Ni kweli TISS hawafahamiani na hawaaminiani?

Mbona hata members wa jamiiforums ni tiss kwan humu kuna mtu ananijua naitwa nani? nakaa wapi? umri wangu? Watoto wangapi? Wake wa ngap? Kazi yangu? Tupige kifua wana jf tuseme na sisi tiss
 
Kuna wanaojuana, kuna wasiojuana, kuna wanao-wafanyia ujasusi wenzao uku nao wakifanyiwa ujasusi bila kuwajua wanaowafanyia ujasusi, kuna wanaofanyishwa kazi za usalama bila wao kujijua, iwe kwenye siasa, biashara, dini kote wapo majasusi.

Tatizo la ujasusi wa bongo umejikita kwenye kukusanya taarifa zaidi za mambo mbali mbali kusaidia utawala uliopo madarakani tofauti na wenzetu ambao wanajikita sana kwenye kuzuia hatari zote mbaya zizazohusu uchumi na siasa bila kuegemea upande wowote wa kisiasa.

TISS wanatakiwa kujikita kwenye ujasusi wa kiuchumi jinsi ya kutengeneza mabilionea, jinsi ya kupigana vita ya kiuchumi na mataifa jirani, kuhakikisha taarifa za kiujasusi wanazokusanya zinafanyiwa kazi haraka bila kuegemea upande wowote.
.....
 
Back
Top Bottom