Kuna tetesi eti maghorofa yanayomilikiwa na shirika la reli la Tanzania na Zambia yameuzwa kwa Oil Com. Wafanyakazi waliokuwa wakiishi kwenye maghorofa haya wametakiwa kuhama kuwapisha watu wa Oil Com. Uuzaji huo umefanyika bila kuishirikisha nchi ya Zambia. Makabidhiano bado. Upande wa Zambia haujatoa hati. Mwenye taarifa atujuze.
Naweka rekodi sawa. Kilichotokea Ni kuwa TAZARA iliwauzia wafanyakazi wa tazara. Zoezi hili lilianza takriban miaka 10 iliyopita. Wafanyakazi wa tazara wakaanza kuziuza na watu tofauti walizinunua akiwemo oilcom. Ikaja kufahamika kuwa oilcom ananunua kwa bei nzuri. Hivyo wafanyakazi wengi wakaziuza kwake. Mfano nyumba ya chumba 1, jiko na choo Ni mil 45 kwa oilcom. Na ya vyumba 2 bei Ni mara mbili yake.
Magorofa hayo yameuzwa kwa sh 2 million kwa top mgt tena kwa kukatana kidogo kidogo sana, kila boss akapata lake.
Kilichofata ni kuyauza kwa oilcom kipamoja, shida hapa ni hati ambazo zipo zambia kwenye hazina kuu.
Ngoja tusubiri?