ukisoma hapa itakuongezea marifa zaidi.
[h=2]Ukiondoa sababu ya kutoelewana na Reginald Mengi, sijaona sababu ya Prof. Muhongo kung'oka[/h]
Wana jamvi, ni matumaini yangu kuwa bado mnaendelea kutafakari mapendekezo hovyo ya Kamati ya PAC yaliyozaa maazimio hovyo ya Bunge juu ya sakata la Akaunti ya ESCROW. Mjadala mkubwa hapa JF kwa sasa ni juu ya sababu ya msingi ya kuondolewa kwa baadhi ya mawaziri kwa kuhusika kwao na sakata la ESCROW achilia mbali utata uliogubika mwenendo mzima wa uchunguzi wake. Ni bahati mbaya sana Ripoti ya CAG haikuainisha makosa ya msingi ya kuondolewa kwa Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo au hata Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi. Hakika hawa jamaa nawaadimire sana kwenye kazi zao. Wameleta displine kwa shirika la umeme na wamevuruga sana miradi ya kifisadi ambayo ilikuwa inapoteza mapato mengi sana ya TANESCO.
Wadau, kuna msemo usemao kuwa mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Ni aibu kwa kamati ya PAC kupendekeza waziri na Katibu Mkuu wa Nishati na Madini wang'oke kwa sababu zisizoeleweka. Eti wanasema kuwa Waziri anaondolewa kwa kusema kwake uongo bungeni. Haya tuambieni, kauli aliyotoa Muhongo ni ile ile aliyotoa Waziri Mkuu Pinda kuwa fedha zile si mali ya serikali wala TANESCO bali ni mali ya IPTL. Pia Naibu Waziri Stephen Maselle alitoa kauli hiyo hiyo ambayo ilitokana na ruling ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Werema. Sasa hapo kosa la Muhongo na Maswi lipo wapi?
Sababu ya pili iliyoainishwa na akina Zitto eti ndo sababu ya Waziri Msomi tena aliyeliletea manufaa makubwa shirika na wizara kwa ujumla wanasema ni kuwa dalali. Eti kwa vile wamiliki wa IPTL na wa PAP walikutana ofisini kwake. Hakika inashangaza sana. Yaani waziri na Katibu Mkuu hawaruhusiwi kukutana na wawekezaji wawe fake au halali? Nani anatambua kuwa mwekezaji fulani ni fake au halali? Hakika inachelesha sana. Nimefuatilia mijadala juu ya sababu ya kuondolewa kwa Viongozi hawa hakika kila mmoja anajikanyaga.
Jamani ifike wakati tuwe wakweli kusema ukweli. Wengi waliopiga kelele ili Maswi na Muhongo waondoke ni wale wale ama waliwahi kukwaruzana hapo nyuma kama ilivyo kwa Ole Sendeka dhidi ya Muhongo, au Kafulila dhidi ya Maswi. Usitegemee kuwa hawa wabunge watakuwa mabalozi wa mahasimu wao.
Wengine wanaopiga kelele ni wale waliotajwa kula mlungula kutoka kwa Reginald Mengi. Tena hawa walikuwa wanaongea kwa jazba kubwa utafikiri wana uchungu kumbe wanatetea rushwa waliyokula. Binafsi hii ndo naona sababu ya msingi ya Muhongo na Maswi kuondolewa. Rushwa rushwa rushwa. Mbowe ananuka rushwa. Zitto ananuka rushwa. Kafulila ananuka rushwa. Mbatia ananuka rushwa. Mnyika ananuka rushwa. Ole sendeka ananuka rushwa. Serukamba ananuka rushwa nk nk. Ndo maana Spika wa Bunge amekemea sana wabunge kupewa fedha kutoka kwa wafanyabiashara ili wawasulubu Mawaziri. Hii ndiyo sababu ya msingi.