Ni mazingira gani unaweza kumpata mchumba?

Dah!hii kali ya mwaka unauliza mazingira yapi,mbona mengi sana jamani kwani wewe hufanyi kazi?hauishi na watu?hausali/kuswali? huna marafiki wa kiume ambao wana mademu au wake?ila nenda taratibu usje ukapanga kulumbembe ukajuta maisha yako yote.
 
Kazini. mtaani unakoishi kanisani kama wewe ni mkiristo. ni vema ukaoa mtu mwenye imani na malengo kama yako kwa afya ya ndoa yako.
 
Shagiguku ndo mawazo gani hayo jamani. Mmmh mke mwema kwako anatoka kwa bwana Mungu, hebu tulia na Mungu, wakati ukifika utamuona tu.
Hivi huu muda ni upi wa kujua ndo Bwana atanipa huyu mke?Ufafanuzi plz!
 
Kwenye kituo unachopandia daladala kwenda ofcn au ndani ya daladala,
wa mgahawani muda wa lunch wazushi kibao!
Kama hupandi daladala we jaribu kutupia macho ukiwa wapita,hasa asubuhi.
Da Pretty umenikumbusha hapa kituoni ninapopandia daladala kuna dada nakutana nae kila asubuhi nampenda kweli wallahi ila muda mchache wa kumweleza:dance:, kesho nitaanza kampeni rasmi
 
Dah! Kazi kweli kweli, sasa hivi labda uende chuo cha kutongoza maana inaonyesha we ni bonge la mshamba kwenye hizi fani(jokes bwana) usijali mjomba haya mambo huwa yanakuja automatically, cha muhimu we jichanganye na watu wote katika sehemu zao walipo mf chuch, kazini na uonyeshe upendo kwa hawa viumbe(unawatafuta) na uonyeshe unawajali.

Nimekuelewa ila Mimi sio mshamba
 
Inaelekea upo serious sana hata njiani ukikutana na warembo huonyeshi uso wa bashasha (sio bashasha la kulazimisha), mkuu hakuna formula wapo wengi tu kuanzia unapotoka tu mlangoni kwako, unaokutana nao njiani, kwenye vituo vya daladala mpaka maeneo yako ya mishemishe kikubwa na wewe uchamke kiasi kwamba hata uwepo wako watu wawe wanautambua na ukiwa haupo watu wanakuulizia (ukianzia hapo mambo mengine yanafuata, yaani huna hata madada wa hiari? au kwenye group discussion nako ulikuwa hushiriki? na kama unashiriki kulikuwa hakuna hata somo moja ambalo mchango wako ulikuwa unaonekana kiasi kwamba ukajenga interest ya kuongeza marafiki wengi mwisho wa siku kwenye ku-network ukaanza kukutana na sampuli tofauti tofauti humo humo unaweza kubahatisha kwa kuanza na urafiki then UCHUMBA)
 
Mawazo yako mazuri
 
mi wangu nilimpata public toilet, siku hiyo nadhani alikua anaendesha.... fanya kupita pita na huko
 
Wana JF nisaidieni kwa hili....
Hivi karibuni nimeanza kazi baada ya kuhitimu chuo. Kipindi nikiwa nasoma nilikuwa sijihusishi na mambo ya mapenzi na wala nilikuwa sina mchumba kwa wakati huo. Hivi sasa ndo naanza maisha ila sijafahamu mazingira ambayo nikipitapita ntapata mchumba. Najua humu ndani kuna wanandoa, wenye wapenzi pamoja na wengine wenye uzoefu nadhani baadhi watakuwa walipitia huku. Jamani wana JF naombeni msaada wenu wa mawazo.

Mkuu mchumba huwa anakuja automatically kwenye mazingira yoyote yale tena ndo una kazi ndo kabisaaaa! Vuta subira tu watamiminika hadi ushindwe pa kukimbilia!
 
Hakuna utaratinu maalumu uliopo wa kupata mchumba, wala mtu huwezi kusema labda leo nasafiri naenda mkoa fulan kutafuta mchumba hi kitu hutokea automatically na nakuambia hutaamini siku utakapo kutana na huyo mchumba unae mtaka!! cha msingi ni kumuomba mungu akusidie! Angalizo usije uwaka kimya every day ukategemea kuwa mungu atakushushia mpenzi au utaota niende mahala fulan ndo mchumba alipo be social i mean socialize then atatoea na mtajikuta mmejenga relation! Nadhan wewe ni mmoja wa wale watu wanaosema ngoja nisome nikiwa kazini ndo nitakuwa na mchumba wakati uko chuo nakwambia ndugu yangu utafika kazini almost kila mtu occupied hapo ndo utabak unashangaa nina nariki yangu hadi leo anaangaika wakati tuko chuo yeye alisema anasubir amalize akiwa kazin ndo atampata mpaka leo anangoja tu! kila la kheri mungu atakusaidia utampata wa ukweli
 
ingia kwenye social networks ila tahadhariii uschague walovaa uchi na kutojistiriiii usije ukaopoaa changu la manzese angalia wanaojistil wapo weng nawaoo wanatafuta wenza anza na jf,badoo,fb,insta msg, ukishindwaa na hukuu tafuta plan B ambayoo unatakiwa uchukue simu yako uwe unqpiga wrong number ahaha utabahatikaaa tu.
plan c: ikishindikanaa chukua elf10 kanunue sumu ya panya unywe usdai change
 
Back
Top Bottom