Ni mahafali ya binti yangu

Ni mahafali ya binti yangu

Mamndenyi

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
44,614
Reaction score
64,470
Salamu sana,

Poleni na majukumu ya kujenga taifa.

Kwanza kabisa napenda kumshukuru sana Mungu Kwa ajili ya binti yangu ambaye amehitimu chuo. Alisoma shahada yake Chuo Cha Usafirishaji Ubungo.

Lengo kubwa la Uzi huu ni kutoa neno la shukrani Kwa wale wote walionitia moyo hasa wakati ule alipokosa mkopo. Namshukuru sana Katibu Mkuu wizara ya elimu ambaye niliingia ofisini kwake nikajieleza na akanishauri, hata hivyo mwaka wa pili alifanikiwa kupata mkopo.

Wapendwa, kwa mapenzi mema kabisa nawakaribisha kwenye mahafali hayo 13/1/2018. Njoo hata tupate soda tu. Endapo utajaliwa kuja niambie ili nikupe simu namba.

Mtakaopenda kutununulia soda pia karibuni.

Ni mbali sana Mungu ametutoa. Nina ushuhuda wa kipekee kwani huyu binti akiwa nursery school ndipo tulipotengana na baba yake ila Mungu hakututupa. Kila hatua amekuwa nasi.

Karibuni.

Mkinitukana nitalia.
 
Kutengana siyo historia nzuri, kama katika ukoo wako mama yako au bibi walitengani, jua fika mbeleni yatatokea kwa binti yako! Dawa ni kuomba huo mkosi kizungu tunasema’Curse’ ivunjwe kwa sala maalum bila malipo wala mchango(free of charge)ukihitaji ushauri sema.
 
Hongereni kwa pamoja,kwanza kwako kama mzazi kwa kutia nguvu kumfikisha hapo na kwake kama mwanafunzi kwa kupigana mpaka kufika hapo.
 
Hongera sana ila fahamu umekuwa sasa habar zakuchangia Uzi usio na maadili achana nazo
 
Back
Top Bottom