Unakata tamaa? Pambana, njia bado ni nyeupe, 2024 hodi, 2023 ilikupa funzo gani?

kitalembwa

JF-Expert Member
Jul 12, 2014
2,870
7,171
With all due respect

Ni mwaka sasa sijaweka bandiko hapa ,,,

Well, kwa kudra za M/Mungu bado tungali buheri wa afya na tunaendelea na majukumu ya kila siku ,,,

2023 ni mwaka ambao pengine umeweka alama kubwa sana kwenye historia ya masiha yangu ,,,,

Ni mwaka ambao niliachana na mpenzi/mchumba wa siku nyingi ambaye tayari tulikuwa na mipango ya ndoa ,,,,
Sitosahau Mapito niliyopitia, Mungu si athumani, tumerudiana na kwa sasa ni mjamzito, mwakani ndoa na mahari nimeshamtolea ,,,,,

Kubwa kabisa ,kuna taasisi moja nafanya ya kiserikali (kazi niliipata kupitia kwa mwana jf mmoja humu, mwenye roho ya dhahabu, nilishaleta uzi humu kuhusu huu mchongo)!!!

Sasa bhana, iko hivi,,, kuna sintofahamu ilitokea job, nilisimamishwa mimi na wenzangu wanne kupisha uchunguzi ,,, tulikaa benchi miezi sita , hatimae ripoti ikatoka, mimi na madam mmoja hivi tulinusurika tukarudishwa kazini ,,, jamaa zangu watatu kwa Bahati mbaya walikumbwa na hii kadhia hali iliyopelekea wao kupoteza kibarua !

Kwa nini nimeeleza haya ? Twende pamoja, unaweza kujifunza jambo, Kipindi job panatokea sintofahamu (sipendi kuiweka humu naweza kufungua code), ni kipindi ambacho nilikua sina akiba yoyote, ndo kwanza nilikuwa kwenye harakati za ujenzi, pia kuna biashara flani nilikuwa ndo nimeifungua mahali ikiwa bado changa kwa hiyo sikuwa na kitu,,,, ghafla job nikapigwa pini, mshahara ukastopishwa,,,,

Huku biashara changa, nina ujenzi,,,aloo nilikwama sitosahau, nilisimamisha ujenzi na kuna bags kadhaa za cement ziliharibika,,,, biashara ikawa ndo changa ngumu, vijana wanaharibu nikawa sina kipato,,,,

Kuna mtu/mshkaji nilikuwa namdai kiasi flani, nae ahadi nyingi , hakuna pesa,,, nilikuwa mtu wa kushinda tu ndani, kunywa pombe tu basi ,,,, nahisi hiki kipindi ndo kilisababisha nikagombana na mchumba, make mda wote nilikuwa mtu wa kisirani , yani sina jema hata unifanyie kitu gani !

Hiki ni kipindi ambacho nilitengwa na kila mtu, nilikuwa kama nimechanganyikiwa,,,, washkaji wadau wakipata habari kuwa jamaa hana kazi wanakukataa na simu hawakupokelei ,,,

Nikiri wazi kuna hadi ndg zangu wa damu ukimpigia simu yani hana mambo mengi anataka akusikie unasemaje sio blah blah,,,, kuna sister yangu blood kabisa aloo kanifanyia dharau sana ,,, hiki ni kipindi ambacho nilimjua ni nani ndg na ni nani adui ,,,,

Kuna bi mkubwa mmoja nilimkuta job ndo alikuwa mfariji wangu wa pekee, sometimes ananipgia simu na kunijulia hali na kunipa moyo,,,, washkaji wote job hakuna mwenye time na wewe ,,,

Ni mengi sijayaeleza hapa,,, pengine lengo la huu uzi ni kama kujifunza ,,, kuishi na watu na mazingira kwa ujumla,,,,usiwaamini sana watu ,,,,
Hakuna anayependa maendeleo yako ,,,, ukitaka kujua una maadui wengi hebu kwama kidogo ndo utaonja joto la jiwe ,,,,,

Now job nisharudi kila kitu kipo OK,, Mungu ni mwema, kampani nimepunguza ama niseme sina kabisa,,,, pia sikopeshi mtu pesa, sitoi msaada kizembe kwa ndg na jamaa marafiki, bora nipeleke kwa wenye uhitaji ,,,,,

Happy 2024 in advance !!! Cheeeeeèeers
 
Pole sana best nilikua nakutag kwenye story nyingi sana naona kimyaa nikahisi something was wrong...
Thanks God kumbe upo na asante kwa story ngoja nikitulia nisome vizuri?
Be blessed
Ahsante best,,,,,alafu app hii inazingua sionagi notifications,,,, !!! Sijui nifute nidanload upya
 
Mwaka 2023 daah mwaka wa maumivu na mateso sana. Mwezi 2 ilikuwa nasubiri majina tu yatoke job TRA interview zote tayar zimeenda powa majina yanatoka olaa nikakosa job nipo.street napambana mwezi wa 7 baba anafariki sitausahau mwaka 2023 mimi kamwee.
 
Mwaka 2023 daah mwaka wa maumivu na mateso sana. Mwezi 2 ilikuwa nasubiri majina tu yatoke job TRA interview zote tayar zimeenda powa majina yanatoka olaa nikakosa job nipo.street napambana mwezi wa 7 baba anafariki sitausahau mwaka 2023 mimi kamwee.
Kamwe usikate tamaa ndg yangu
 
Back
Top Bottom