Ni mahafali ya binti yangu

Ni mahafali ya binti yangu

Salamu sana,

Poleni na majukumu ya kujenga taifa.

Kwanza kabisa napenda kumshukuru sana Mungu Kwa ajili ya binti yangu ambaye amehitimu chuo. Alisoma shahada yake Chuo Cha Usafirishaji Ubungo.

Lengo kubwa la Uzi huu ni kutoa neno la shukrani Kwa wale wote walionitia moyo hasa wakati ule alipokosa mkopo. Namshukuru sana Katibu Mkuu wizara ya elimu ambaye niliingia ofisini kwake nikajieleza na akanishauri, hata hivyo mwaka wa pili alifanikiwa kupata mkopo.


Wapendwa, kwa mapenzi mema kabisa nawakaribisha kwenye mahafali hayo 13/1/2018. Njoo hata tupate soda tu. Endapo utajaliwa kuja niambie ili nikupe simu namba.

Mtakaopenda kutununulia soda pia karibuni.

Ni mbali sana Mungu ametutoa. Nina ushuhuda wa kipekee kwani huyu binti akiwa nursery school ndipo tulipotengana na baba yake ila Mungu hakututupa. Kila hatua amekuwa nasi.

Karibuni.

Mkinitukana nitalia.

Naomba namba ya binti yako nimpongeze
 
Kutengana siyo historia nzuri, kama katika ukoo wako mama yako au bibi walitengani, jua fika mbeleni yatatokea kwa binti yako! Dawa ni kuomba huo mkosi kizungu tunasema’Curse’ ivunjwe kwa sala maalum bila malipo wala mchango(free of charge)ukihitaji ushauri sema.
Shindwa!
 
I think ulikuwa unamaanisha Mahafari yanafanyika Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji ( NIT) kilichopo mabibo na siyo Chuo cha Usafirishaji cha Ubungo.
Ni sawa, si unajuwa tena i am old enough kujuwa hivi vitu.
 
Asanteni sana kwa mlionipa hongera,
Mungu awabariki sana;
Kweli kama siyo Mungu sijui hata ingekuwaje.
Asanteni wote,
 
Hongera kwa Binti na kwako Mamndenyi kwa kumkuza na yote.

Mola azidi kuwabariki na kuwamwagia Baraka tele tele.
 
Back
Top Bottom