Ni kweli Harmonize hana milioni 500 ya kulipa Wasafi?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,704
Business as usual, but also data never lie!

Ni taarifa ya mkanganyiko na jamii imejigawa katika pande mbili kubwa. Moja likisema ana huo uwezo ila anatafuta tu public sympathy. La pili ni kundi la wapondaji. Hili linasema hana huo uwezo na zile show zake nyingi za misafara mirefu ni "kujimwambafy" tu ili aonekane matawi.

Wote hawa wana hoja lakini hoja zao zitaleta mashiko kama tu zikiwa na supportive data ambazo hata hivyo karibia wote hawanazo. Hivyo, mambo haya kubaki kama story za vijiweni huku kila upande ukichagua kuamini ama kutoamini kutokana tu na mitazamo, uelewa mapenzi binafsi na kufuata upepo.

Iko hivi, ukitaka kujua ukweli wa chochote, tafuta uhalisia wake kwenye data zake. Ulaya hakuna ku fake wala kudanganya. Unacho, unacho; huna, huna; full stop! Hawa wenzetu kila thumni yako inayoingia iko screened. Hivyo, wakiamua kutoa takwimu zako kama wakikosea ni kidogo mno, ndiyo maana wenzetu wana madaraja. Ukifikia daraja fulani la ukwasi utaambiwa uhame huko uliko, uende ukaishi panapokustahili.

Natambua kuna shobo za Kibongo. Mtu hana kitu lakini anavyojitutumua utadhani yeye ni Bill Gates. Na hii tabia iko sana kwa wasanii wa kaliba zote hapa Bongo. Sasa takwimu za mtu hupatikanaje ukiachana na zile tasilimu zilizoko benki kwenye kibubu?

1. MKOPO

Ni hulka ya wenye pesa wengi kutotaka kugusa cash yao bank. Hivyo, kama kuna mwanya wa kupata mkopo, basi atafanya hivyo. Sasa basi, afisa mikopo ukishajaza kiwango cha mkopo utakao atakuja kwako na maswali dodoso ili ajiridhishe kama kweli unastahili mkopo na baadhi ya maswali ni haya:

Kipato chako kwa siku na kwa mwezi
Matumizi yako kwa siku na kwa mwezi
Faida yako kwa kila bidhaa na kwa mwezi
Kipato cha ziada
Matumizi ya ziada
Familia na wategemezi
Starehe
Balance unayobaki nayo nknk

2. IDADI YA WAFANYAKAZI (Rasmi na wasio rasmi)

Ukishakuwa na watu kumi nje ya familia yako wanaokusaidia mishe zako tambua hapo unahudumia zaidi ya watu 30. Hivyo, ukwasi wako unaweza kujulikana hasa kwa idadi ya watu wanaokutegemea ndani na nje ya familia.

Kule kwa wenzetu kila mfanyakazi wako anastahili haki zote za mfanyakazi. Kibongo bongo hakuna hiyo. Sometimes ni kutoana tu kibingwa lakini kama ni kwenye biashara ama kiwanda. Pato lako linaweza kujulikana kirahisi kabisa.

3.UWEKEZAJI

Hapa utaangaliwa una miliki mini na umewekeza kwenye nini kuanzia biashara, majumba, ardhi magari n.k. Hivi vyote vikipigiwa thamani yake, utajulikana tu.

4. UZALISHAJI

Kwa msanii utaangalia show na kiasi anacholipwa, lakini pia kuna matangazo n.k. Lakini mfano unaoelezeka zaidi ni mchanganuo wako wa uzalishaji. Hili mamlaka ya mapato wanaliwezea sana hili.

Nikupe mfano rahisi wa bakery ya mikate. Mapato yako halisi yanaweza kujulikana hata kama ukidanganya. Kwa mfano ukisema kwa siku unaingiza million kumi, jamaa wataingia kazini na kuangalia yafuatayo:

Idadi ya wafanyakazi
Kiasi cha maji unachotumia kwa siku
Mafuta ya magari
Umeme
Malighafi kama unga wa ngano, hamira, baking powder n.k. Hivi vyote vitaangaliwa idadi yake kwa siku. Vyote hivi vikikokotolewa utajulikana kama umeongopa ama la.

Hivyo basi, kupima utajiri wa mtu si lelemama ni kazi inayohitaji ujuzi na umakini.
Tukirudi kwa Harmonize sasa, anasisitiza sana biashara.. Kwahiyo ABC za biashara ameshaanza kuzijua. Kiuhalisia hakuna mtu mgumu kulipa pesa isiyo na faida kama mfanyabiashara. Harmomize anaweza kabisa asishindwe kulipa milion mia 5, lakini inamuuma kutoa cash. Hata wafanyabiashara wakubwa kabisa wasingeweza kufanya hivyo. Hii ni kanuni ya asili.

Kwahiyo, ni afadhali auze kitu ndio kilipie deni kuliko kutoa cash. Kuuza nyumba zake tatu ni biashara tena yenye faida. Nyumba zinajengwa ardhini na ardhi haishuki thamani. Hakuuza kwa dharura hivyo kafanya biashara yenye faida.

Yote juu ya yote, kujua ukwasi wa mtu si mavazi wala show na shobo za mitaani - ni DATA!

Kwaiyo Mr mshana unataka tuambia hawa vijana wanajimwambafai mwambafai tu kuwa wana pesa za mziki kumbe hakuna kitu eti

ipo siku tu wataotewa ndio tutajua kati ya mziki na ngada ipi inawalipa, maana tukiwaita uku kolomije wapige shows pesa wanayoitaji eti million 50 sasa unawaza hiyo milion 50 itarudije kijiji kama kolomije

Tushawajua biashara zao mjini ipo siku itafahamika tu achana wandeleee kuzuga na mziki
 
Hapana maana yangu ni kwamba bila data kamili hatuwezi kumhukumu Harmomise kama ana uwezo wa kulipa milion 500 ama la.. Je anazuga tu au kuna uhalisia?

jamaa unaomba kazi kijanja kweli kwa harmonize.
 
Kwaiyo Mr mshana unataka tuambia hawa vijana wanajimwambafai mwambafai tu kuwa wana pesa za mziki kumbe hakuna kitu eti

ipo siku tu wataotewa ndio tutajua kati ya mziki na ngada ipi inawalipa, maana tukiwaita uku kolomije wapige shows pesa wanayoitaji eti million 50 sasa unawaza hiyo milion 50 itarudije kijiji kama kolomije

Tushawajua biashara zao mjini ipo siku itafahamika tu achana wandeleee kuzuga na mziki
Hahahaha we jamaa unaakili sana,Mfano kale ka Sheta!!eti nako kanapesa za show kutokana na music. Biashara hii bana
 
Back
Top Bottom