Ni kweli Nelson Mandela alifia gerezani 1985?

Utoto raha sana. Mnakaa mnasimuliana stories za kitoto. Inasemekana,inasemekana nyingi. But hata kutumia tu common sense hamtaki. Ujinga tu wa hovyo hovyo
 
Inawezekana mana inasemekana kuwa Wakristo ndio hao hao walioanzisha imani na dini ya kiislamu. Kama hilo limewezekana bas possibly hata iyo conspiracy kwa mzee Madiba was possible!
 
Bahati mbaya sana kizazi hiki kumekuwa na maarifa mengi sana , huku ukweli unaweza kuwa uongo na uongo ukawa ukweli
 
Wazungu walitupa elimu ili tujitambue na watutawale kwa njia rahisi, walifanya makusudi, kwann nchi nyingi za Africa zilianza kupata uhuru miaka ya 1960'
 
Habari zenu wadau, katika pitapita zangu nimekutana na mwandishi mmoja anayedai kuwa mtu anayefahamika kwa jina la Nelson Mandela, si huyu tunaye mfahamu sisi, Nelson original alifia jela mwaka 1985. Kwa mujibu wa maelezo yake nikwamba huyu tunaye mfahamu alitafutwa mtu anayeendana naye kidogo na alilazimishwa kutoa talaka kwa Winnie Mandela maana wangekaa pamoja kwa muda mwanamama huyu angejua kuwa hakuwa Mandela Original.

Inasemekana mwanamuziki Johnny Clegg alishawahi pia kuimba kitu hiki katika wimbo wake wa "Asimbonanga" yaani hatujamwona yeye. Kwenye wimbo huo kuna maneno Asimbonang' uMandela thina akimaanisha hatujamwona Mandela Laph'ekhona - mahali alipo Laph'ehleli - mahali alipo zikwa. Wimbo huu ulitoka mwaka 1987.

Nani aliyetolewa gerezani 1990?

Inasemekana ni mtu ajulikanaye kwa jina la Gibson Makanda ambaye alipelekwa katika gereza la Pollsmor mwezi May mwaka 1985 na akiwa huko alifanyiwa plastic surgery iliyofanywa na timu ya madaktari wachache toka London Uingereza, mara baada ya zoezi hilo kufanikiwa alipatiwa mazoezi ya kuongea na kutembea kama Nelson Mandela mpaka alipo fuzu ndipo mpango wa kumtoa ukatekelezwa ndomaana hata baada yakutoka alilegeza sana masharti kwa watu weupe.

Nilipitia pia vyanzo mbalimbali mtandaoni nikakutana na zaidi ya waandishi 50 tofauti wakizungumzia juu ya Gibson Makanda kuigiza kama Nelson Mandela.

Je, nikweli Nelson Mandela alifariki mwaka 1985?

Acheni utoto.
Wengine tumemwona Mandela na Winnie kwa macho yetu alipotutembelea hapa Dar 1990.
 
Kuna mdau alishawahi kusema hivyo, ila inawezekana alifanyiwa "Brain washing". Ila inawezekana pia. Tatizo mambo mengi yanafichwa sana yaani
 
Teknolojia inayohusu kumzuia Winnie tu asigundue kuwa kuna Nelson Mandela fake lakini wote aliosoma nao, aliofungwa nao, aliofanyanao kazi, dada zake, watoto wake etc isiwaguse? Dhana hiyo ni zaidi ya wehu.
Kama sehemu za Siri aliezifahamu alikuwa Winnie tu hao wengine mwisho wao nje tu. Kama ndivyo basi ilikuwa sawa kumtaliki Winnie mapema sana
 
Hili jambo ni fikirishi sana kwasababu misimamo na hoja aliyokuwa nayo Mandela wa kabla ya kufungwa na baada ya kutoka gerezani ni tofauti kabisa.

Pia swala la kumtaliki Winnie kwa hoja dhaifu aliyoitoa Mandela nayo ina ukakasi. Si Mandela yule aliyehamasisha umoja wa kitaifa na maridhiano kati ya makabira ya wanakusini katika kupambana na mkaburu kutoa taraka kwa Winnie bila ya kusikiliza ushauri kutoka kwa wazee na marafiki zake wa karibu.
Mambo ya ndoa hayako kama unavyofikiri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom