Biashara ya boda boda

kasambalakk

Senior Member
Apr 2, 2011
126
17
Hongereni kwa kufunga kwa upande wa ndugu zetu waislam na pia kwa ndugu zetu wakristo tunasema tupo pamoja na nyinyi ili mradi tusiweze kuaribu swaumu zenu kwa njia moja au nyingine..

sasa ndugu zangu me nataka kuanza kufanya biashara ya boda boda nitampa kijan awe dereva wangu...tatizo nina idea kwa mbali sana na biashara hii lakni kuna watu nimeongea nao wamesema ni biashara nzuri kama utampata kijan mwaminifu sana..

maswali yangu ni haya:
  1. nataka kujua hesabu ya wiki
  2. njia gani ya kumshawishi kijan huyo kuwa makini kazini kama kumpa bonus na mengineyo
  3. muda gani unafaa kwa boda boda kuuzwa kabla haijachoka sana.
  4. ipi ni boda boda nzuri kwa biashara kwani zipo nyingi kama toyo, t-better nyingine zina kitu cha kuegemea na nyingine hazina kabsa...
  5. bei halisi ya boda boda ikiwa na plate number na insurance( inaweza kuingia barabarani bila kikwazo)
  6. duka lipi ni zuri kwa kununua ambalo lipo cheap(bei rahisi) NB: usijitangazie biashara yako hapo weka kitu halisi
  7. kama nikinunua mtaji wa mafuta naanza kumuwekea wa kiasi gani.
  8. pia napokea ushauri mwingine kama upo kwenye biashara hii ya boda boda
natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu wanajf

==================

Wana JF,

Sikuwahi kudhani hapo nyuma kama bodaboda inaweza kutajirisha mtu kwa kumtengenezea mpaka Tshs 3 millioni kwa mwezi (other factors remain constant) kwa kuanza na bodaboda moja tu!

Imagine umenunua bodaboda MPYA aina ya Boxer (pamoja na gharama zingine kama insurance nk) kwa Tshs 1.7 million.

Kwa hapa Dar, kila siku bodaboda inaingiza Tshs. 10,000 (kama umeajiri dereva akupigie kazi). Hivyo kwa wiki unapata Tshs. 70,000 ambayo kwa mwezi ni Tshs 280,000 Net.

Kwa mapato hayo ya mwezi, itakuchukua takribani miezi 6 kurudisha mtaji wako wote. Hivyo kuna option 2, kuuza bodaboda na kuongeza fedha kidogo ili upate zingine mbili, au kuendelea kubaki nayo kwa miezi mingine 6 ili ununue nyingine na ziwe 3.

Hii maana yake ni kwamba, ndani ya mwaka (if other factors are constant) unaweza kuanza na bodaboda moja na kuufunga mwaka na bodaboda 3!

Unaweza kufanya hesabu ili kupata mapato ya mwezi kwa bodaboda 3. Hivyo kama mambo yataendelea vizuri, kuna uwezekano ndani ya miaka 3 kuwa na boda zaidi ya 10 na kufanya pato la mwezi kuwaTshs 2. 8 millioni.
 
Kulikuwa na thread moja ya biashara ya bajaji, itafute itakusaidia majibu ya swali la pili na 3.
 
kaka nimeshajua bei yake inaanza 1.3 to 1.5 million....

Sawa dada, fanya hivi, nunua piki piki mkabidhi kijana kwa makubaliano kuwa baada ya muda fulani litakuwa la kwake(huo muda uzingatie return ya hiyo biashara). Kwa mfano tuassume baada ya mwaka utamwachia, kama kijana atakuwa anakuletea 20000/day, tuassume atafanya kazi siku 6 katka wiki that means
Per week:120000.
Per month:480000.
Per year: 5,760,000.

Gharama za matengenezo na kila kitu itakuwa juu yake. B'aada ya mwaka piki piki yako itakuwa imezalisha zaidi ya mara 3 ya mtaji.
 
Ndg yangu Kasamalaki, hili wazo lako ninaliunga mkono kwa karibu asilimia zote, kwani utamfanya huyo kijana awajibike.
 
Wakuu habari, nimemnunua bodaboda, katika kutafuta nadereva nimekutana na hii biashara ambayo inaitwa ya mkataba, ntaileleza:-
  1. unampa dereva bodaboda, mnakubaliana akurudishie kiasi fulani baaada ya muda fulani inakuwa bodaboda yake. naomba nisaidiwe yafuatayo:-
  2. Nipate elimu zaidi juu ya hii biashara, faida zake na hasara zake, ni faida kiasi gani ipo accepted kwenye market na payback period ni muda gani
  • Kama kuna mtu aliyefanya hii biashara angenipa sample ya mkataba wenyewe, nijue wapi tunaandikiashiana naye na nanai mediator wa makubaliano yetu
Ni hayo tu wakuu naomba pm au call 0654000253
 
Pamoja na mikataba ufuatiliaji ni muhimu, hao madereva wengi wao ni watu wasiothamini kazi zao na hata chombo chenyewe.
 
Mkuu usikubali kama upo kibiashara. wenzio wanafanya hivi;

Kama umenunua pikipiki mpya huwa haisumbui so muelewane awe anakuletea bei gani kwa wiki. ikishamaliza mwaka ndo mnaingia mkataba. hapo unakuwa na uhakika wa kurudisha hela yako vinginevyo hutapata faida. ni hayo tu. mia
 
Ndugu kuwa makini sana na hao watu wa boda boda,kweli wengi c makini na hualibu chombo makusudi kwa kisingizio cha cost sharing,sas unapompa hakkikisha hakubani ktk garama ya matengenezo,la sivyo hela ya wiki utakua unapata nusu,na uwe mkali sana na kua unakifuatilia sana chombo chako,uclale bila kuiona na unaikagua,ucmpe alale nayo labda kwa mashart mahalum mana wengne wanaeza ipigia kazi 24hrz then wakakupa kihela cha 12 hrz,kulala na boda boda ni mkataba mwngne kbisaaa
 
Wana JF,

Sikuwahi kudhani hapo nyuma kama bodaboda inaweza kutajirisha mtu kwa kumtengenezea mpaka Tshs 3 millioni kwa mwezi (other factors remain constant) kwa kuanza na bodaboda moja tu!

Imagine umenunua bodaboda MPYA aina ya Boxer (pamoja na gharama zingine kama insurance nk) kwa Tshs 1.7 million.

Kwa hapa Dar, kila siku bodaboda inaingiza Tshs. 10,000 (kama umeajiri dereva akupigie kazi). Hivyo kwa wiki unapata Tshs. 70,000 ambayo kwa mwezi ni Tshs 280,000 Net.

Kwa mapato hayo ya mwezi, itakuchukua takribani miezi 6 kurudisha mtaji wako wote. Hivyo kuna option 2, kuuza bodaboda na kuongeza fedha kidogo ili upate zingine mbili, au kuendelea kubaki nayo kwa miezi mingine 6 ili ununue nyingine na ziwe 3.

Hii maana yake ni kwamba, ndani ya mwaka (if other factors are constant) unaweza kuanza na bodaboda moja na kuufunga mwaka na bodaboda 3!

Unaweza kufanya hesabu ili kupata mapato ya mwezi kwa bodaboda 3. Hivyo kama mambo yataendelea vizuri, kuna uwezekano ndani ya miaka 3 kuwa na boda zaidi ya 10 na kufanya pato la mwezi kuwaTshs 2. 8 millioni.
 
Tulishapita huko mkuu na tulipga sana hizo mathematics kabla hatujawakabidhi hawa vijana bodaboda!
Sipendi kukukatisha tamaa ila ukitaka kuwezana nao ingia nae mkataba na umkabidhi hiyo bodaboda kama yake kwa dhamana maalum ndani ya miezi 10 tu daily akuletee Tsh10k. Akifuzu huo mtihani muachie iwe yake. Na ili ufanikishe mambo yako anza na pikipiki3 mpaka5 ili ikitokea mmoja kazingua usiumie sana roho.
All in all ugopa kuletewa kipande utabuluzwa na huyo chalii vibaya sana uichukie bodaboda na biashara yenyewe.
 
Pindi Rafiki yangu alivyolizwa kwa kuibiwa na na Nyingine ikapata Ajali
hii biz naiona nux!!
 
Bado hajakubadilishia vfaa,yaan vzima aweke vbov yaani ni mizinga kila leo,labda upate mtu mwaminifu.
 
Tulishapita huko mkuu na tulipga sana hizo mathematics kabla hatujawakabidhi hawa vijana bodaboda!
Sipendi kukukatisha tamaa ila ukitaka kuwezana nao ingia nae mkataba na umkabidhi hiyo bodaboda kama yake kwa dhamana maalum ndani ya miezi 10 tu daily akuletee Tsh10k. Akifuzu huo mtihani muachie iwe yake. Na ili ufanikishe mambo yako anza na pikipiki3 mpaka5 ili ikitokea mmoja kazingua usiumie sana roho.
All in all ugopa kuletewa kipande utabuluzwa na huyo chalii vibaya sana uichukie bodaboda na biashara yenyewe.

Yani kuna jamaa yangu aliingia na hizo assumptions kilichomkuta mpaka leo hana hamu na boda boda!!
 
Wana JF,

Sikuwahi kudhani hapo nyuma kama bodaboda inaweza kutajirisha mtu kwa kumtengenezea mpaka Tshs 3 millioni kwa mwezi (other factors remain constant) kwa kuanza na bodaboda moja tu!

Imagine umenunua bodaboda MPYA aina ya Boxer (pamoja na gharama zingine kama insurance nk) kwa Tshs 1.7 million.

Been There, Done That.
Jaribu lakn. Kila La Kheri.
 
Back
Top Bottom