Salamu sana,
Poleni na majukumu ya kujenga taifa.
Kwanza kabisa napenda kumshukuru sana Mungu Kwa ajili ya binti yangu ambaye amehitimu chuo. Alisoma shahada yake Chuo Cha Usafirishaji Ubungo.
Lengo kubwa la Uzi huu ni kutoa neno la shukrani Kwa wale wote walionitia moyo hasa wakati ule alipokosa mkopo. Namshukuru sana Katibu Mkuu wizara ya elimu ambaye niliingia ofisini kwake nikajieleza na akanishauri, hata hivyo mwaka wa pili alifanikiwa kupata mkopo.
Wapendwa, kwa mapenzi mema kabisa nawakaribisha kwenye mahafali hayo 13/1/2018. Njoo hata tupate soda tu. Endapo utajaliwa kuja niambie ili nikupe simu namba.
Mtakaopenda kutununulia soda pia karibuni.
Ni mbali sana Mungu ametutoa. Nina ushuhuda wa kipekee kwani huyu binti akiwa nursery school ndipo tulipotengana na baba yake ila Mungu hakututupa. Kila hatua amekuwa nasi.
Karibuni.
Mkinitukana nitalia.