Ni kweli watu walionywa kabla ya Mkutano na JK?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Nikiwa palepale kwenye mkutano wengine walishangalia na wengine walishangaa na kusema kwamba kumbe ndiyo maana tuliandikiwa mails za kuonyowa na kuambiwa you must behave mbele ya Rais kama utakuja kwenye mkutano wake .Je Es na wengine ambao kama mlipata mails hizo maana mimi sikuipata .Je watu walionywa in advance ku behave ? Ina maana kuacha maswali mazito na walipo kaidigi kijana akaitwa na shahidi ni ES baada ya mkutano na JK .Nisaidieni maana nilisikia wengi wakati wa vinywaji wanasema haya .
 
Ninajua kuwa wananchi hao NY wengi walitumiwa E-mails za kualikwa na kuambiwa kuwa watoe maswali yao in advance na kuyapeleka ubalozini mapema, at least a week before,

sasa kama kawaida yetu wabongo, kuna waliorukia kimbele mbele na kutuma maswali, sasa kilichofanyika ni watu wa JK, kuyakusanya na kuchambua yaliyorudiwa kwa wingi na kuyaita kuwa ndiyo kero ya wananchi wa NY, kwa hiyo hotuba nzima ya rais ilitenngenezwa kwa kutumia maswali hayo, na hii ikampa advantage rais ya kugusa issue muhimu kwa juu juu, halafu yalipokuja maswali kugusa hizo issue akasema kuwa hawezi kurudia tena aliyokwisha yasema,

wananchi wa NY, walipaswa kujibu na kuujibu ubalozi kuwa watauliza maswali pale pale uwanjani sio kutuma kabla kama bungeni, maana hata bungeni kuna maswali ya nyongeza, but psychologically, kuwaambia wananchi watume maswali mapema ilikuwa ni mbinu ya kuwatisha pia na wote mliokuwepo mmeona results,

Yes, kuna kijana aliyeuliza swali la mwisho ambaye aliitwa ndani nakuonana na JK, usoi uso kwani pamoja na mengine kile kitendo cha kumuita Bwana Rais, hakikukubalika, anyway sijui kama kuna waliotishwa as kutishwa kabla ya mkutano!
 
Sasa kwanini Rais yuko tayari kuzungumza na radio zote za wazungu lakini hataki kuzungumza na radio za Watanzania kwa lugha yao na kujibu maswali yao!!!?
 
Bwana Es , maana kwa kawaida unaitwa Mzee Es sasa usije nawe ukaniita pembeni kama ilivyo kuwa kwa rais kubwa bwana anaona ajabu anataka kuitwa Mheshimiwa je angalitwa dry kwa jina la Kikwete ama Jakaya ingalikuwaje ?

Kwa hiyo sasa nakubaliana na mchango wa mtu aliyehoji kwamba JK did not walk out of that meeting as a hero kwa kuwa njama zilitumika kuanzia ofisini kwa Mahiga kuwa hadaa wadanganyika na kutengeneza speech.Kama maswali haya yangaliulizwa pakavu JK angalipiga chini . Hizi si siasa kabisa .Na he was not a hero kwa maana hiyo ya kuchukua maswali na kuandikia hotuba .He is not sincere pia maana watu labda hawagusa rusha naye akakaa kimya , Mikataba , na Elimu .Vitu vyenye matatizo makubwa Nchini alipashwa kuwaeleza wananchi lakini kwenye rushwa na Elimu na Madini hana la kusema maana henchmen wake ama yeye kwa namna moja ama nyingine yumo .

Je kumbe kumwita Bwama Rais ni vibaya lazima uite Mheshimiwa ?
 
Jamani yule kijana aliyeitwa anatoka NJ, kama sikosei anakaa Jersey City, hebu aitwe aje hapa aseme alichoitiwa ndani?, Mzee Murangira hapana ndugu yangu mimi sina noma na jina lolote lile, halafu mimi ni samamki mdogo, ila wakubwa ndio hao wasiotaka kuitwa bwana!
 
Mwanakijiji,

Nadhani itakuwa ni vigumu sana kwa Rais kuzungumza na Radio ambayo host wake anaitwa Mwanakijiiji , Tafadhali mirekebishe kama nimefanya kosa Mwanakijiji sio jina lako halisi !

Tafadhali , tumia jina lako halisi kwenye matangazo yako then utaona tofauti.
 
Kama utarativu ndio huo,basi yapo mawili ama rais hajiamini au wasidizi wake wanajua uwezo wa bosi wao,wakalazimika kumuokoa mapema!
 
Waalikwa kuambiwa wabehave good mbele ya rais sidhani kama ni katika point za kuuliza maswali, ila itakuwa ni trends ambayo may be ipo kwa wabongo kufanya mbwembwe/kujishebedua kusikokuwa na mpango pale wawapo kwenye jumuia kama ile "yaani kijionesha" Tukabaliane kule majuu kuna vijana wengine wa vibosile ambao wapo tuu huko sio kusoma haswa bali just kuspend life! sasa wangeweza kumwaibisha rais mbele ya hadhara kwa vijimambo vyoa!

...........................
:U Can't Change The Nature:
 
Rais au wapambe wake wana tabia ya kuomba maswali kabla ya kufanya mahojiano. Na kama alivyofanya NY alitumia maswali aliyopelekewa kabla kutayarisha mazungumzo yake na Watanzania alipokuwa Washington D.C. mwezi Mei. Nasikia yale maswali alipelekewa na mtangazaji wa VOA na akayatumia kutayarisha aliyoyasema mbele ya Wabongo.
 
Mr. Clean,

Heshima yako mkuu, lakini sio watoto wote wa vibosile ni design maana ni mtoto wa JM aliyemtoa jasho BM, tena kwa maswali very valid kwa taifa!
 
Kama hii ndiyo tabia ya wapambe wake je siku akiingia kwenye maeneo ambayo maswali hayatumwi ila yanauliza kavu kavu ataweza ku walk hero kama ilivyosemwa? Je JK anaweza kukabiliana na Watanzania wajuvi kama Mlalahoi na mimi ambao nasisitiza hapa Songea tuna shida nyingi tangia uhuru?Je siku akikosa maswali in advance na yuko kikaoni watu wakaanza kurusha mavitu JK ataondoka ama atafanyaje ? Wapambe wake najua wengine mnasoma hapa tupeni majibu .
 
mambo hayawezi haribika hata kama Raisi "akitonywa" kuhusu maswali. haiyumkiniki mtu ukawa na swali moja tu la kumuuliza Raisi, na kwamba akilizungumzia katika hotuba basi na wewe ndiyo umeishiwa hoja.

kama Raisi alizungumzia masuala uliyotarajia kumuuliza, bado una nafasi ya kuongeza swali la ziada. tena mchezo unaweza kuwa mtamu kwasababu atalazimika kujibu kwa undani zaidi, akitumia data. na zaidi anaweza hata kujikanganya mwenyewe.

kinachonishangaza mpaka sasa hivi hakuna mtu aliyemuuliza Raisi kuhusu hili suala la Mahakama ya Kadhi. Mgao wa umeme, kwanini serikali inataka kutumia wakala, badala ya kuagiza mitambo yenyewe. Vilevile amechukua hatua gani kupunguza matumizi ya serikali ukizingatia kwamba nchi ina uhaba wa chakula, na umeme.
 
Mzee Mwanakijiji,
Kesho JK anazungumza na wahariri moja kwa moja Ikulu...unaweza kuwahi?!

Kikwete sasa kuzungumza ‘live’ na wahariri

na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete, keshokutwa anatarajiwa kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wake na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini utakaofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini jana na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Maura Mwingira, mazungumzo hayo yataonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa pamoja na kutangazwa na Redio Tanzania.

Rais Kikwete atazungumza ikiwa ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea wa kuhutubia taifa kila mwisho wa mwezi ingawa mwisho wa mwezi uliopita hakuweza kufanya hivyo kwa vile alikuwa ziarani nchini Marekani. Ikulu haikusema ni nini hasa rais anataka kuwaambia wananchi keshokutwa.
 
Wazee,
Kesho tutarajie mada gani wakati JK anaongea na Watanzania kupitia Wahariri?
Mada (huenda na Mpangilio) unaweza kuwa kama ifuatavyo:

UTANGULIZI
Shukrani kwa Vyombo vya Habari kwa kuitikia wito kufika Ikulu, na kwa kuonyesha ushirikiano na serikali katika masuala mbalimbali, ikiwemo suala la kupambana na ujambazi, na suala la kuhamasisha machinga kuhama.

Kuwatakia Waislam mfungo mwema wa mwezi mtukufu.

AJENDA
1. Briefing ya safari ya Cuba (NAM) na Marekani: Kikao cha UN, Vikao vya Kuitangaza Tanzania kwa Wawekezaji (utasikia "ziara imekuwa ya mafanikio sana, nawashangaa sana wale wanaodhani hatufaidiki na ziara hizo"); Pole kwa Msiba wa Watanzania uliotokea wakati huo huo wa ziara.

2. Tanzania kukubali kupeleka wanajeshi Darfur baada ya matakwa yake kutimizwa (Bush katupa pesa na zana??)

3. Uhusiano na Kenya kuingia dosari (utasikia "Siku hizi magazeti ya Kenya yananichora sana! Tena mchoraji mwenyewe ni Mtanzania, mi nashangaa sana!")

4. Utendaji wa Serikali katika miezi 9 tangu iingie madarakani:
* Matatizo ya Umeme
* Bei ya Mafuta
* Kuporomoka kwa Shilingi
* Upitiaji wa Mikataba ya Madini
* Kuangalia upya Uuzaji wa Nyumba za Serikali
* Kuangalia upya Aina na Matumizi ya Magari ya Serikali
* Vita dhidi ya Dawa za Kulevya
* Vita dhidi ya Rushwa
* Suala la Mahakama ya Kadhi

5. Mini-cabinet reshuffle!!!

MASWALI


SHUKRANI ikifuatiwa na COCKTAIL PARTY!!!!
 
Back
Top Bottom