Ni kweli hawa ni Watanzania wa kweli au ...

Kimbembe

Senior Member
May 14, 2006
122
15
Mimi Kimbembe
Leo nimekuja na hoja nzito inaweza kutugawa ama kusema no Kimbembe wewe mbaguzi lakini ni kweli kwamba nina haki ya kusema mawazo yangu na kusikia maoni yako. Mwa muda wa miaka 40 na zaidi ya Uhuru wa Tanzania tuan Watanzania wazalendo kama mimi na wewe na wazawa pia lakini pia tuna Watanzania wa uraia wa kununua ama kuomba .

Hawa wengi ni wahindi . Wahindi hawa wengi wanasema wamezaliwa Tanzania katika mikoa tofauti lakini wamekuwa muda wote wanaishi kama first class citizens.Wahindi hawa ama wahamiaji hawa hawana heshima na mtu mweusi mwenye Nchi yake .Soscial life yao imejengewa mipaka kwamba huwezi kuwakuta wako na Watanzania weusi wakila na kunywa , kucheka na kuolewa na ama kuoa hapana .

Mimi kwa muda nimekuwa najiuliza hawa watanzania wana shule zao na bado wana tutumikisha sisi Watanzania weusi wenye nchi yetu.Bado hawa wahindi ndiyo wanao ongoza kwa rushwa na kuungwa mkono na watanzania weusi yaani sisi wenye Nchi ambao hatukuomba ial Tanzania na Africa ni yetu .

Sisi ni wakarimu tunawapa hata Ubunge nk , ila wao hata misikiti yao ni yao na si zaidi ya hapo . Kibaya zaidi ni kwamba hata lugha ya Tanzania wengi hawaijui kabisaaaaa. Wao lugha yao ni Kiingereza na maneno machache ya kiswahil . Kuna Mtanzania Mhindi anafanaya kazi na daily News nadhani yuko Arusha huyu kwa miaka yote hii kukaa na hata kufanya kazi na gazeti la serikali lakini ukiseme naye baada habari , jambo asante mengine anasema hajui Kiswahili .

Je tuanze kuwapa mitihani ya Kiswahili wageni hawa na watanzania wa aina kabla hawajapewa Uraia wa Tanzania ?Maana kama u Mtanzania na hujui Kitanzania yaani Kiswahili sasa wewe ni Mtanzania wa aina gani ?

Naomba nitoe hoja .
 
Mzee Kimbembe,

Weka mawazo yako, huna haja ya kuomba radhi kwa mtu wala msamaha, weka vitu as long as hakuna matusi weka vitu, kama ni uongo tutakwenda kufanya RESEARCH na kukuweka sawa,

Usiogope mtu bro, weka vitu hapa!
 
mwanakijiji
Mtanzania ni nani ? Ina mana hujui Mtanzania ni nani ? Mtanzania si yule wa kununua Passport ama kusema naukataa Uhindi na usomali nataka Utanzania . Utanzania ni ule a kuzaliwa Tanzania kwenye mahospitali ya Kitanzania na kuishi Kitanzania kuanzia mila nk . Kuna wahindi walio zaliwa hapa tanzania sawa lakini they never value Mtanzania na utanzania mbali na kuutumia Utanzania kusema ni watanzania lakini wanatuona watanzani si lolote .
 
Mzee Shughuli, hili tulishalizungumza huko nyuma na mimi nikiwa ni miuongoni mwa watu wanaopinga vikali kumdefine Mtanzania kwa kutumia rangi yake. Kwangu mimi Mtanzania ni mtu yeyote yule ambaye aidha kwa kuzaliwa au kulelea anaitambua Tanzania kama nchi yake na kwa hiyo pekee ameweka utii wake. Tukianza kuchambua watanzania kwa misingi ya rangi, dini, nasaba n.k... hatutaishia kwa wahindi!!!
 
tatizo hapa nafikiri si jinsi ya kudefine nani ni mtanzania na nani si mtanzania,
tatizo hapa ni perception ya watu kuwa na feeling kuwa they are not treated justly!!
hatuwachukii au kuwakataa wahindi kwasababu ni wahindi, hapana ila tunachopinga ni ubaguzi na unyanyasaji wanaufanya dhidi ya watanzania wenzao tena kwenye nchi yao.
sisi waafrica tumesha suffer vya kutosha... from slavery to colonization to racial discrimination which is still today,not to mention about poverty and diseases,
we cannot afford these sufferings in our own country no way!!
serikali inatakiwa ichukue hatua kali dhidi ya ubaguzi au any injustice done to tanzanians.
naomba kuwakilisha.
 
quarz

Naongezea kwamba Mtanzania anaongea kiswahili , ana changamana na watanzania wenzake.Lakini wahindi si watu wa aina hii .Nimesema hapo wazi kwamba kwa nini kama ni kweli kazaliwa Tanzania na baada ya miaka yote asiweze kuongea kiswahili ? Hili ni kuliko yote utii wake lazima uanze na hili . Lugha ya nchi yako ndiyo mmojawapo ya Identity yako .

Wachilia mbali mateso na upuuzi mwingine kwa wausi hata mlango wa kuingia kazini , hata mahala pa kupumzikia nk yote haya yanafanyika Tanzania na wahindi wanabaki na uhindi wao Utanzania wa jina mbona si matendo ya kitanzania ? Again kwa nini wasiongee kiswahili ?
 
Vipi kuhusu yule Mtanzania aliyezaliwa Kigoma na anazungumza na kuelewa Kiha peke yake, au yule aliyezaliwa Tabora na anaelewa Kisukuma peke yake, na hachanganyiki na Watanzania wengine kwa sababu ya ugumu wa lugha ya Kiswahili, au mila tofauti? Je ni nusu Mtanzania?
 
Mzee Mwanakijiji said:
Vipi kuhusu yule Mtanzania aliyezaliwa Kigoma na anazungumza na kuelewa Kiha peke yake, au yule aliyezaliwa Tabora na anaelewa Kisukuma peke yake, na hachanganyiki na Watanzania wengine kwa sababu ya ugumu wa lugha ya Kiswahili, au mila tofauti? Je ni nusu Mtanzania?

Mzee Mwanakijiji nadhani unaelewa sana kinachoongelewa hapa ila unataka tu kuendeleza mjadala,which is not a bad thing.Mtoa mada anazungumzia "Utanzania" wa Wahindi,section of our "fellow Tanzanians" who hardly speak any Swahili,our beloved national language.Anazungumzia "Watanzania" wenzetu ambao tunapoelekea uchaguzi mkuu wanakimbilia Canada na kwingineko kuhofia vurugu huko "nyumbani"; anawazungumzia "Watanzania" ambao hata wanapoiba hawaendi jela,wanapougua wanakwenda kwenye hospitali zao maalum,wanawapatia watoto wao kwenye shule ambazo ni exclusive kwao tu,na fedha zao haziwekwi kwenye mabenki yetu bali huko nje ya nchi,na anazungumzia WATANZANIA WENYE URAIA WA INDIA,tanzania,na CANADA kwa wakati mmoja.

Ni kujidanganya kwamba eti hawa wababaishaji ni sawa na mie Mndamba au Msukuma,sio kwa vile tu nimezaliwa hapo bali I am proud of being born there,have the sense of belonging to that part,and ready to die for it.Magabacholi ni Watanzania wa "kuchonga" (feki) kwa vile hawana allegiance kwa nchi yetu.Acha niitwe m-baguzi lakini nawachukia magabacholi ambao licha ya kuwa chachu ya rushwa na ubadhirifu (ni wepesi sana kwa kutoa rushwa ili wapate wanachotaka) na kuendelea kuiharibu NCHI YETU bado wanatuletea dharau.To hell with those who might brand me a racist,but mie nina uchungu na nchi yangu zaidi ya Mhindi kutoka Bombay ambaye yuko mguu ndani mguu nje kwa vile tu ana uraia wa nchi mbili au tatu.
 
Mlalahoi, hivi Watanzania wengine weusi wote wanaipenda nchi yao? Je ni wote wamakua, warangi, wanyakyusa n.k ambao hawawadharau watanzania wenzao? Je ni watanzania wote weusi ambao hawatoi na kupokea rushwa ili wapate kila wanachotaka? Hivi ni Wahindi pekee wanaoiharibu nchi yetu? Ni kujidanganya kudhani kuwa kwa vile mtu ni mweusi basi ni mtanzania zaidi na anaipenda nchi yake zaidi! Hilo halijali mtanzania ni nani!

Kama tunataka kuzungumzia ubaguzi unaofanywa na wahindi dhidi ya watu weusi hilo linazungumzika...! Wakati watu weupe wa Marekani wanawabagua watu weusi hiko hakikuwaondolea Umarekani wao! Wakati kina Malcom X na wengine walipoanzisha jitihada za kusimama dhidi ya ubaguzi wa rangi "by any means necessary" hilo halikuwaondolea Umarekani wao! Lakini yote yale yalizungumzika! Watu weupe wakawezeshwa kuona ubaya wa njia zao na watu weusi vivyo hivyo! Na Marekani ikawa bora zaidi. Na tunajua hata hivyo bado kuna watu weupe ambao wanawadhihaki watu weusi kila siku. Na wapo watu weusi wanaowachukua watu weusi wenzao!!

Kwa upande wetu Tanzania, nitakuwa muongo na mzandiki nisipokiri kuwa Watanzania wenye asili ya uhindi wana kasumba ya kubagua watu weusi na kuwadharau, na wao kujiona bora. Lakini hilo haliwapunguzii Utanzania wao, linaonesha tu kuwa wanahitaji kueleweshwa kuwa kama Tanzania ni yao basi hawana budi kuipenda pamoja na watu wake wote! Na kushirikia katika raha na shida katika kuijenga nchi yetu. Na wapo wahindi waliofanya hivyo (labda wachache - lakini wapo)

Hata mimi najiuliza, ni Wahindi wangapi ambao watoto wao wameeingia katika ajira za jeshi la wananchi, polisi au magereza ambako ndiko chachu ya uzalendo inapandwa! Ningekuwa mimi nina uwezo, ningelazimisha kukaa chini na jumuiya ya wahindi na kuwaambia wazi kuwa kujitenga kwao hakujengi nchi! Kwa sababu hatari iliyopo ni kuwa pindi Tanzania itakapoanza kufanikiwa sana kiuchumi, Waasia hao wataanza kurejea Tanzania kwa wingi na kudai Tanzania ni nchi yao! Hilo linazungumzika.

Kuonyesha kosa la watu au kikundi cha watu katika jamii na kuwakosoa ili wajirekebishe kwa kutumia mantiki, siyo ubaguzi wa rangi. Kuwaona watu fulani ni duni, hawafai, waondoke, na wanyimwe haki fulani za kiraia kwa sababu tu ya rangi zao, huo ni ubaguzi na hauna nafasi katika Tanzania yetu. Binafsi, ni bora kuwa na Mhindi anayejali na kuheshimu watanzania wenzake, na kuisaidia kujenga nchi yake kwa kila namna, kuliko kuwa na mtu mweusi ambaye anajitahidi kuiingiza Tanzania katika mikataba mibovu, anakula rushwa kuuza madini yetu, na anatafuna pesa za serikali ubalozini kama mchwa! Ukinipa uchaguzi, nitachagua Mhindi!!!
 
Mwanakijiji
Naungana nawe kabisa. Hapa kuna baadhi wanachanganya mambo. Na bila shaka ni hisia za wivu na chuki without proper reasoning.Wanaoiua nchi hii ni watanzania weusi by all standards. Wahindi mnawasingizia tu.

Kwa nini wahindi wanaonekana kuwadharau watanzania weusi. Jibu lake ni kwa sababu sisi wenyewe watitu(weusi) tunawatukuza PERIOD!

Mtanzania ni yeyote mwenye pasipoti ya Tanzania au mwenye haki ya kupata hiyo pasipoti. Mijadala mingine hii inakula muda bure tu.
 
Ukisoma vyema utaona mwenye mada anauliza Utanzania ni passport na lugha ya Watanzania na Tanzania huiwezi kuisema ?Mengine yanafuatia tu
 
Wahindi ni the most racist nation on earth. Ila racism yao ni ngumu kwa mtu kuwa aware. Nakumbuka article moja aliyoandika Cynthia Stacey, ( mwandishi wa kike mwingereza ambaye nadhani kaolewa na Mtanzania) kama miaka 20 iliyopita kwenye gazeti la Daily News kuhusu Indian racism. Alifananisha na kupumua. Aliuliza kuwa huwa unafahamu kuwa unapumua?? Ni kama india racism. You're not aware of it but it is there, just like breathing. Niliipenda mno hiyo article ndio maana naikumbuka hata sasa!!
 
Kumbuka kuwa Wahindi jamii yao imejengwa na misingi ya mfumo wa caste.. ambapo watu wako katika ngazi mbalimbali za maisha! Ndiko huko tunapata mfumo wa half-caste. Wao wenyewe hawaoni kama hilo ni ubaguzi, wanaona ni sehemu ya dini yao. Rangi yetu kama weusi inaendana sana low caste people wa India na ninafikiri wamebeba hilo katika akili zao!
 
haya wa kunyumba nimesoma .Sasa issue ni race pekee na kuoana ? Lugha je maana kama ni Watanzania nini lugha yetu Tanzania jamani wanakaa hapa miaka kibao lakini hawajui kiswahili .Je tuanzishe utaratibu wa kuwasomesha kiswahili na kuwapa mitihani ama wazungu watakuja na human rights zao ?
 
Wazungu wenyewe mbona wameshtuka! hapa UK lazima upigwe paper na kimombo lazima kipande. Lazima mtu anayeomba uraia ajue values za nchi sio kuingia kichwa kichwa tu! Kwa mfano, UK wamekuja kushitukia misikiti imejaa maimamu wazee ambao wanapiga kiurdu kwenda mbele, kimombo zero! How can they keep track with burning issues of the society? matokeo yake wanajitenga na kung'ang'ania values za huko walikotoka!
 
Kwa sasa nadhani watu wameona nini maana ya Utanzania .Wahindi kibao wanajua maneno machache ya kiswahili na wachilia mbali wao kujitenga na sisi ni sawa pamoja na misikiti yao baso waongee lugha ya Tanzania ndipo walie na Passport zetu ama la Mambo ya ndani na Uhamiaji waziri peleka muswada tuanza Kiswahi test ama unasemaje na kila Mgeni sasa iwe ni kiswali kwa kwenda mbele na nyuma kuukata mzizi a fitina .Aklishindwa mtu ndege inayo fuata hii ni tanzania yetu .Kaka sisi wangoni tunaweza kingoni , Kimakonde na kiswahil vipi wageni hawa ? Hebu nani kafika India atueleze kama mweusi kama mimi na wewe tunaweza kupata maisha na kuwa valued na tuanze manyanyaso kama yao ? Manji mwizi mkubwa na bado anapapatikiwa na wasirikali kisa mjuzi wa kuhonga na pesa iko .Tanzania ni ya mweusi bwana hatukataki wageni lani wawe na heshima ama unasema wewe wa kwetu ?
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom