NI LIPIBLENGO LA RC MAKONDA NA KAMATI YAKE YA HAMASA KWA TAIFA STARS?

Ufwandunkanye

Senior Member
Jan 7, 2017
123
192
Salaam ndugu zangu.

Kwanza awali ya yote, nimpongeze ndugu yetu RC Paul Makonda kwa kuona kuwa sasa Taifa Stars inahitaji hamasa kufuzu AFCON. Hili ni jambo zuri na la kizalendo ambalo kila mtanzania anainuia mazuri kwa timu yetu. Lakini katika pongezi hii, kuna maswali yakufikirisha.

Kabla ya kuelekea katika maswali hayo, lazima tufahamu kuwa, mpira wetu wa Bongo umeshikamana na siasa ambayo si rahisi kuiona moja kwa moja. Siasa ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kudumaza maendeleo ya vilabu vikubwa nchini- Simba na Yanga.

Pasipo kufikiria sana, siasa yetu, hususani ya Chama Cha Mapinduzi, chama dola, ni sababu kuu ya kutokukua kwa vilabu hivi viwili, na udumavu wake, ndio udumavu wa timu yetu ya Taifa. Zipo sababu nyingi za udumavu, lakini hii ya siasa ni sababu kuu inayotafuna maendeleo ya mpira wetu chini kwa chini.

Miaka ya hivi karibuni, tumeona ni jinsi gani viongozi wa mpira na vilabu hivi vikubwa nchini wakitumia jukwa la mpira kujipatia umaarufu ili wakagombee nafasi kadha wa kadha katika siasa. Na wengi wao wakielekea Chama Cha Mapinduzi. Mifano mitatu tu, naweza kuitoa, najua ipo mingi. Fredrick Mwakalebela, aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la mpira nchini, TFF, aliamua kujitosa kuwania ubunge Iringa mjini kwa tikiti ya CCM. Sasa kuna huyu msemaji wa Simba, Haji Manara, achilia mbali ya kuwa mwanachama hai wa CCM, pia ameonesha nia ya kuutaka ubunge, bado hatujui ni jimbo gani. Si kwamba wamefanya kosa, katiba inawaruhusu. Nitazungumzia ninayoona madhara kwa mpira wetu katika aya zinazofuata.

Mfano wa tatu, na wa mwisho. Ni kutoka kwa Rais wa sasa wa TFF, Wallace Karia. Katika mkutano mkuu wa TFF jijini Arusha, Februari 2, waka huu, Karia alitoa kauli si tu ambayo iliwakera wanachama wa CHADEMA, bali wapenda soka wasio na ufuasi wa vyama vya siasa. Kauli yake ya kutweza, akiwahusisha wanaoisema na kuikosoa TFF kuwa ni 'ma Tundu Lissu'. "Nimesema kama kuna 'ma Tundu Lissu kwenye mpira, na dhani mnaelewa Lissu anahangaika kwenye vyombo vya habari kuikashifu serikali. Na Wambura anazungumza kwenye vyombo vya habari kuikashifu TFF na uongozi wake".

Ukiachana na kauli yake ambayo mtu yoyote aliyekereka na maneno ya Lissu, angeweza kumshutumu kwa kuikosoa serikali. Lakini swali la kujiuliza. Je, ni nani alimtuma Karia kuyaongea hayo na wakati yeye ni kiongozi wa chama cha mpira na si siasa, na wakati huo Lissu alikuwa akishambuliwa kwa maneno kila kona kuwa anakashifu serikali? Je, inamaana TFF ni tawi la serikali? Je, serikali ilimtuma Karia kutumia jukwaa la mpira kwa mabezo ya kisiasa tofauti na kanuni za FIFA? Kwa tulio wengi, siku ile tuliamini kuwa, TFF ni jukwaa lingine la serikali. Nikisema serikali siyo nchi wala Taifa, namaanisha inayoundwa na chama cha siasa, sasa serikali yetu inaundwa na CCM.

Julius Mtatiro, mwaka jana kabla hajatangaza kuhamia CCM, katika ukurasa wake wa Instagram, alibandika maandiko aliyotumiwa kama meseji, japo ameyafuta, ila kwa wale waliokuwa wanamfuatilia watakuwa mashahidi kwa hili. Watu waliomtumia hizo meseji, walitoa lawama kwa namna CCM inavyorudisha mpira wa vilabu vya Simba na Yanga, nyuma kwa kuviingilia kiintelijensia ili kudhibiti kuchukua 'influence' ya kuweza kutishia uwepo wa chama hicho. Walitoa mifano kwa namna Mwalimu Nyerere alivyoweza kuzima kwa haraka 'influence' za vilabu hivi pale alipoona vinataka kuwa ulingo wa vuvugu la kisiasa kwa kupandikiza migogoro kwenye vilabu hivi. Ndio maana migogoro ilikuwa haiishi, leo ukiisha Simba; kesho Yanga. Na migogoro hii imevidumaza vilabu hivi miaka nenda rudi, hadi leo tu havina hata viwanja vya kisasa vya mazoezi, achilia mbali vya mechi licha ya kuwa na mgawo wa mashabiki nchini.

Hata leo unaweza kujiuliza swali dogo tu. Ni nani anayempa jeuri mzee Akilimali kuzua mgogoro pale Yanga? Huyu mzee ana nguvu gani ambayo yanga wameshindwa kuiepuka? Mzee kama huyu, na wengine upande wa Simba kama mzee Kilomoni, wamekuwa vikwazo katika maendeleo ya Vilabu hivi. Nani hasa yupo nyuma yao?

Haya, narudi kwenye mada husika. Ni kuhusu hamasa ya kizalendo kabisa chini ya mwenyekiti wake RC Makonda. Kuna maswali yakujiuliza.

Moja, ni kwanini hii hamasa imekuja wakati huu wakuchelewa ambapo Taifa Stars imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Uganda? Mbona kipindi chote hatukuiona wakati Taifa Stars inacheza hapa nyumbani na inapitia magumu?

Mbili, kila mTanzania anajivunia timu yake. Hamasa iliyopo uwanja wa Taifa ni kubwa sana. Hata bila kuhamasisha watu waende uwanjani, bado wangeenda tu. Je, hamasa hii ya mitandaoni imeenda mbali zaidi? Yaani michango kama alivyofanya Mh Rais kwa kutoa milioni 50 walipokuwa wakienda Lesotho. Kama, ni maneno matupu ya akina Stev Nyerere, basi hamasa ya mashabiki inatosha.

Tatu, Je, hili si jukwaa lingine la kutumia mafanikio ya timu ya taifa(pindi itakapofuzu) kujitafutia umaarufu wa kisiasa? Yaani yarudi kama ya akina Haji Manara na Mwakalebela. Au badala ya kuanza kuogelea mipango na mafanikio ya timu, tuanze kumuongelea mtu, kwamba bila huyu, isingefanikiwa.

Nne na mwisho. Nimesikia kwamba Taifa Stars ikifuzu basi vinywaji ni nusu bei. Je, hii nusu bei ni kwa hiari? Kama si kwa hiari, nani analipia?

Bila shaka sote tunavuja damu nyekundu ya uzalendo. Twende tukaishangilie timu yetu. Mungu ibariki Taifa Stars, Mungu ibariki Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam ndugu zangu.

Kwanza awali ya yote, nimpongeze ndugu yetu RC Paul Makonda kwa kuona kuwa sasa Taifa Stars inahitaji hamasa kufuzu AFCON. Hili ni jambo zuri na la kizalendo ambalo kila mtanzania anainuia mazuri kwa timu yetu. Lakini katika pongezi hii, kuna maswali yakufikirisha.

Kabla ya kuelekea katika maswali hayo, lazima tufahamu kuwa, mpira wetu wa Bongo umeshikamana na siasa ambayo si rahisi kuiona moja kwa moja. Siasa ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kudumaza maendeleo ya vilabu vikubwa nchini- Simba na Yanga.

Pasipo kufikiria sana, siasa yetu, hususani ya Chama Cha Mapinduzi, chama dola, ni sababu kuu ya kutokukua kwa vilabu hivi viwili, na udumavu wake, ndio udumavu wa timu yetu ya Taifa. Zipo sababu nyingi za udumavu, lakini hii ya siasa ni sababu kuu inayotafuna maendeleo ya mpira wetu chini kwa chini.

Miaka ya hivi karibuni, tumeona ni jinsi gani viongozi wa mpira na vilabu hivi vikubwa nchini wakitumia jukwa la mpira kujipatia umaarufu ili wakagombee nafasi kadha wa kadha katika siasa. Na wengi wao wakielekea Chama Cha Mapinduzi. Mifano mitatu tu, naweza kuitoa, najua ipo mingi. Fredrick Mwakalebela, aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la mpira nchini, TFF, aliamua kujitosa kuwania ubunge Iringa mjini kwa tikiti ya CCM. Sasa kuna huyu msemaji wa Simba, Haji Manara, achilia mbali ya kuwa mwanachama hai wa CCM, pia ameonesha nia ya kuutaka ubunge, bado hatujui ni jimbo gani. Si kwamba wamefanya kosa, katiba inawaruhusu. Nitazungumzia ninayoona madhara kwa mpira wetu katika aya zinazofuata.

Mfano wa tatu, na wa mwisho. Ni kutoka kwa Rais wa sasa wa TFF, Wallace Karia. Katika mkutano mkuu wa TFF jijini Arusha, Februari 2, waka huu, Karia alitoa kauli si tu ambayo iliwakera wanachama wa CHADEMA, bali wapenda soka wasio na ufuasi wa vyama vya siasa. Kauli yake ya kutweza, akiwahusisha wanaoisema na kuikosoa TFF kuwa ni 'ma Tundu Lissu'. "Nimesema kama kuna 'ma Tundu Lissu kwenye mpira, na dhani mnaelewa Lissu anahangaika kwenye vyombo vya habari kuikashifu serikali. Na Wambura anazungumza kwenye vyombo vya habari kuikashifu TFF na uongozi wake".

Ukiachana na kauli yake ambayo mtu yoyote aliyekereka na maneno ya Lissu, angeweza kumshutumu kwa kuikosoa serikali. Lakini swali la kujiuliza. Je, ni nani alimtuma Karia kuyaongea hayo na wakati yeye ni kiongozi wa chama cha mpira na si siasa, na wakati huo Lissu alikuwa akishambuliwa kwa maneno kila kona kuwa anakashifu serikali? Je, inamaana TFF ni tawi la serikali? Je, serikali ilimtuma Karia kutumia jukwaa la mpira kwa mabezo ya kisiasa tofauti na kanuni za FIFA? Kwa tulio wengi, siku ile tuliamini kuwa, TFF ni jukwaa lingine la serikali. Nikisema serikali siyo nchi wala Taifa, namaanisha inayoundwa na chama cha siasa, sasa serikali yetu inaundwa na CCM.

Julius Mtatiro, mwaka jana kabla hajatangaza kuhamia CCM, katika ukurasa wake wa Instagram, alibandika maandiko aliyotumiwa kama meseji, japo ameyafuta, ila kwa wale waliokuwa wanamfuatilia watakuwa mashahidi kwa hili. Watu waliomtumia hizo meseji, walitoa lawama kwa namna CCM inavyorudisha mpira wa vilabu vya Simba na Yanga, nyuma kwa kuviingilia kiintelijensia ili kudhibiti kuchukua 'influence' ya kuweza kutishia uwepo wa chama hicho. Walitoa mifano kwa namna Mwalimu Nyerere alivyoweza kuzima kwa haraka 'influence' za vilabu hivi pale alipoona vinataka kuwa ulingo wa vuvugu la kisiasa kwa kupandikiza migogoro kwenye vilabu hivi. Ndio maana migogoro ilikuwa haiishi, leo ukiisha Simba; kesho Yanga. Na migogoro hii imevidumaza vilabu hivi miaka nenda rudi, hadi leo tu havina hata viwanja vya kisasa vya mazoezi, achilia mbali vya mechi licha ya kuwa na mgawo wa mashabi nchini.

Hata leo unaweza kujiuliza swali dogo tu. Ni nani anayempa jeuri mzee Akilimali kuzua mgogoro pale Yanga? Huyu mzee ana nguvu gani ambayo yanga wameshindwa kuiepuka? Mzee kama huyu, na wengine upande wa Simba kama mzee Kilomoni, wamekuwa vikwazo katika maendeleo ya Vilabu hivi. Nani hasa yupo nyuma yao?

Haya, narudi kwenye mada husika. Ni kuhusu hamasa ya kizalendo kabisa chini ya mwenyekiti wake RC Makonda. Kuna maswali yakujiuliza.

Moja, ni kwanini hii hamasa imekuja wakati huu wakuchelewa ambapo Taifa Stars imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Uganda? Mbona kipindi chote hatukuiona wakati Taifa Stars inacheza hapa nyumbani na inapitia magumu?

Mbili, kila mTanzania anajivunia timu yake. Hamasa iliyopo uwanja wa Taifa ni kubwa sana. Hata bila kuhamasisha watu waende uwanjani, bado wangeenda tu. Je, hamasa hii ya mitandaoni imeenda mbali zaidi? Yaani michango kama alivyofanya Mh Rais kwa kutoa milioni 50 walipokuwa wakienda Lesotho. Kama, ni maneno matupu ya akina Stev Nyerere, basi hamasa ya mashabiki inatosha.

Tatu, Je, hili si jukwaa lingine la kutumia mafanikio ya timu ya taifa(pindi itakapofuzu) kujitafutia umaarufu wa kisiasa? Yaani yarudi kama ya akina Haji Manara na Mwakalebela. Au badala ya kuanza kuogelea mipango na mafanikio ya timu, tuanze kumuongelea mtu, kwamba bila huyu, isingefanikiwa.

Nne na mwisho. Nimesikia kwamba Taifa Stars ikifuzu basi vinywaji ni nusu bei. Je, hii nusu bei ni kwa hiari? Kama si kwa hiari, nani analipia?

Bila shaka sote tunavuja damu nyekundu ya uzalendo. Twende tukaishangilie timu yetu. Mungu ibariki Taifa Stars, Mungu ibariki Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app

Asante kwa uchambuzi wako...sina majibu ya swali ulilouliza...nami siku zote najiuliza kwa Nini Kamati imeundwa kwa ajili ya mechi ya mwisho ambayo hata tukishinda kufuzu kwetu kutategemea matokeo ya mechi Kati ya Lesotho na Cape Verde!
Pengone Kamati itaendelea kuwepo siku zijazo na kwa timu zote za taifa (Serengeti boys, Twiga stars, Ngorongo heroes...
 
Back
Top Bottom