Wajameni tuache ushabiki for the sake of ushabiki, kwa maoni yangu, Clouds wanafanya kazi mzuri ya kuipa jamii kile ilichokosa, japo nakubaliana na dhana nzima ya profesionalism kwenye kazi yoyote, utangazaji ni kipaji, sio elimu, watangazaji wazuri wote wa iliyokuwa RTD wengi wote walikuwa maForm Four Levers wenye pass za chini ambao hawakuweza kwenda form 5. Wale waliosoma RTD walipolekwa newsroom, huko ndiko profesionalism ya media inaaply, watangazaji kazi yao ilikuwa ni kubwabwaja, hata wasoma habari kazi yao ilikuwa ni kusoma tuu kitu walichoandikiwa na vichwa vya newsroom.
Kuwa mtangazaji mzuri, huhitaji kuwa kichwa, unahitaji kipaji tuu na moral standards kuwa hiki niseme, au hiki nisiseme, hivyo naombeni hoja ya elimu ya watangazaji wa Clouds tuondoe.
Kwa vile sasa tumeendelea zaidi, kazi ya utangazaji sio kubwabwaja tuu, ni pamoja na kufanya analysis na coments, hivyo kunahitajika just general knowledge ya mambo ya kawaida ambayo kwa kweli hii Clouds hawana.
Nimesema Clouds ni redio nzuri kwa sababu inawapatia watu kile walichokosa, miaka ya nyuma nikiwa mtaani, nikadhani magazeti ya udaku ni kwa ajili ya watu wa chini, mastandard 7 levers na wale watu wa uswahilini. Nilipojoin UDSM, nilidhani magazeti hayo hayawezi kuwa na soko sehemu ya wasomi kama Mlimani!, to my surprise ndio magazeti yanayonunuliwa sana na wanafunzi wa Chuo kuliko magazeti mengine yoyote, na huisha mapema zaidi wakati magazeti mengine kibao, hudoda! (japa sababu inaweza kuwa ni bei poa, wakati huo yakiuzwa Sh.100).
Ndivyo ilivyo Clouds Radio, ni radio ya vijana, mambo ya udaku udaku and such sort, wamejikuta kumbe kuna sehemu kubwa ya jamii hiki ndicho wanachokitaka, hivyo hawahitaji watangazaji wasomi na bado wasikilizaji ni kibao.
Kipindi cha Jahazi, cha Gadner na Kibonde, ndicho kipindi kinachosikilizwa kupita kipindi kingine chochote wakati huo, Clouds wanalijua hili, na Gadner na Kibonde pia wanalijua, matokeo yake sasa wamevimba vichwa mpaka wanaharibu. Mimi ni msikilizaji wao mzuri na ninaendelea kuwasikiliza japo huwa nakereka.
Siku walipoishukia JF, pia niliwasikiliza, kusema ukweli pamoja na vipaji vyao vya hali ya juu, wanabwabwaja kupindukia, hali inayopelekea kuvuka mipaka na hata kutumia lugha isiyofaa( Kibonde), kwa sababu amesifiwa amevimba kichwa, hivyo amejiweka juu na kuwaunder estimate wasikilizaji wake, kuwa mtangazaji ndio zaidi. Hii inapelekea wenye akili zao kuwaona they are just fools fulani wanafurahisha genge. Kibonde ni MC, lugha zake nyingi za utani na uwezo wa kuigiza sauti za watu mbalimbali, unakipa kipindi hicho ladha ya pekee na vionjo adimu, Gadner alionekana kama modarator akimdhibiti Kibonde asipitilize, lakini sasa lao limekuwa moja ndio kwanza Gadner anamchochea Kibonde kuzidi kumwaga upupu.
Mimi yangu macho na masikio, ngoma ikilia sana mwishowe hupasuka, nawathibitishia wana JF, hii ngoma ya Jahazi, sasa yalia sana, inakaribia kupasuka!.