Ni kweli maghorofa ya TAZARA Chang'ombe vetenary yameuzwa?

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
0
Kuna tetesi eti maghorofa yanayomilikiwa na shirika la reli la Tanzania na Zambia yameuzwa kwa Oil Com. Wafanyakazi waliokuwa wakiishi kwenye maghorofa haya wametakiwa kuhama kuwapisha watu wa Oil Com. Uuzaji huo umefanyika bila kuishirikisha nchi ya Zambia. Makabidhiano bado. Upande wa Zambia haujatoa hati. Mwenye taarifa atujuze.

Naweka rekodi sawa. Kilichotokea Ni kuwa TAZARA iliwauzia wafanyakazi wa tazara. Zoezi hili lilianza takriban miaka 10 iliyopita. Wafanyakazi wa tazara wakaanza kuziuza na watu tofauti walizinunua akiwemo oilcom. Ikaja kufahamika kuwa oilcom ananunua kwa bei nzuri. Hivyo wafanyakazi wengi wakaziuza kwake. Mfano nyumba ya chumba 1, jiko na choo Ni mil 45 kwa oilcom. Na ya vyumba 2 bei Ni mara mbili yake.

Magorofa hayo yameuzwa kwa sh 2 million kwa top mgt tena kwa kukatana kidogo kidogo sana, kila boss akapata lake.

Kilichofata ni kuyauza kwa oilcom kipamoja, shida hapa ni hati ambazo zipo zambia kwenye hazina kuu.

Ngoja tusubiri?
 

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,517
2,000
hii itakuwa sio habari njema kwa wananchi hata kidogo,kama tazara walishindwa,tunayo mifuko na mashirika yangeyoweza kuzikarabati au kujenga upya lile eneo,sio oil com,wananchi wanahitaji maeneo pia ya kuishi lazima tunapofanya mahamuzi tufikirie maslahi ya wengi,oil com amtafute alompa hela zake amrudishie kama ni kweli,tuna nnsf,nhc tutawapa maeneo hayo wstujengee nyumba za bei rahisi za kisasa ntahakikisha rais anaporudi toka mapumzikon na kumteua mtu wa kwenda kuvaa viatu vilivyovuliwa na prof tibauijuka,rais aniteue mimi naapa baada ya uteuzi wangu ntarirudisha eneo hilo mikononi mwenu watanganyika.INAKATISHA TAMAA KUONA WAKUBWA MNYOMEGEANA KEKI HII (RASILIMALI ZA TAIFA) KWA FUJO
 

hekagongoo

Member
Apr 10, 2014
80
95
Hio habar haina utata ya kwel na baadhi ya eneo ambalo kulikuwa na nyumba ya kawaida walisha bomoa natayari washajenga yaadi
 

dostum

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
215
225
Naweka rekodi sawa. Kilichotokes Ni kuwa tazara ilieauzia wafanyakazi wa tazara. Zoezi hili lilianz takriban miaka 10 iliyopita. Wafanyakazi wa tazara wakaanza kuziuza na watu tofauti walizinunua akiwemo oilcom. Ikaja kufahamika kuwa oilcom ananunua kwa bei nzuri. Hivyo eafanyakazi wengi walaziuza kwake. Mmfano nyumba ya chumba 1, jiko na choo Ni mil 45 kwa oilcom. Na ya vyumba 2 bei Ni mara mbili yake.
 

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,100
1,195
Kuna tetesi eti maghorofa yanayomilikiwa na shirika la reli la Tanzania na Zambia yameuzwa kwa Oil Com.Wafanyakazi waliokuwa wakiishi kwenye maghorofa haya wametakiwa kuhama kuwapisha watu wa Oil Com.Uuzaji huo umefanyika bila kuishirikisha nchi ya Zambia.Makabidhiano bado.Upande wa Zambia haujatoa hati.Mwenye taarifa atujuze.

Magorofa hayo yameuzwa kwa sh 2 million kwa top mgt tena kwa kukatana kidogo kidogo sana, kila boss akapata lake.

Kilichofata ni kuyauza kwa oilcom kipamoja, shida hapa ni hati ambazo zipo zambia kwenye hazina kuu.

Ngoja tusubiri?
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
107,135
2,000
Wakwapuzi washafanya yao chini ya carpet....Dah!!!! Mafisadi hawana huruma hata chembe kwa Watanzania.
 

shabani ponera

Senior Member
Oct 15, 2014
158
195
Wakwapuzi washafanya yao chini ya carpet....Dah!!!! Mafisadi hawana huruma hata chembe kwa Watanzania.

tazara waliwauzia nyumba wafanyakazi na wafanyakazi wameziuza, tatizo liko wapi hapo? kama imefanyika kinyume na hivyo labda kunaweza kuwa na tatizo
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
107,135
2,000
Ngoja tupate more details kuhusu hili. Isije kuwa linafana na lile sakata la kuuza nyumba za Serikali lililofanywa na mafisadi Mkapa na Magufuli.

tazara waliwauzia nyumba wafanyakazi na wafanyakazi wameziuza, tatizo liko wapi hapo? kama imefanyika kinyume na hivyo labda kunaweza kuwa na tatizo
 

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,962
2,000
Watu tunasahau kuna eneo lingine sehemu hizo la TAZARA kuelekea Sokota lilikuwa wazi Azam kajenga siku nyingi!
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,478
2,000
hii itakuwa sio habari njema kwa wananchi hata kidogo,kama tazara walishindwa,tunayo mifuko na mashirika yangeyoweza kuzikarabati au kujenga upya lile eneo,sio oil com,wananchi wanahitaji maeneo pia ya kuishi lazima tunapofanya mahamuzi tufikirie maslahi ya wengi,oil com amtafute alompa hela zake amrudishie kama ni kweli,tuna nnsf,nhc tutawapa maeneo hayo wstujengee nyumba za bei rahisi za kisasa ntahakikisha rais anaporudi toka mapumzikon na kumteua mtu wa kwenda kuvaa viatu vilivyovuliwa na prof tibauijuka,rais aniteue mimi naapa baada ya uteuzi wangu ntarirudisha eneo hilo mikononi mwenu watanganyika.INAKATISHA TAMAA KUONA WAKUBWA MNYOMEGEANA KEKI HII (RASILIMALI ZA TAIFA) KWA FUJO

Kwani lazima uwe Waziri ndipo uwe na uwezo wa kuondosha au kurejesha? Mbona Mtikila hana madaraka yoyote nchini lakini anaenda mahakamani tu na haki za wananchi zinapatikana... wacha utegemezi wewe.... Kama kwenye soccer unasubiri uletewe mpira karibu na goli tu ufunge...
 

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,100
1,195
tazara waliwauzia nyumba wafanyakazi na wafanyakazi wameziuza, tatizo liko wapi hapo? kama imefanyika kinyume na hivyo labda kunaweza kuwa na tatizo

Wee nawe sijui ni mweu, hivi gorofa moja ni sh 2 million kweli, na mtu anakatwa sh 50,000 kwenye mshahara wake unasema sawa, ungekuwa karibu kibao cha tumbo ungekula.

Baada ya wafanyakazi wachini kipiga kelele, wakapozwa nawao kwakuuziwa vikota kila station sh laki sita chumba, sebure, jiko na choo bila hata hati ya nyumba, kiufupi ni use.nge tu.

cc. mbeyaman BAK
 
Last edited by a moderator:

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,361
2,000
mbeyaman
[h=2]Dr H Mwakyembe hii inakuhusu! Ukiisikia ifanyie kazi kiongozi wetu mpambanaji[/h]
Nimemtaja Mh Mwakyembe nikiwa na maswali na hoja ambazo zimejikita kwa shirika lililopo chini ya wizara anayoiongoza ya uchukuzi,ninaongelea the "sleeping giant- TAZARA"

Nikiwa mmoja wa wakereketwa wa uuzaji wa mali za serikali na mashirika ya Umma na hasa nyumba.Sote tunatambua wazi kuwa Mahospitali,Mashule,Polisi,Maj eshi,Reli na Bandari zzilivyo na umuhimu kwa watumishi wake kuwa na makazi jirani na sehemu zao za kazi ili kurahisisha uutendaji wao na kuongeza ufanisi.uuzaji wa nyumba husika unanikwaza kwani ni mali ya UMMA na inakuwaje anayeishi humo a-qualify kupata haki hiyo na kupoteza haki za watanzania wengine ambao kimsingi wote ni wamiliki wa mali hizo?

Kadhia nyingine ya kustaajabisha ni pale kwa mfano shirika la reli kumuuzia nyumba dereva wa treni anayestaafu,je dereva mpya atakayeajiriwa atakaa wapi? Na kwa mshahara mdogo wa kuanzia na ughali wa nyumba za Mjini si ndo mwanzo wa yeye kwenda kupanga nje ya mji kwenye unafuu wa kodi na kwa foleni za Dar ikamuathiri kuwahi kwake kituo cha kazi na kuathiri safari ya treni na watumiaji wengine?

Sasa niulize
· Shirika la Tazara ni mali ya nani?
· Mkopo wa kujenga reli hiyo kutoka jamhuri ya watu wa China lilishalipwa?
· Chombo gani hutoa maamuzi ya uuzwaji mali za shirika?
· Mali zikiuzwa fedha hupelekwa mfuko gani na hutumika vipi?
· Mfumo wa kurejesha nyumba wizarani then TBA kupangiwa matumizi au mauzo hauihusu Tazara?

Nyumba za Tazara za Maganga Estate zilizopo jirani na makao makuu ya shirika hilo mkabala na wizara ya kilimo maarufu kama Veternary zimeuzwa kwa wafanyakazi wanaoishi humo na wasioishi humo kwa bei chee ya kuanzia 1m to around 2m tena kwa mkopo wa kulipa kwa kukatwa mishahara.Nao pia wameziuza kwa mfanyabiashara mwenye asili ya kiarabu kwa bei kubwa zinazofikia hadi 70m kwa apartment moja na lengo kuu ikiwa ni kuzigeuza kuwa za kibiashara.Tayari nyumba ndogo za kota walizokuwa wakikaa askari polisi wa Tazara zimeshazungushiwa uzio ili zibomolewe na eneo litumike kuhifadhia makontena yaani Inland Container Depot(ICD).

Sasa niendelee
· Je mtumishi wa umma anapouziwa nyumba hutakiwa asiiuze wala kubadili matumizi baada ya muda gani?
· Ukiuziwa apartment moja iliyopo ghorofani umiliki wa kiwanja cha ghorofa lenye apartment kadhaa unakuwa wa nani?
· Askari polisi waliokuwa wakikaa nyumba za kota wamepewa makazi mengine?
· Kibali cha kubadili maeneo ya makazi kuwa ya kibiashara hutolewa wapi?
· Jiji la Dar lenye utitiri wa ICD's zipatazo 17 tunataka kuuruhusu uwe na msongamano zaidi wa ICD zingine kwenye makazi?
· Ukiacha uuzwaji nyumba kuna eneo linalozunguka nyumba hizo,je utaratibu upi ulifuatwa wenye uwazi na kutoa fursa kwa watanzania wengine kununua uliotumika kuliuza?

Sote tunafahamu ustawi wa Bandari ni inlets na outlets zake.outlet kuu ikiwa ni reli .sasa kwa ubomoaji huu wa shirika serikali ina matumaini gani ya kufufua reli hii ambayo ni muhimili mkubwa wa kibiashara kati ya TZ na Zambia na DRC hasa kwa kipindi hiki ambacho dhahiri tunatakiwa tuimarishe uhusiano na matajiri wenzetu DRC na Zambia na kuondokana na EAC ya akina KKK?(Kaguta,Kenyatta,Kagame)

Usafirishaji mizigo kwa njia ya treni ni haraka,rahisi na salama zaidi.safari moja ya treni inaweza kuwa ni sawa na safari ya malori zaidi ya 100.hivi kweli serikali inaishia kupata port charges ndogondogo na kuachia mizigo isafirishwe kwa gharama kubwa kwenda nchi jirani wakati reli ipo?

Tukiimarisha usafiri wa treni kwa mizigo tutajiokoa na mengi

1. Tutapunguza idadi ya ajali zinazosababishwa na malori haya ambayo mengi ni second hand na chakavu
2. Tutapunguza uharibifu wa barabara na kupunguza gharama kubwa za matengenezo ya barabara yanayogharimu fedha nyingi
3. Tutapunguza misongamano na adha kwa watumiaji wengine wa barabara.mifano hai ni kama kero ya mizani ya kibaha ama boda ya Tunduma
4. Hata kasi ya ukimwi katika njia kuu yapitayo malori haya itapungua
5. Tutaongeza trust ya wateja kusafirishiwa mizigo yao hasa baada ya wimbi la wizi wa mizigo njiani katika malori kuongezeka

Mheshimiwa,waswahili wanasema kiroho safi hivi ni kweli hamuyaoni wala hata kuyasikia haya yakitendeka? Na je yapo sahihi kabisaa?

Najua maswali yangu ni mengi na pia yatawaudhi beneficiary wa mali hizo za umma na pia beneficiaries wa loophole hizo za biashara kwa upofu wa serkali na mashirika yake lakini ukitusaidia kujibu mawili matatu hapo juu binafsi utakuwa umekonga moyo wangu na ya watanzania wengi walio gizani

Tunaposema SU ama mali ya umma mtanzania aliyeko Mtwara anaechangia kodi yake anafaidika na kushiriki vipi kunapotokea sherehe hizi za uuzaji mali za UMMA kwa bei za kutupwa?ili nae ajione anapata mgao wa keki ya taifa?vinginevyo tunajenga tabaka la kusema vyao wanakula wao na vyetu tule wenyewe na kuleta migogoro isiyo na tija kama ya kuzuia ujenzi wa bomba la kusafirishia.ukichunguza sana vyanzo vyake ni kama hivi

Hizi sintofahamu na usiriusiri ukiwekwa wazi hatutalalamika.sijui kwa wanaUMMA wenzangu wanaionaje hii kwani mimi naiona imekaa vibaya

Many Thanks to Jamii forums WHERE WE DARE TO TALK OPENLY!
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom