Ni maneno gani matamu unaweza kumwambia mpenzi wako yakamfanya asisimuke na kukupenda?

Kwa wale wataalamu wa maneno Hebu tusaidiane ni maneno Gani ukimwambia mtoto wa kike au kiume akiwa kama mpenzi yakamfanya moyo wake usisimke na kukupenda zaidi

Kama unayo hebu tupia maneno matamu ya kumsisimuaa mpz wako kiasi kwamba akasisimka na kukupenda hatari
Yani mimi demu akiniambia maneno matamu sana, akawa na mahaba yaliyopitiliza kama ya kwenye vitabu uwa nahisi kama anataka kunitapeli au ataka kunipa limbwata uwa nakuwa muda wote nimesimamisha machale mguu nje mguu ndani.
 
Yani nikutumie 2M kisha uninunulie chocolate ya ivori ya buku? 😁😁😁
Hahaaa babe zawadi ni zawadi ila ukituma hiyo aki naongeza zawadi! Naenda kutafuta kiatu kikali na shati flani la blue bahari hivi na suruali dark blue! Nikikuletea hapo utachekelea kumbe kwenye 2m nimetoa laki 2 tuu then 1.8m ni net profit 😀😀
 
Hahaaa babe zawadi ni zawadi ila ukituma hiyo aki naongeza zawadi! Naenda kutafuta kiatu kikali na shati flani la blue bahari hivi na suruali dark blue! Nikikuletea hapo utachekelea kumbe kwenye 2m nimetoa laki 2 tuu then 1.8m ni net profit 😀😀
Hahahahah ndio maana hatuwaachi wanawake wetu wa kibongo. Mna vituko vya pekee ambavyo ni ngumu sana kuvipata hata Kenya tu 😂😂😂
 
Hahahahah ndio maana hatuwaachi wanawake wetu wa kibongo. Mna vituko vya pekee ambavyo ni ngumu sana kuvipata hata Kenya tu 😂😂😂
Hahaa mbona kawaida tu sasa si bora hata anayekunulia chochote! Kuna wengine ukiwapa hiyo ndo ishatoka anapanga bajeti zake huko 😀😀
 
Hahaa mbona kawaida tu sasa si bora hata anayekunulia chochote! Kuna wengine ukiwapa hiyo ndo ishatoka anapanga bajeti zake huko 😀😀
Maneno matam yanajenga penzi zaidi ya pesa Penzi linalojengwa kwa pesa jepesi kupata usaliti kuliko ninalojengwa kwa maneno matam yatokayo moyoni na yenye kuonesha uhalisia . Mfano " Nikwambie kitu mpenz Najiona mwenye bahati sana kua na mke/mume kama ww mbali na uzuri wa umbo lako akili fikra na mawazo yako yananipa nguvu ya kujiona ni mtu kwenye watu hata kwa hiki kidogo nilichonacho na kwa namna unavyonistahamilia na kunishauri vyema hakika ww ni make/mume sahihi kwangu.

Nakupenda zaidi ya neno lenyewe" Mfano wa madhara ya pesa " Nimekutumia milioni 1 kafanye shopping beby kina kudume mwengine day lake million 2 kipi kitamuweka kwako milioni 1 au 2 ya jamaa .maana anakua hana kitu kitakachomfanya ajihisi special kwako.
 
Cha msingi ukiongea nae kua polite ktk simu onyesha kujali onyesha kumtegea sikio mwisho wa maongezi muulize matatizo yake akikwambia hana basi usimpe pesa akisema analo mtatulie au akikohoa tu mwambie ntakutumia pesa ununue uviko,barakoa na sanitizer ili awe safe maana ye ndo furaha kwako
 
Maneno matam yanajenga penzi zaidi ya pesa Penzi linalojengwa kwa pesa jepesi kupata usaliti kuliko ninalojengwa kwa maneno matam yatokayo moyoni na yenye kuonesha uhalisia . Mfano " Nikwambie kitu mpenz Najiona mwenye bahati sana kua na mke/mume kama ww mbali na uzuri wa umbo lako akili fikra na mawazo yako yananipa nguvu ya kujiona ni mtu kwenye watu hata kwa hiki kidogo nilichonacho na kwa namna unavyonistahamilia na kunishauri vyema hakika ww ni make/mume sahihi kwangu Nakupenda zaidi ya neno lenyewe" Mfano wa madhara ya pesa " Nimekutumia milioni 1 kafanye shopping beby kina kudume mwengine day lake million 2 kipi kitamuweka kwako milioni 1 au 2 ya jamaa .maana anakua hana kitu kitakachomfanya ajihisi special kwako.
Wacha maneno mengi ww pesa ni mpesa tu, maneno hayalipi bills
 
Wacha maneno mengi ww pesa ni mpesa tu, maneno hayalipi billsp
Punguza miamala Mapenz hayanunuliwi utakuja kuwalaumu bure hawa viumbe uchawi wao ni kuwafanya wajione muhimu wake kwako sio ww kwake yy anajua anakuna na watu wenye pesa zaidi yako ila atawapuuza akijua thamani yake kwako
 
Kama ni hivyo acha niendelee kuzisaka kwa ajili ya mke wangu mpenzi
 
Mshikaji ananitumia sms "oya kaka ule mzigo tumeuza wote ila daa kidogo tukamatwe na police"

Namtumia sms mywangu

"baby kesho mchana mdogowangu atakuletea laki 8 uongezee kwenye biashara yako alafu jion ntakutumia laki 2 utatue mahitaji yako binafsi"


MUDA HUO NIKO NA MCHEPUKO WANGU LODGE
 
Back
Top Bottom