Hahahaha umepewa onyo umeanza kulainisha lugha, eti kitabu kitakatifu. Kitabu hicho hicho kinakuasa utiii mamlaka iliyowekwa kihalalinitashangaa kama polisi wakitumia silaha za moto , maana waandamanaji siku hiyo tutakuwa tumebeba BIBLIA NA QURAN takatifu...... Tukiomba Mungu atuletee mapinduzi ya viwanda,kifikra,kiroho na kiakili Tanzania
Nakukumbusha tu kule Misri raia walikuwa wakishangilia juu ya vifaru au hukuwaona?Haki ya Nani nina hamu ya kuona kwa macho nini kitatokea siku hizo. Jeshi letu limesikika kwa kudhibiti machafuko nchi za wenzetu. sasa ni zamu ya nyumbani
Hata ww si haujui bas na hii ndo teknik ya 26/4. Si Polisi wala JW anaejua nini kinaenda kutokea. Hawajui wajipangaje (kulinda raia/kudhibiti), hata mahali yatakapofanyika na yataratibiwa kwa namna gan kila kitu hakijulikan. Ila yapo.Kumbe hata hamjui!
Wanaongozwa na Mnyonya koni. Mapinduzi kote duniani hudhibitiwa kwa silaha za moto. Na ndivyo itakavyotokea siku hiyo wakithubutu
Kwa kuwa wewe utaishi milele?Hahahahahahaaaaaaa. Hapo mmeeleweka. Siku hiyo wanaume wa Kazi watakuwa na zana zote halali. subirini mkufilie mbali wakati huyo anayewahamasisha ananyonya koni huko majuu
Yanaruhusiwa kwa kufuata sheria na kanuni zake. Sasa sina uhakika kama hivyo vitu vimefutwa na hawa wanaotaka kuandamana.Me najua maandamano kikatiba yanaruhusiwa ila mapinduzi hapana.
Ni Mange huyu huyu anafanya jeshi litoe stock yote je mkitishiwa na Al shababu itakuwaje.So long mmetoa muda wa kutosha na sisi tukajipanga, haki ya nani siku hiyo mtatafuta pa kukimbilia. stock zote za silaha zilizotapakaa nchi nzima siku hiyo zitakuwa nje nje. Na kwa vile tupo na maandalizi ya Siku ya Muungano, tutatest kila silaha ili tuone kama zipo kisawasawa. Maana nyingine zimekaa muda mrefu
Tuliwaambia maandamano yapo mkatubeza lkn kadri siku zinavyosogea ndio akili zinaanza kuwarudi, mwanzo mlisema malaya wa Calfonia huwezi kuongoza maandamano Tanzania, sasa mnasema jeshi lijiandae kisawasawa, na bado hadi maji myaite mma.
Tusibeze, maandamano yapo ila kufanikiwa au kutofanikiwa kwake inategemea Polisi imejipangaje
Sheria inasema kutoa taarifa 48hrs before leo bado miezi miwili wasiwasi wa nini si msubiri?Yanaruhusiwa kwa kufuata sheria na kanuni zake. Sasa sina uhakika kama hivyo vitu vimefutwa na hawa wanaotaka kuandamana.
Nchi za watu??,mtu unapigwa na vumbi hapo lumumba eti nchi za watu,sema baada magu kusitisha buku 7 na uteuzi ulizira...Nipo shule ndugu tena huku nchi za watu. Nimeibuka kwenye hii ishu kutokana na jinsi inavyotaraji kuzaa vilema watarajiwa na marehemu watarajiwa. Ni vema hawa wanaotaraji kufanya hivyo tukawapa somo la kutosha. Maana wengine wanaendeshwa na akili za Wanyonya Koni huko ng'ambo
Tunataka kuandamana ili kufanya mapinduzi. Unaonaje hiyo imekaa vizuri?
Zanzibar waliandamana au walipindua?Wadau, amani iwe kwenu.
Nimefuatilia baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Instagram na Telegram kuhusu haya makundi ya watu wanaotamani kuuangusha utawala wa Rais Magufuli. Kwa kiswahili wanasema kuwa hayo ni maandamano ya Amani. Ila kwa Kiingereza wanatamka Tanzania Revolution.
Kwa uelewa wangu, Maandamano tafsiri yake kwa Kiingereza ni Demonstration au Protests. Na Revolution maana yake kwa kiswahili ni Mapinduzi. Kwa uelewa wangu finyu, busara huweza kutumika katika kudeal na maandamano ikiwa ni pamoja na matumizi kiduchu ya nguvu. Ila Mapinduzi hapo lazima ujidhatiti kukabiliana nayo. Hapo silaha za moto na nzito hutumika na ni haki ya vyombo vya dola kutumia nguvu zote ili kulinda himaya dhidi ya maadui wa ndani na nje.
Kingine, Maandamano hudhibitiwa na Jeshi la Polisi. Ila Mapinduzi hapo wanaume wa kazi, JWTZ huingia mzigoni. Hapo silaha zinazotumika ni za moto tu. Hawajafundishwa kutumia TEAR GAS hao.
Kwa hiyo, ni vema wale wanaotamani kuona utawala wa Rais Magufuli unaangushwa wakatafakari upya ni nini hasa wanataka kufanya siku hiyo na nini madhara yake. Ni vema wakaweka wazi je wanataka kuandamana ama wanataka kufanya mapinduzi? Maandamano YES ila MAPINDUZI ni BIG NO. Watu wasije kufumuliwa vichwa wakifanya mapinduzi then wakaanza kulalamika kuwa jeshi la polisi na JWTZ wametumia nguvu ya ziada.
Ndoto za nchi za wenzenu endeleeni kuziota tu.....Not in Tanzania..mtuachie kisiwa chetu cha amani.Moja ya kitu ulichosahau labda nikukumbushe MISRI ni moja ya nchi yenye jeshi imara kabisa Africa na vifaa vya kisasa kuanzia ndege za kivita za kutosha, mamia ya vifaru na gari za delaya, manowari vita na meli za kivita... lakini mwisho wa siku watu walijiselfie na vifaru barabarani..
Hiyo movie haiwezi fanikiwa sio kwa sababu ya jeshi imara la Tanzania lahasha bali kwa sababu ya uoga na ujinga wa watanzania, Hakuna jeshi lenye nguvu kuliko umma, nahuhakikishia hapo Dar es salaam waandamane watu 10000 tu JWTZ haitaweza kuwazuia kamwe, tuombe Mungu na tuache kauli za kejeli haya mambo ni hatari sana Lizaboni...