Ni kweli kwamba watumishi wasiopitishia mishahara yao benki ya CRDB hawana nafasi ya mikopo katika benki hiyo?

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,992
1,197
Hili suala nimelisikia sehemu ndugu zangu wanajamii forum kwa mnaojua ukweli wa suala hili Basi mtujuze tusiojua vizuri.
 
Hiki wanachokileta CRDB ni kilio kwa wateja wao, haiwezekni ulazimeshe mkopo upitie CRDB. Ni aibu sana
 
CRDB anataka wateja mkuu. Ukicheka na nyani utavuna mabua, ki biashara yupo sahihi hutaki acha kakopa ulipo na account
Huo ni udikteta uchwara, sasa kila benk ikifanya hivyo hali itakuwaje? Bure kabisa
 
Yaani hao CRDB wanafanya hivyo ili wanufaike na zile transactions utakazozifanya baada ya kupata mkopo na wala si kingine. Mfano, umekopa unajenga nyumba, lazima utakuwa una-withdraw mara kwa mara ili kuendelea na ujenzi. Japo huwa wanakutana na wabishi ana-withdraw hata milion 20 anaziweka ndani anaanza kutekeleza mradi wake taratibu.

Rahisi sana kama hautaki mshahara wako upitie CRDB, sema ina usumbufu; Unafungua akaunti CRDB ili upate mkopo, na ukiishapata mkopo unaenda kwa afisa utumishi unabadilisha akaunti unarudi benk unayoipenda. Kwani tatizo liko wapi?

Kuna kipindi ni vyema kupuuzia usumbufu mwingine humu Tanzania!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
CRDB anataka wateja mkuu. Ukicheka na nyani utavuna mabua, ki biashara yupo sahihi hutaki acha kakope ulipo na account
kuna taasisi hujichagulii banki ya kupitishia mshahara.


halafu mbona kama ndio target yao hii haiathiriki na mshahara kupitia kwingine.zaidi wanajikosesha kibiashara,mabenki kibao yanakopesha kwa sasa wala kigezo hicho sio sababu.
 
kuna taasisi hujichagulii banki ya kupitishia mshahara.


halafu mbona kama ndio target yao hii haiathiriki na mshahara kupitia kwingine.zaidi wanajikosesha kibiashara,mabenki kibao yanakopesha kwa sasa wala kigezo hicho sio sababu.
Upo sahihi, kila bank ina mashart na vigezo vyake pia naamini bank kubwa kama CRDB wana idara ya tafiti na maendeleo hili itakuwa wameisha lifanyia kazi na wamekuja hivyo
 
Hivi crdb wamesha anza kutoa tena mikopo ya wafanyakazi!?wengine tuna miezi mitatu Sasa,hata hawana jibu la kueleweka
 
Back
Top Bottom