Ni maandamano au ni mapinduzi?

Matokeo ndio yatakayotupa jibu la hili swali. Tusubiri.
 
Lizaboni na genge la wahuni wenzake kutoka Lumumba hawafai wanatupoteza
 
Tunataka kuandamana ili kufanya mapinduzi. Unaonaje hiyo imekaa vizuri?
Ka jinsi tangazo lao lilivyo ni wazi wanataka kuendesha mapinduzi. Na wategemee kukutana na wazee wa kazi itawagarimu, Maana mnakurupuka tu
 
Kuandamana nendeni nyie mi nitakuwa kwenye tv nikiangalia kitakachowakuta
Poa mkuu,sio mbaya,wewe kaa kwenye sofa na remote yako angalia matokeo ya manamano,acha wanaume wakapambane,wewe msubiri Kiringo akuletee sharbati
 
Miaka miwili aliyokaa hali iko namna hii je akiongeza iwe saba si tutavaa jinja na kutumia magwanji
 
Poa mkuu,sio mbaya,wewe kaa kwenye sofa na remote yako angalia matokeo ya manamano,acha wanaume wakapambane,wewe msubiri Kiringo akuletee sharbati
We huna dalili ya kuwa muandamanaji
 
USHAJIULIZA KWANN ANAYECHOCHEA YUPO MAREKANI?
 
Mkuu naona unahanyahanya tu!
 
Aaah
 
Safari moja ina anzisha nyingine
 
Ningekuona wa maana kama ungemshauri uchwara aheshimu katiba aliyo aapa kuilinda
 
Kama kutakua na atakaediriki kuandamana nashauri kusitumike risasi za moto kuwatawanya. Badala yake watumie zana mbadala kama:
[emoji830]Mabomu ya moshi
[emoji830]Paper spray (mace)
[emoji830]Teasers (nyaya za kushitua za umeme)
[emoji830]Maji ya washa washa
[emoji830]Maji ya magari ya zimamoto (water cannons) wenye nguvu
[emoji830]Risasi za mpira - rubber bullets
[emoji830]Mbwa wa polisi
[emoji830]Kelele elekezi - directional sirens (kelele kali za ving'ora zinazoelekezwa kwa waandamanaji tu)

Hivi vitawatia temporary ulemavu lakini hakuna atakaekufa.

AU

Kwa uoga ninaoujua wa waTZ, njia effective ya kuyafanya haya maandamano hata yasianze ni kufanya kama walivyofanya kipindi kile kuelekea UKUTA.

Wiki moja au mbili kabla ya D-DAY, Polisi, FFU, JWTZ, JKT, Mgambo wafanye kwata kwenye viwanja vya michezo, open spaces mitaani, na drills kwenye misitu inayozunguuka makazi.

Nguvu kubwa iwekwe kwenye zile ngome kuu za upinzani. Kama walivyofanya kuelekea hukumu ya Sugu vile.

I can guarantee you watu wataweka makopo ya kukojolea vyumbani mwao ili wasitoke nje usiku.

Just play mind games with them.
 
Tutaona movie live bila ku danload, siku hiyo mm muangalizi wa kimataifa
 
Haya sio maandamano ya chama fulani,ni maanadamano yaliyoandaliwa na watanzania kutoka vyama tafauti vya siasa na visivyo vya siasa,sasa hao uliowataja ni akina nani??!
Watanzania wengi, hasa vijijini hawana smart phones au computers. Hii ina maana hawamo kwenye social media.

Mlitumia platform gani ya kuwataarifu na kupata ridhaa yao kuhusu haya MAPINDUZI?
 
Mbona watu kama wameichoka hii serikali mapema namna hii?
Sio watu. Ni viongozi walafi wa upinzani wanaoona kuwa huko tunakoelekea vyama vya vitakufa, kama havijakufa bado.

Sasa anawashakiza watu waingie mitaani na kuleta vurugu ili nchi isitawalike.
 
Ndiyo shida ya ccm, watakwambia hilo ni jambo dogo haliwasumbui lakini they will lose their shit every second.

Mara huyu alete list ya watu hatari.

Wengine ndiyo mpo humu kuanzisha nyuzi kila siku.

Relax wazee
HAHAAHA AHAA
 
Wabongo bwana, kweli CCM imewafifisha akili! Sasa kwa nini serikali itumie nguvu zote hizi wakati tumeaminishwa kuwa serikali ya awamu hii inapendwa sana kuliko awamu zilizotangulia. Na je hao 'wachache' wasioipenda wakiachwa waandamane na kuongozwa na poilisi ili waeleze wanachotaka kueleza kuna ubaya au hasara gani? Mimi ningekuwa ninamshauri mtukufu asiyejaribiwa, ningesema atoe amri kwa poiliccm kuhakikisha wanatoa ulinzi wa kutosha kwa waandamanaji po pote pale maandamano yanapopangwa kufanyika ili tusikie wanataka serikali ifanye nini. Sijui kwa nini CCm inaogopa mikutano ya hadhara na maandamano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…