Ni kwanini watanzania bara wanachukia kuitwa wana visogo, kwanini tusiwe proud na jinsi tulivyo ?

Ni kwanini watanzania bara wanachukia kuitwa wana visogo, kwanini tusiwe proud na jinsi tulivyo ?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
Ni kwanini tukasirike badala ya kujivunia tulivyo?

Watanzania, wanaume kwa wanawake, mara nyingi tunaonekana kukasirika sana tukitajwa kuhusu maumbile yetu, kama vile kuitwa tuna visogo. Lakini tukijiuliza kwa utulivu, kuna ubaya gani kuwa hivi tulivyo ?

Kujipenda ni kukubali kila sehemu ya mwili wako bila aibu. Kama una kisogo, hicho ni sehemu ya upekee wako. Hakikupunguzii thamani, wala hakibadilishi utu wako.

Badala ya kuchukulia maneno kama mashambulizi, tunaweza kubadili mtazamo wetu. Maneno yana nguvu tu pale tunapoyapa nafasi ya kutuumiza. Ukijiamini na kujikubali, hakuna neno litakalokutikisa.

Tumeshazoea kuona vitu hivu kwa baadhi ya wanawake wakichukia walivyo na kutaka kuwa kama watu engine, mfano nywele zao natural huzificha kwa kuvaa mawigi, kuzishonea weave au kuzisukia rasta, wana inferiority complex, lakini mwanaume mtu mzima kabisa unajijua una kisogo, unachukua nini sasa ukiitwa unacho ?

Tujifunze kujivunia maumbile yetu ya asili, nywele zetu, maumbo yetu, na kila kinachotutofautisha. Hapo ndipo tunapopata uhuru wa kweli wa kuwa sisi wenyewe.

Yani mtu akiniita nina kisogo au hata chogo anappoteza muda wake tu ni sawa na kuniita nina kiwiko, mkono, mdomo, n.k. sina haja ya kuanza kumuita ana kichwa flat, mviringo, n.k.

Jivunie ulivyo. Hiyo ndiyo nguvu yako.
 
Back
Top Bottom