Ni kweli Prof Muhongo anahujumiwa?

Ni kweli Prof Muhongo anahujumiwa?

Pamoja na kutupandishia bei ya umeme bado Tanesko imeendelea kupata hasara kubwa mwaka hadi mwaka

Hasara ni lazima ionekane kwa kuwa Tanesco wameanza kuwekeza wenyewe kwenye mitambo ya kufuwa umeme, Kinyerezi I, II, III na IV na wamekopa fedha nyingi sana kwa hayo,

Sasa ulitaka wawekeze halafu hasara isionekane wakati hawajaanza kuzalisha na hiyo mitambo mipya?

Kumbuka, katika uwekezaji mkubwa uliofanywa na Tanesco kipindi cha Mhongo, hata wakianza kuzalisha hasara itajionesha mpaka watakapo fikia hatua ya ku breakeven.
 
Hivi kwa nini tunajitoa ufahamu kwa kuwashutumu wanaompinga Prof, ilhali taasisi za serikali yake, CAG na PCCB wameona amefanya mambo kwa mapungufu makubwa? Je, tunajaribu kuzidharau taasisi hizi na kuona kwamba wabunge ndiyo wa kulaumiwa?

Kuisakama kamati ya PAC juu ya ripoti yao ambayo ilijadiliwa na bunge zima na kuwekewa maazimio ya maridhiano ni kujifanya hatuelewi kabisa kilichotokea, matokeo yake tunajenga visasi kwa mtu mmoja mmoja aliyekuwepo kwenye kamati ile...mtazamo wa aina hii juu ya mambo ya kitaifa unatia shaka sana uwezo wetu wa kuchambua mambo.

Zaidi ya hayo, uwaziri ni political post, kwa sababu hakuiomba kazi hiyo, basi asiondoke kwa kuvunjiwa heshima...tukumbuke kwamba Bunge limependekeza kwa Rais amuwajibishe, na hatua za kisheria ndiyo zitakazoonesha sasa ana makosa gani...akiwa hana hatia si ataendelea kupeta sehemu nyingine? Hivi Kuwa mchapakazi lazima uwe waziri?

Wenzetu tuhuma tu zinatosha kumfanya mtu aachie ngazi, sasa sisi ni vile hatuna mishipa ya aibu au nini hasa? Haya mambo yako wazi, watu tunaamua tu kuendesha mijadala humu kama vile PCCB, CAG, PAC na Bunge vyote vilikosea...kama hatuamini taasisi hizi tumwamini nani?
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Jamani Kadri ya siku zinavyokwenda mbivu na mbichi zinazidi kubainika,hata hili la watu kusema kwa sauti kubwa na mate kuwakauka kwamba huyu waziri Muhongo ajiuzuru huenda tutajua msingi wake,maana nikipima uzito wa lawama na jinsi anavyotuhumiwa nahisi kama kuna shinikizo maana kelele dhidi yake zinazidi hata waliotajwa na akaunt zikatajwa,jaman mie nilikuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba huenda kuna kitu cha kupigwa dhidi ya muhongo sasa naanza kuamini,ila yatafichuka,kama ya Seth nae huyoo sasa ni raia wa Iringa na mtanzania halisi anadai,acha ncheke mie,adui yako muombee njaa tu. wasalaam
 
Kosa lake ni kupinga kumpa Mengi utajiri wa watanzania wote wa mafuta kwa tickt ya uzawa aka uchaga.Mengi
Anaota kuwa Dangote wa mafuta wa bongo hafahamu Nugeria kuna Dangote 10 , masikini million 100, Delta force million 10 na Boko haram million 10
Yeye anachojali awe Dangote wetu tu.
Humkuti kutetea TPDC kutuwakilisha na husikii kuichagiza serikali shirika hilo lipewe nyenzo ili lituwakilishe vixuri kwa manufaa yetu sote....
Muhongo alimkatalia hivyo pesa zikatumika PAC ikafanya kazi kwa niaba ya Dongote Mengi
 
Kosa lake ni kupinga kumpa Mengi utajiri wa watanzania wote wa mafuta kwa tickt ya uzawa aka uchaga.Mengi
Anaota kuwa Dangote wa mafuta wa bongo hafahamu Nugeria kuna Dangote 10 , masikini million 100, Delta force million 10 na Boko haram million 10
Yeye anachojali awe Dangote wetu tu.
Humkuti kutetea TPDC kutuwakilisha na husikii kuichagiza serikali shirika hilo lipewe nyenzo ili lituwakilishe vixuri kwa manufaa yetu sote....
Muhongo alimkatalia hivyo pesa zikatumika PAC ikafanya kazi kwa niaba ya Dongote Mengi

Unataka kutuambia kamati ya bunge imemuonea na imehongwa kwa hilo?
 
Kamati ipi?ile ya PAC chini ya Zitto na Filikunjombe?wanauzalendo gani wale wamehongwa na Mengi mapesa kibao ili tu prof Muhongo na Maswi wafukuzwe,,na pia Lowasa kuwaahidi uwaziri pindi atakapoingia Ikulu na ndo maana wamemu-include PINDA NA PROF TIBAIJUKA ili kupunguza idadi ya wautakao Urais.Ni majizi yameungana kwa interest zao binafsi na uzuri Ikulu ilikwisha libaini hilo mapema,nyie mnapiga kelele serikali yenyewe inaendelea na utekelezaji wa ilani ya CCM 2010/2015
 
Toka Bunge limalize kazi yake juu ya Escrow kumekuwa na mijadala mizito hasa humu Jf huku wengi wakimtetea Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo kwamba anasakamwa na baadhi ya watu wenye maslahi binafsi. Sasa kwa wale mliofanikiwa kusoma vizuri taarifa ya CAG na kupitia ile ya PAC na mjadala wa bungeni. Tuwekeeni makosa ya mh Prof Mhongo na wale mnaoamini hana makosa toeni utetezi. Kama hujaelewa vema suala la Escrow usichangie usichojua. Karibuni wajuzi.

Kwa bahati njema sana kwa taifa letu, mjadala wako unaouitisha hapa jf, umepitwa na wakati (Overtaken by events), mjadala huu hapa Jf, with due respect to the forum, hauwezi kurudisha saa nyuma,(can not turn back the tide!); it is pure political satire for all intents and purposes; hata kama kuna "tuhuma za udhaifu" dhidi ya JK! I believe the man is intellectually and morally very present kwa kiwango cha kutopenda kuona a repeat of the events of yesterweek!! Nonetheless, nisimkanie mtu, itoshe tu kusema kwamba ni maazimio ya Bunge pekee yatakayozingatiwa katika maamuzi ya JK na sio hii weired push and shove bantter hapa JF. I rest my case.
 
Kosa kubwa la Muhongo ambalo kwangu mie naweza kusema MDOMO wa MUHONGO ndio ULIOJENGA HASIRA NA UKAKASI WA UMMA DHIDI YA ESCROW.

Waswahili walishesema MDOMO ULIPONZA KICHWA...Kauli za KUBEZA NA MAJIBU YA DHARAU YA MUHONGO dhidi ya Wabunge mbalimbali kwenye vikao vya Bunge vilivyopita kabla ya kikao cha 16/17 ndio kulipelekea Hisia za Baadhi ya Wabunge Na Wanachi kuvutwa na kupata hisia za Wananchi kujua kulikoni majibu ya KUBEZA NA UJIVUNI wa Pro Muhongo.

Kwa Wasomi walio wengi watakubaliana nami ukweli kuna Academic Bull ndani ya Taaluma hizi mbili GEORGY na ELECTRIC NA ELECTRONICS hasa hapa Nchini kwetu. Kuna baadhi ya watoto wa Wakulima Waliokwenda Kusoma Kada hiyo ya Masomo hayo Geology na Electric hasa hapa kwetu Kitaaluma waligeuka na kuwa ni watu wenye majivuno sana kwenye Facultys zao kuwa wao ndio wasomi bora Duniani na kuunda dharau kwenye Kada zingine za Kitaaluma kama Education, Sociology na masomo mengine.Dharau hizo kwa baadhi ambao hawakustaarabika imeendelea mpaka kwenye maisha yao ya kila siku.

Kama kuna Watanzania wamebahatisha kufanya kazi na baadhi ya Wajiolojia wa Kitanzania watatwambia tabia za baadhi ya Wajiolojia wetu ni zile za dharau sana na majibezo ya hali ya juu sana...Nilichojifunza Walimu wao pia kumbe wamechangia sana kuwajenga wanafunzi wao kuwa na SUPER EGO HIZO.

Kwa tabia ya Pro Muhongo ambayo aliionyesha kwenye vipindi vya awali vilivyopelekea hisia za udadisi ambao ulipepelekea kuibua NATIONAL INTEREST.Na ukiongeza Tabia za Kikabila ambazo ndugu yetu pia anazo kinasaba basi mchanganyiko huo ulipelekea kutengeneza iki tunachokiona leo.

Muhongo hakujua wapi azungumze nini,ili kutengeneza POLTICAL ATMOSPHERE NJEMA juu ya jambo hili kwenye UMMA.Mazungumzo yake yalijaa Maringo ya Kitaaluma na nasaba ya Kikabila.Nikisema Nasaba ya Kikabila nieleweke Wakurya na Wanyaturu ni wakali na wenye misimamo mikali sana sana unaweza kuona ilo kwa TINDU LISSU -MNYATULU, na AG-MKURYA.

Wajita ni wenye majivuno sana kama alivyo yeye Pro Muhongo.Wasukuma ni wapole sana lakini wenye Jeuri Kali sana kama alivyo AG wa zamani ENDREW CHENGE.Hivyo hizi kabila nazo zinatengeneza nasaba zenye haiba ya aina fulani fulani fulani kwenye jamii zetu.Nani asiye jua tabia ya ndugu zetu Wahaya toka Bukoba au Wazaramo wa Pwani!!!

Sasa unapokuwa na Kiongozi ambae AJAJITAMBUA na anataka kuongoza bila kujifunza jinsi ya kuwasilina na Watanzania wenzake basi anatatizo kubwa tena la msingi na anaitaji Shule je Taifa lina muda wa kumfundisha Mtu mzima Kama Muhongo juu ya Kuwasiloian na Umma No Sidhani muda hup upo.

Ili la kumsema Mzee Mengi binafsi naliona na ESCAPING GOAT, manake Mzee Mengi kuwa nae tofauti kimtazamo sio ndio tiketi ya yeye kumwandama, lakini ni fursa pia ya kuona kuwa kama umemuona Waziri ni tatizo kwenye UCHUMI wa TAIFA lakE basi ni haki yake kwa Mzee Mengi kuwajibika na kujipambanua dhidi yake hata ikibidi kwenda kinyume na mapenzi ya Waziri.

Inawezekana vipi Waziri ukauza viwanja vya madini ya Watanzania kwenye mtandanao [Online] ili Mtanzania anunue kwa mnada na wageni toka nje.Kwanini usifilikilie utaratibu mzuri wa kuwapa wazawa Viwanja hivyo ili Mgeni [Mwekezaji] akija akutane na mzawa...ni kwa style hiyo mzawa anapata fursa ya kuwa EMPOWERED NA TAIFA lake kwa kuwa akija mwekezaji na CAPITAL YAKE huyu raia wa Tanzania [citizen] yeye anakuwa na ARDHI YENYE MADINI ambayo mwekezaji anainvest CAPITAL mwenyeji anainvest Land ndio unakuwa mtaji wake, tayari mtanzania huyu anakuwa amepiga hatua ya juu na kwa sekta ya madini atatoa ajira na kuvuna Technolojia.

NENDA EMIRATES ndio wanavyofanya kwa raia wao. MUEMIRATES yeye Serikali yake ndio inamtanguliza mbele na Mwekezaji anamsikiliza raia wa EMIRATES.Leo raia huyo kama akisema amtaki mwekezaji Partner wake Nchi yake EMIRATES wanamwondoa mara moja.Sisi Leo Pro Muhongo anamwambia RAIA ashindane na Mzungu mwenye DOLLAR kununua viwanja vya madini,kweli NMB BANK YA TANZANIA inaweza kwenda kufungua TAWI LA BANK New York Marekani?, hayo si maneno yangu ni maneno ya Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere.

Hivyo swala la Mzee Mengi halina nguvu kwa wenye ufahamu kilichojitokeza Mzee Mengi alimwangilia Pro Muhongo KUMPIGANIA Mtanzania Muhongo alimwangalia KUMTETEA Mwekezaji....Tatizo labda Mzee Mengi anamindset ya Kibishara kumkomboa Mtanzania ambayo Pro Mhuhongo Sivyo.Busara ilikuwa ni Pro Muhongo alipaswa kuitumia Mindset Ya Mzee Mengi matokeo yake Yeye akamsukuma mbali, tena kwa matusi na masimango mazito na kukumbatia Mindset ya Theory ambazo HAZIISAIDII NCHI NA WATU WAKE bali kuwaongezea UMASKINI KWA MTAJI WA MALIASILI ZAO KWENDA KWA WAGENI.Sasa akiwekwa kwenye kona na Wananchi kwa jambo lile lile ambalo Mzee Mengi alikuwa ANAMUONYA NALO LAWAMA TENA ZIENDE KWA MZEE MENGI.

Na hakika hapa Mzee Mengi alisimama upande wake kuwawezesha Watanzania, yeye Pro Muhongo aliangalia kuwapa wageni Maliasili zetu za Madini.Hivyo lilipokuja la kutokea Mzee Mengi akawa MSHINDI.
 
Back
Top Bottom