Ndoto ya kuwa darasani au mazingira ya shule ina maana gani?

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Japo mrisho mpoto alikmbaga kwamba usimsimulie mtu Ndoto yako ya jana usiku lakini mi binafsi imenishinda imenibidi niisimulie tu,

Ni hivi Nimekuwa nikiota mara nyingi sana, ni ndoto inayojirudia mara kwa mara,
"Naota nikiwa mazingira ya shule ya sekondary nasoma tena ile shule niliyomalizia kabisa, lakini kila inapofikia kipindi cha karibu na kufanya mtihani wa Taifa Nacte, tusema labda wiki moja kabla huwa Najikuta hakuna chochote nilichogain darasani,

Yaani kuna baadhi ya masomo naona kabisa hakuna nilichosoma kila Nikishika daftari nakuta nina mengi ya kucover na muda wenyewe hautoshi basi nabaki kuchanganyikiwa, mpaka karibu na mtihani ila cha kushangaza siku zote hii ndoto huwa inaishia tu pale ninapokaribia kuingia kwenye chumba cha mtihani huku nikiwa na mawazo lukuki"

Je kuna yeyote mwenye kujua maana ya hii ndoto kweli? Anisaidie maana ni inakuja mara kwa mara mpaka nahisi kuna kitu naambiwa kupitia ndoto lakini napuuzia.

Na kuna Ndoto nyingine nayo kama hii ya shule nayo inanijia mara kwa mara ni kama zinapokezana Ndoto yenyewe ni kwamba,

" huwa Naota niko darasani kidato cha nne tena shule ile ile niliyosoma na kumaliza, wanafunzi ni wale wale niliosoma na kumaliza nao.

Huwa najikuta niko darasani tunasoma let say mwalimu kaingia kafundisha na kuondoka lakini ghafra tu nakuwa kama nimefumba macho na kufumbua nakuta darasa jeupe pee halina mwanafunzi ata mmoja,ata yule rafiki niliekuwa nakuwa nae kila sehemu nae hayupo.

Nakuwa mwenyewe naangaika kuita majina, mara huyu mara yule basi ile kutokuwaona nashikwa na huzuni na kuanza kulia nahisi kama wamenikimbia na ni vipi naweza kukutana nao tena, kuna wakati nililia tena kwa kwikwi kiasi cha kuamshwa na manzi flani nilikuwa nae siku ile na kuniuliza mbona nalia usingizini" ni kweli huwa napata hisia za ajabu ata kwenye maisha ya kawaida baada ya hii nahisi kama nimetengwa na niko mpweke peke yangu.

Mwenye kujua maana ya hii ndoto pia naomba anifafanulie kwa kweli inanitesa pia tena sana.

Najua kuna watu wenye hii taaluma.

Cc Zero IQ
 
Roho ya kurudishwa nyuma kimaisha...

Uchawi au Mizimu inahusika...

Ni kweli amka,utarudi nyuma binafsi nilikua naota nipo chuo najiandaa na UE,katika pitapita zangu nikakutana page ya Mchungaji Emanuel alikua anaelezea ndoto Kama hiyo na maana yake ni kurudi nyuma kwa tafsiri yake kiroho.Nikapuuzia kiana,

Nakuambia niliyopitia ili uamke Mapema
Kilichofuata aisee Mungu Ndio aliingilia kati,nikapoteza kazi, nikauza kiwanja,Nikauza gari mambo hola, bado kidogo nikopee mkopo nyumba nayo nahisi ingeenda.Nilisimama kwa Mungu nikamuomba sana maana nilikua naaibika mjini.
 
Sehemu uliokwama ni hapo,shule..kama hukumaliza kamalizie semester kama ulimaliza you chose the wrong course or ulitakiwa usome juu zaidi like postgraduate or masters..mkwamo wako unahusiana na shule
Kweli mkuu nilisoma ila nilipoishia si sehemu nilikuwa nategemea, mkwamo wa ada tu si unajua maokoto ya mavyuo ya Afya
 
Umechakata nuksi mkuu kwenye kiwanda chako.

Pumzika kuchakata, fanya ibada.. Kuna mlango mkubwa uko mbele yako. Ukifunguka utabadilisha maisha yako na ya jamii Kwa kiwango kikubwa. Sasa nguvu kinzani ipo kukurudisha nyuma. Pambanaa
 
Japo mrisho mpoto alikmbaga kwamba usimsimulie mtu Ndoto yako ya jana usiku lakini mi binafsi imenishinda imenibidi niisimulie tu,

Ni hivi Nimekuwa nikiota mara nyingi sana, ni ndoto inayojirudia mara kwa mara,
"Naota nikiwa mazingira ya shule ya sekondary nasoma tena ile shule niliyomalizia kabisa, lakini kila inapofikia kipindi cha karibu na kufanya mtihani wa Taifa Nacte, tusema labda wiki moja kabla huwa Najikuta hakuna chochote nilichogain darasani,

Yaani kuna baadhi ya masomo naona kabisa hakuna nilichosoma kila Nikishika daftari nakuta nina mengi ya kucover na muda wenyewe hautoshi basi nabaki kuchanganyikiwa, mpaka karibu na mtihani ila cha kushangaza siku zote hii ndoto huwa inaishia tu pale ninapokaribia kuingia kwenye chumba cha mtihani huku nikiwa na mawazo lukuki"

Je kuna yeyote mwenye kujua maana ya hii ndoto kweli? Anisaidie maana ni inakuja mara kwa mara mpaka nahisi kuna kitu naambiwa kupitia ndoto lakini napuuzia.

Na kuna Ndoto nyingine nayo kama hii ya shule nayo inanijia mara kwa mara ni kama zinapokezana Ndoto yenyewe ni kwamba,

" huwa Naota niko darasani kidato cha nne tena shule ile ile niliyosoma na kumaliza, wanafunzi ni wale wale niliosoma na kumaliza nao,
Huwa najikuta niko darasani tunasoma let say mwalimu kaingia kafundisha na kuondoka lakini ghafra tu nakuwa kama nimefumba macho na kufumbua nakuta darasa jeupe pee halina mwanafunzi ata mmoja,ata yule rafiki niliekuwa nakuwa nae kila sehemu nae hayupo,
Nakuwa mwenyewe naangaika kuita majina, mara huyu mara yule basi ile kutokuwaona nashikwa na huzuni na kuanza kulia nahisi kama wamenikimbia na ni vipi naweza kukutana nao tena, kuna wakati nililia tena kwa kwikwi kiasi cha kuamshwa na manzi flani nilikuwa nae siku ile na kuniuliza mbona nalia usingizini" ni kweli huwa napata hisia za ajabu ata kwenye maisha ya kawaida baada ya hii nahisi kama nimetengwa na niko mpweke peke yangu.

Mwenye kujua maana ya hii ndoto pia naomba anifafanulie kwa kweli inanitesa pia tena sana.

Najua kuna watu wenye hii taaluma.

Cc Zero IQ
Ndoto zozote za madarasa ya nyuma ni kiashiria cha kukwama katika maisha. Ndoto hizi huashiria kukwama au kurudishwa nyuma kimaendeleo kunakofanywa katika roho.

Kuota classmates wamekuacha kuna maanisha kuchelewa katika jambo la rika lako kama vile kuchelewa kupata fedha, mafanikio au kuoa/kuolewa.

Unapaswa kuchukua hatua za haraka sana kujinasua na mtego uliokunasa la sivyo utachelewa zaidi na kuharibu maisha yako.
 
Hatua za kuchukua ni zipi?
 
Japo mrisho mpoto alikmbaga kwamba usimsimulie mtu Ndoto yako ya jana usiku lakini mi binafsi imenishinda imenibidi niisimulie tu,

Ni hivi Nimekuwa nikiota mara nyingi sana, ni ndoto inayojirudia mara kwa mara,
"Naota nikiwa mazingira ya shule ya sekondary nasoma tena ile shule niliyomalizia kabisa, lakini kila inapofikia kipindi cha karibu na kufanya mtihani wa Taifa Nacte, tusema labda wiki moja kabla huwa Najikuta hakuna chochote nilichogain darasani,

Yaani kuna baadhi ya masomo naona kabisa hakuna nilichosoma kila Nikishika daftari nakuta nina mengi ya kucover na muda wenyewe hautoshi basi nabaki kuchanganyikiwa, mpaka karibu na mtihani ila cha kushangaza siku zote hii ndoto huwa inaishia tu pale ninapokaribia kuingia kwenye chumba cha mtihani huku nikiwa na mawazo lukuki"

Je kuna yeyote mwenye kujua maana ya hii ndoto kweli? Anisaidie maana ni inakuja mara kwa mara mpaka nahisi kuna kitu naambiwa kupitia ndoto lakini napuuzia.

Na kuna Ndoto nyingine nayo kama hii ya shule nayo inanijia mara kwa mara ni kama zinapokezana Ndoto yenyewe ni kwamba,

" huwa Naota niko darasani kidato cha nne tena shule ile ile niliyosoma na kumaliza, wanafunzi ni wale wale niliosoma na kumaliza nao,
Huwa najikuta niko darasani tunasoma let say mwalimu kaingia kafundisha na kuondoka lakini ghafra tu nakuwa kama nimefumba macho na kufumbua nakuta darasa jeupe pee halina mwanafunzi ata mmoja,ata yule rafiki niliekuwa nakuwa nae kila sehemu nae hayupo,
Nakuwa mwenyewe naangaika kuita majina, mara huyu mara yule basi ile kutokuwaona nashikwa na huzuni na kuanza kulia nahisi kama wamenikimbia na ni vipi naweza kukutana nao tena, kuna wakati nililia tena kwa kwikwi kiasi cha kuamshwa na manzi flani nilikuwa nae siku ile na kuniuliza mbona nalia usingizini" ni kweli huwa napata hisia za ajabu ata kwenye maisha ya kawaida baada ya hii nahisi kama nimetengwa na niko mpweke peke yangu.

Mwenye kujua maana ya hii ndoto pia naomba anifafanulie kwa kweli inanitesa pia tena sana.

Najua kuna watu wenye hii taaluma.

Cc Zero IQ
Katafutie chumvi ya mawe,ogea kwa manuizi asubuhi na jioni.chumvi kiganja kimoja.
Utanishukuru
 
Back
Top Bottom