Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
CCM imekamilisha kupanga timu ya kusaka kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Mabadiliko ya watendaji serikalini yanatarajiwa kufanyika hivi punde kwa lengo hilo hilo la kuvutia kura za wananchi.
Katika harakati zao hizo ni vyema wakazingatia ushauri ufuatao:
- Janga namba moja kuu litakalowakosesha kura nyingi ni hili tatizo la umeme. Linazidi kujenga chuki ya wananchi kila siku tatizo hili linapoendelea na hivyo kupeperusha kura. Linabidi limalizwe haraka. Angalao wananchi wangependa kuona kwamba mabadiliko ya watendaji serikalini yanayotarajiwa yanafanyika kwenye sekta/ wizara hii. Waliopo sasa hata kama ni wazuri lakini wananchi walishapoteza imani nao. Mambo mengine huwa ni ya kisaikolojia. Jitihada zinatakiwa si tu kufanyika bali kuonekana zinafanyika.
- Janga kuu la pili ni kupanda kwa bei ya mafuta (gasoline). Ni kweli kwamba jambo hili linatokana na vita ya Ukraine ambayo inaweza kuendelea kwa miaka kadhaa. Hata hivyo jambo hili lisipodhibitiwa haraka litapeperusha kura nyingi za wananchi. Imeshuhudiwa hata huko ulaya, jambo hili limesababisha mfululizo wa mabadiliko ya mawaziri wakuu hasa huko Uingereza. Mbinu mbali mbali zinaweza kutumika, pamoja na kutumia shirika letu la TPDC kununua mafuta hayo moja kwa moja toka Uarabuni au Urusi badala ya makampuni ya binafsi kama tunavyofanya sasa. Tusiogope kununua mafuta haya toka Russia ambako bei yake ni nafuu sana. China na India wanafanya hivyo. Hata ulaya magharibi wanaendelea kununua mafuta haya na gesi toka Urusi. Sisi kitu gani tunakiogopa?
- Jambo kuu la tatu ni mfumuko mkubwa wa bei hasa wa chakula. Wananchi haiwaingii kichwani wakiona chakula kikipelekwa Kenya na Somali wakati wao wakiwa hawana chakula cha kutosha. Kwani bei nzuri kwa wakulima wetu haiwezi kupatikana bila vyakula hivyo kupelekwa Kenya na Somali?
- Hili la wananchi kudhani ufisadi na rushwa imeongezeka halina shida kubwa.