Ni kweli CORONA ni hatari tena hatari sana tuunganeni na Amiri jeshi mkuu wetu kwenye hii Vita kila mmoja wetu awe chachu ya Mabadiliko be the change

Corticopontine

JF-Expert Member
Sep 20, 2019
664
1,272
Ni kweli tangu nijitambue hapa Duniani kwa kuwa na ufahamu sijawahi kuona hofu kama hii inapamba moto Duniani, inaitisha DUNIA kiasi hiki kweli hofu imetawala lakini lazima tuishinde

Nawaombeni vijana wa kitanzania huu si wakati wa kuimba nyimbo za vyama, dini, hadhi au kabila huyu mdudu ni adui yetu hana utani, amedhamiria kutumaliza tusikubali lazima tupambane kumshinda lazima tushinde kwa kuchukua tahadhari

Kila mmoja wetu awe mwanamabadiliko tuwahimize wasioelewa waelewe umuhimu wa kufuata kanuni na Taratibu za afya

Viobgozi wa Dini huu ndio mda wa kuwahubiri waumini wenu njia za kuchukua hatari tusikubali huyu mdudu atuangamize anatisha

Huyu ni ibilisi mtoa roho amekuja kwa mtindo wa Virus tupambaneni kumuondosha

Tuunganeni na Rais wetu kutii sheria kanuni na matumizi ya njia za kitaalamu

Watanzania wenzangu nawaombeni kila mmoja achukue tahadhari Vita bado ni kubwa tupambaneni tena bila kuchoka adui ana nguvu za kutisha tuunganeni kumuangamiza
 
Vijana wa kitanzania wanawaza vyama na siasa kosa wamuunge mkono rais wao kwenye mapambano yamekalia kubishana

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Watu wanataka total lockdown ukiwafungia watanzania ndani wiki moja unazika wengi kuliko ambao wangekufa kwa corona yenyewe,

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni bora tuuze ndege tupate fedha za kuhudumia wananchi chakula wakati wa total lockdown
Kwa sasa hivi corona ilivtopamba moto mandege hayana faida yeyote .
Korona ikiisha tutanunua mengine kama italazimu
 
Binafsi nawaza tungekua na lugha moja kama Taifa, sasa huku tunasema hivi, ukirudi kwa Mwenyekiti anasema tuchape kazi, spika anahubiri hicho hicho, Polisi nao wanaimba wimbo huo huo.

Kwa sababu hoja inakua imetolewa na mpinzani basi hskuna mtu wa CCM ataunga mkono. Huu ni ujinga na tutakufa. Martin Luther King Jr aliwahi kusema hivi, We must learn to live like Brothers or we will perish like fools.
 
Attachments

  • IMG-20200331-WA0074.jpg
    IMG-20200331-WA0074.jpg
    47.8 KB · Views: 2
Binafsi nawaza tungekua na lugha moja kama Taifa, sasa huku tunasema hivi, ukirudi kwa Mwenyekiti anasema tuchape kazi, spika anahubiri hicho hicho, Polisi nao wanaimba wimbo huo huo.

Kwa sababu hoja inakua imetolewa na mpinzani basi hskuna mtu wa CCM ataunga mkono. Huu ni ujinga na tutakufa. Martin Luther King Jr aliwahi kusema hivi, We must learn to live like Brothers or we will perish like fools.
Rais wa wanyonge yuko holiday Chato amewaacha wanyonge wapambane na corona kwanza.
 
Ni bora tuuze ndege tupate fedha za kuhudumia wananchi chakula wakati wa total lockdown
Kwa sasa hivi corona ilivtopamba moto mandege hayana faida yeyote .
Korona ikiisha tutanunua mengine kama italazimu
Akili za wapi hz
 
Akili za wapi hz
Akili za kawaida tu watu kibao wanauza hadi nyumba ili kutatua matatizo ya kesi au magonjwa , mali zitatafutwa baadae ila uzima ukishaondoka hauwezi kuutafuta tena, sasa kwa mfano katika kipindi hiki hizo ndege zina faida gani kwa nchi ?, nyie ndio mnaweza acha watoto wafe kwa njaa wakati una dhahabu umeitunza kabatini
 
Nan anataka ndege saiz safari zote zimekufa,bei za mafuta zimeshuka,utalii chali.Uchumi unapumulia mashine.Think bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom