Ni miaka 10 sasa tangu hayati Mkapa atuite watanzania tunaopenda upinzani “malofa”

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
11,449
Reaction score
9,738
Nyakati zinakimbia sana!

Miaka 10 iliyopita wakati wa kampeni za kumuweka madarakani John Pombe Magufuli, hayati Benjamin Mkapa alitupa tusi lenye kejeli ndani yake la kutuita malofa.

Sijui nini kilimsibu mzee wa lupaso mpaka apayuke neno lile gumu kwa Watanzania.

Anyway yeye na Magufuli waendelee kupumzikaa kwa amani huko walipo!!
 
Kama niko sawa, hii kauli alitoa akizindua something NMB akasema kila m Tanzania awe na akaunti hata ukiwa lofa huwezi kosa elfu kumi ya kufungua akaunti.
 
Hapana,ilikuwa mkutano wa kampeni Jangwani kama sikosei.
Alikuwa sahihi sana.
 
Kama niko sawa, hii kauli alitoa akizindua something NMB akasema kila m Tanzania awe na akaunti hata ukiwa lofa huwezi kosa elfu kumi ya kufungua akaunti.
Mama unazeeka sasa.

Kauli ya kuwa wanaotaka mabadiliko ni malofa au wavae siketi hii aliitoa katika majukwaa ya kisiasa.
 
Kama niko sawa, hii kauli alitoa akizindua something NMB akasema kila m Tanzania awe na akaunti hata ukiwa lofa huwezi kosa elfu kumi ya kufungua akaunti.
Hapana, hakuwa akiongea mambo ya benki wala biashara. Alikuwa anafoka kuhusu kitu na ndio maana akasema "ni malofa tu hao" na alikuwa amepaniki balaa anaongea kwa jazba sana. Video mbona zipo.
 
Au huenda gauge ilikua inasoma kile kinywaji chake pendwa chenye jitu limenyanyua mikono😃
 
Alichotuambia ni ukweli, wengi wetu ni malofa
 
Back
Top Bottom