Ni lazima kufikiri sana kabla ya kutenda

Mzungu_bahili

Senior Member
Oct 24, 2019
174
420
Wasalam wandugu.Niende moja kwa moja kwenye mada Apo juu. Ilikua siku ya Alhamisi. Nilijiandaa kutoka Dar kwenda Moshi. Saa 12 nilikata tiketi kwenye basi fulani, sikumbuki jina. Lakini tulipofika njia panda ya Mabibo. Basi hilo lilikufa, inaonekana hawakutoa huduma kwake(service).

Tulikaa pale tukisubiri uamuzi wa mwisho. Kwangu nililipa nauli ya basi kupitia tigo pesa. Kwa hivyo wakati abiria wengine walikuwa wakisisitiza kurudishiwa nauli yao. Nilikuwa dilemma coz sikujua la kufanya.

Wengine walirudishiwa nauli zao.Ile kampuni Waliamua kubadilisha Basi, basi la MARANGU likaja pale kwa ajili ya kutufaulisha . Lakini ilibidi niulize abiria wengine walilipa kiasi gani, wengine walisema 30k, wengine 28k lakini kwangu nililipa 36k iliyoandikwa kwenye ticket,.Kuona hivyo Niliamua kurudisha muamala ili nilipe kiasi walicholipa wenzangu.

Hili lilikuwa kosa langu kubwa .Ikabd niongee na Kondakta kuwa nitampa hela yake nasubr muamala urud. Ila pia nilitaka ikishindikan nipige simu nitumie ili nikupe 28k. Ili wakat muamala unarud niwe cjalipa elf 36 Kama mwanzo, Kondakta akasema nitoke ndani ya basi.

Nilichukua mabegi yangu na kutoka nje, Ila nilijiuliza Kwa nini nilirudisha muamala. Niliamua kwenda Mbezi kuangalia kama naweza kupata basi lingine, Lakini safari hii sikuwa na pesa za kutosha kulipa nauli ya basi kwa sababu muamala utarudi ndani ya masaa 12. Niliwapigia simu baadhi ya watu ili kuona kama wanaweza kusaidia lakini hakuna mtu wakat ule aliyeweza kunitumia hela.

Baadae kidogo ndipo nikampigia simu rafiki yang akanisaidia, basi nikapata basi jingine lakini ni basi, basi liliendelea kusubiri kwa takribani masaa 3. Kumbuka nilifika Mbezi saa 3, kwahyo tulikaa mpaka saa Saba kasoro

Somo

1. Ninapaswa kufikiria kwa makini matokeo ya maamuzi yangu.
2. Ikiwa tayari imeshatokea, huna haja ya kuwa na msongo wa mawazo bali tumia muda wako kufikiria nini cha kufanya ili kulitatua.
3. Nahitaji kujali muda kuliko pesa (Sababu kubwa ya tatizo hili)
4. Huna budi kumshukuru Mungu kwa mambo yote, haijalishi ni nini ila wako hai .
5. Pia aliyekusaidia wakat hauna usimsahau.

Prepared by AmArtist
 
Hahaha hapana anayelipa ni mungu pekee, ukitenda wema nenda zako mkuu..
Tuna mtazamo tofauti tu lakn mim mtu ambaye nikiwa na shida akanisaidia, siwez msahau kwa kigezo kwamba Mungu atamlipa. Lazima nimuomyeshe kuwa alichofanya n kikubwa na c kila mtu anaweza kufanya (appreciation). Kuna wengine wanafiki Sana, They acted like they are trying to Help you, kumbe wanafiki tu
 
Tuna mtazamo tofauti tu lakn mim mtu ambaye nikiwa na shida akanisaidia, siwez msahau kwa kigezo kwamba Mungu atamlipa. Lazima nimuomyeshe kuwa alichofanya n kikubwa na c kila mtu anaweza kufanya (appreciation).
Me nimekusaidia kwa moyo sasa ile backup yako yakutaka kulipa fadhila inanifanya nione kama msaada wangu umekua deni kwako....

Na ndio maana binafsi nikikusaidia huwa nakwambia hata asante usinipe ila nenda kawashuhudie watu yale mungu amekutendea
 
Me nimekusaidia kwa moyo sasa ile backup yako yakutaka kulipa fadhila inanifanya nione kama msaada wangu umekua deni kwako....

Na ndio maana binafsi nikikusaidia huwa nakwambia hata asante usinipe ila nenda kawashuhudie watu yale mungu amekutendea
It's true yote kwa yote Lazima uonyeshe shukran. Kama kwenye Bibilia Kuna kipindi yesu aliwaponya watu wengine waliondoka. Ila Kuna mmoja alirud kushukuru kuonyesha appreciation ya alichofanyiwa. Na mm naona ni Jambo zuri . So kwa anayetenda asingoje shukran, lakin anayetendewa asisahau fadhila.
 
It's true yote kwa yote Lazima uonyeshe shukran. Kama kwenye Bibilia Kuna kipindi yesu aliwaponya watu wengine waliondoka. Ila Kuna mmoja alirud kushukuru kuonyesha appreciation ya alichofanyiwa. Na mm naona ni Jambo zuri . So kwa anayetenda asingoje shukran, lakin anayetendewa asisahau fadhila.
Pamoja sana
 
Back
Top Bottom