Ni mashine ipi nzuri kwa kutotoleshea vifaranga?

Manchid

JF-Expert Member
May 29, 2016
217
445
Kama ambavyo kichwa Cha habari kinaeleza, Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji toka singida singidani Nina deal na Hawa kuku na hakika nmeona ni wastahimilivu sana wa magonjwa endapo wataanza kupewa chanjo na mazingatio mengine toka wakiwa wadogo.

Sasa nataka kununua mashine kwaajili ya kuboresha na kuongeza kipato changu, hivyo nahitaji wajuvi wa Mambo mnijuze je mashine ipi ni nzuri zaidi Kati ya hizi zinazotengenezwa sido I mean made in Tanzania na hizi za kisasa toka nje.

Na je Bei rafiki ya nashine yenye uwezo wa kuchukua mayai around 300 mpk 400.

Mahali nilipo upatikanaji wa mayai ya kienyeji unaridhisha sana,je ni sahihi kununua mayai kwa wafugaji wengine na kuyatotolesha? Ama mpaka nitengeneze mzunguko wangu binafsi utakaokidhi mahitaji yangu?

Mwisho napenda kuwakaribisha ndugu zangu kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji kwani wanalipa na Wana faida sana pale wanapozingatiwa na kutunzwa vizuri.

Alamsiki
 
Kuku ninaowafugaView attachment 2122356View attachment 2122357
IMG_20211226_090832_674.jpg
Screenshot_20211218-163716.jpg
IMG_20211218_163945_998.jpg
IMG_20211218_164006_107.jpg
IMG_20211218_164024_289.jpg
Screenshot_20211218-163439.jpg
IMG_20211022_171916_731.jpg
IMG_20211022_155221_633.jpg
 
Attachments

  • IMG_20211022_172119_775.jpg
    IMG_20211022_172119_775.jpg
    159.9 KB · Views: 96
Kwa upande wa mayai jitahidi utengeneze mzunguko wako. Ukiwa na majike waziri 50 nina imani utaweza pata hayo mayai unayotaka kwa mda muafaka
 
Manchid Hongera kwa ufugaji. Mashine ya mayai 300-400 hapo bajeti iwe kwenye 600,000 kuendelea.

Mashine za hapa Bongo. Siwezi kuthibitisha ubora wake, tuliwahi kuwa nayo haikufanya vizuri Sana. Sasa hivi imekuwa screpa. Fanya utafiti.

Kuhusu kununua mayai na kuyatotolesha inawezekana Kama una uhakika ni mayai Safi, Yana mbegu ya jogoo (kumbuka kuku anaweza kutaga HATA kama hakuna jogoo Ila mayai hayataweza kutotoa) na pia kama hayajapitisha siku 7. Na hayajaanza kulaliwa.

Ni vizuri kuatamisha mayai yaliyotoka bandani kwako kwa sababu unayajua yametagwa lini, mbegu ya kuku, una uhakika wa kuwa na jogoo n.k
 
Shukrani Sana kwa ushauri mkuu
 
Kuna tatizo la kukatika
kwa umeme, vipi umeme wetu huu ukikatika inakuwaje au incubator zenu zinao Mfumo wa umeme wa Solar?
Umeme haukatika kwa siku nzima mayai hayana shida sana cha muhimu uweze kukontro unyevu maana embryo huwa inajitengenezea joto lake lenyewe
 
Back
Top Bottom