyote ukitanguliza undugu au urafiki sana huwezi kufanikisha lengo.
Madereva wa bodaboda usiwaonee aibu unawapa makavu live na kingine mkataba ni muhimu.
Hyo biashara ya bodaboda bila mkataba imepitwa/ni ya kizamani.
Dili ni kuandikishiana mkataba akizingua hakuna maongezi mnafuatisha mkataba unasemaje,hakuna kubembelezana.
 
vyombo vya moto ni usimamizi na sikuzote usiogope changamoto ka unahisi kunanjama na fundi tafuta fundi mwingine unae mwamini
 
Ni mwaka mmoja nimekuwa kwenye hii biashara ya bodaboda, wiki 2 zilizopita baada ya kubadilisha tairi LA mbele la toyo, leo bike yangu ya toyo imepiga shoti kwenye wiring..sasa cjui ni dereva wa bodaboda anakula njama na fundi ili nitoe hela, hlf toyo yenyewe mwezi wa pili mwaka huu ndo imetimiza miaka 3 tu tangu inunuliwe, wiring elf 20 hlf hesabu elf 30 kwa wiki kuna faida hapo kweli

Narekebisha ili tatizo, ikitokea tatizo lingine nauza bike:mad:sijui wameniloga, coz juzi nlianza kuuza skygo kwa mkataba, nkiuza hizi bike mbili ntabakiwaa na bike 1, sijui ndo kufilisika kunapoanzia..
pole sana
 
Back
Top Bottom