Ni kweli kenya wameleta treni ya umeme?

Ni kweli kenya wameleta treni ya umeme?

Train ya kwanza morocco.jpg
Mkuu sio kweli ni Kenya, hizi picha ni za Rabatt huko Morocco. Ingekua ni majirani hapa saa hizi hapakaliki humu JF
 
wakenya kama kawaida misifa sana,utasikia tena kenya nchi ya kwanza kutengeneza tren.mnakumbuka ishu ya laptop last month



Usiwe na wivu, wenzetu wanafanya kweli sie tulie na malighafi za kufa mtu eti tunanunua matreni ya wahindi tena yale ya 1908. Hii nchi kamwe haitaendelea chini ya CCM hata iweje.
 
Ingelikuwa ni Kenya ningefurahi sana wakuu, maana na sisi tungeona aibu angalau tukaboresha yetu ya kuni

Kweli mkuu wivu wa maendeleo ni mzuri sana. Niliona video youtube kuna mmarekani anazileta hizo Dar na mkataba washasaini. Sasa sijui ni kweli. Maana bongo kwa usanii, wao wanajengea midomo na kwenye makaratasi
 
Jaslaws, kwa taarifa yako wakamba ndio wanaoongoza kwa uchawi Africa nzima
 
Last edited by a moderator:
Inaonesha jinsi gani wananchi wanavyotamani vitu vizuri kama hivi na hawavipati.
 
Inaonesha jinsi gani wananchi wanavyotamani vitu vizuri kama hivi na hawavipati.

Hata viongozi wetu wanavitamani sana sema wao wanaenda kuvitumia huko huko na wakirudi hapa maneno meeengiiii
 
Spain imegubikwa na economic crisis, uchumi wake ni wa kusuasua miaka yote. Kwenye nchi zilizoendelea ni moja ya nchi zilizo nyuma kabisa kiuchumi, lakini ukija kwenye swala la usafiri acha kabisa. Wana hizi high class speed train za kisasa kabisa hata wamarekani wenyewe hawana.

Hapa nataka kusema, uchumi tulionao hata kama sio kuwa na high speed train lakini usafiri ulio bora na salama tusingeshindwa, kwani wao wamewezaje sisi tushindwe. Lakini Tanzania maneno mengi matendo hakuna, kila siku kulialia viongozi ni wala rushwa lakini wananchi wenyewe ndio wanaowaweka madarakani...Ukimuuliza mtu kwani walikushikia mtutu kuwachagua, jibu hapana, tuliwachagua ili kuwakomoa watu fulani.

Acha mi nikaongeze kikombe kingine cha kahawa!
 
Serial I kwa sasa inachojua wimbo mmoja tu kichwani mwake

Tumejipangaa!
Mwaka huu wataisomaa! ×2
 
Back
Top Bottom